R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,178
Shule hizi kwa miji ya Arusha na Moshi zipo kama International School of Moshi, Arusha Meru international school, Sunflower international school, ccis, Tanganyika schools, Jaffery academy, Braeburn, Kennedy House, St Constantine, n.k.
Shule hizi kwa nchi nzima zinaweza zisifike 30, Kwa Dar jiji kuu zipo kama 15 hivi, inayofahamika zaidi ni Internationa school of Tanganyika ada milioni 85 ila imejaa Foreigners maana hata bei tu imekaa kwa wageni pengine wasiojua kuna shule zingine za nusu bei. ukiachana na Dar, sehemu pekee yenye idadi ya kuridhisha ya hizi shule ni katika miji inayokaribiana kama pua na mdomo ya Arusha na Moshi, nje ya hapo ni nadra sana kuzikuta kwengine, Mwanza ipo Isamilo International na Mwanza international. Iringa ipo iringa international, Morogoro ipo Morogoro international.
Ni shule zenye mifumo yao inayofanana, hata uende Marekani ama nchi za Ulaya kuna shule za serikali na private ambazo watoto wengi huenda lakini huwa kuna international schools za wachache tu (ni gharama kubwa ) zinafuata mfumo moja bila kujali nchi, hata mtu anesoma international school huko Marekani akihamia leo Tanzania, kesho anaendelea na shule, hapa Tanzania hawaingiliani na Necta iwe ni mitihani, Likizo, masomo, n.k. Mtaala wanaotumia ni Cambridge unatambulika dunia nzima, ni rahisi kupenya vyuo vizito kama Havard na hawaombwi mambo mengi linapokuja suala la kuapply vyuo na ni rahisi kusoma hata kwa kufadhiliwa (scholarships). Hizi shule zilizojaa hapa hapa bongo kama saint mary wameongezea neno "internatinal school" nadhani huwa ni fasheni tu maana hazikidhi vigezo.
hizi shule huwa zinajaa watoto wa mabalozi wa nchi za ulaya wanaolipiwa na bajeti za serikali zao lakini nje ya hapo mzazi inabidi awe na mpunga wa maana, exposure na uwe mwamko wa kielimu. hapa wazazi wengi wanaosomesha huku huwa ni matajiri wa kizungu, wahindi na waarabu mfano kina Mo na bakhresa, n.k. lakini pia katika darasa la wanafunzi 20 wanaweza kuwepo wanafunzi wanne wenye asili ya hapa kwetu na mara nyingi huwa ni watoto wa matajiri wa hukohuko Moshi waliojaa pia Arusha, wengine walishasomeshwa na wazazi hizo shule nao wamekuwa wakubwa wanasomesha huku watoto, nimeshuhudia pia huwa kuna nafasi chache sana kwenye shule hizi kusomesha watanzania bure, ni watu wa hukohuko wanapigia connection aidha watoto wao ama ndugu zao.
Wanafunzi wa hizi shule tangu watoto lugha za Kiingereza, Kifaransa, n.k, huwa ni kama kunywa maji, najua kuna hizi english medium za bei nafuu ila huku kiingereza ni kile cha kufundishwa kuandikia essay, kusomea vitabu, kujibia mitihani ama kutoa speech ambayo ilishaandikwa, lafudhi ya hizi shule za english medium imekazwa sana imekaa kibantu bantu, kutamka neno "the" mtu anasema "ze", temperature akiitamka anakaza sana ulimi, na ndio mana hata walimu wa hizi shule wanapata wakati mgumu wakikutana na mzungu wa marekani ama uingereza, ukitaka kuamini nachosema muite mwanafunzi wa hizo english medium muwekee mziki hata wa chris brown aandike mashairi yote mpe hata dakika 10 arudie rudie, akimaliza ingia google usechi hayo mashairi anza kumsahisha.
Wengi wakimaliza shule wanapata njia nyepesi kuingia moja kwa moja vyuo vikubwa kidunia kama Havard, Oxford, Cambridge, n.k. huku wanazidi kuongeza connection na uzito wa status.
wakihitimu vyuo wanapata wepesi wa kuaminiwa na mashirika ya Kimaifa kama UN, UNHCR, UNICEF, connection huwa zinawasaidia sana lakini pia hizi shule mtu anaweza awe na uwezo wa kawaida darasani lakini anazungumza lugha tatu tofauti na zote ni kimataifa, chuo kasoma huko oxford, field kafanya mashirika makubwa huko ulaya na marekani, hapa kupenya inakuwa fasta. na sidhani kama kuna hasara endapo mtoto akisoma shule hizi na akaja kupata ulaji hapa hapa Tanzania sehem kama benki kuu, bandarani, ikulu, tanapa, n.k.
Watanzania wengi huwa tukiona mtu kwao wakiwa na utajiri wa kipimo flani mfano familia ina biashara za kuwafanya wawe wanatembelea v8 na range tunaanza kuwaita mambo safi na pengine mtu wa familia hio anaridhika lakini mtoto akienda hizi shule akipata exposure ya kuwajua wenzake wahindi, waarabu na wazungu anaona wenzake kwao zipo Ferarri, Lambogini, n.k, anaanza kujiona ule utajiri wa nyumbani ambao wabongo tunauita mambo safi, si kitu kwa familia za marafiki zake, hii itampa moto wa kutaka kuimarisha zaidi biashara ya familia iwe hata kimataifa, kama mihogo walikuwa wanawauzia wahindi elf 10 lwa debe wao wanaenda kuuza laki 2 huko ulaya, connections zinaweza kumsaidia ajue namna ya kuuza moja kwa moja ulaya.
Pia kupata mambo kama connections za wawekezaji inakuwa rahisi pamoja na kupata idea mpya za biashara. mfano kama huyu Fenandes mwenye App ya Nala wabongo wengi tulimshangaa anakataa mshahara wa milioni 40 kila mwezi kumbe jamaa kapitia hizi shule ashapata exposure na connections, Leo hii ana app yake ya kawaida tu lakini mara kwa mara utasikia kapata wafadhili wamemwaga pesa, kapewa ruzuku, kampuni yake imeshinda kitu flani imezawadiwa pesa, n.k. ujue nyuma ya pazia jamaa anatumia exposusure na connections zake kufanikisha hizi mambo, sio bahati.
Tukatae tukubali connection na exposure ni kitu kikubwa sana kwenye maisha, Kama huna connection au exposure sio kwamba hutafanikiwa, unaweza ukafanikiwa ila either kwa kutumia nguvu kubwa sana au uwe mtu wa bahati sana