Shule hizi zimejaa Arusha na Moshi kama vile; International School of Tanganyika, International School of Moshi, Braeburn, Kennedy House, St Constantine, n.k.
Kwa hizi shule huwa zinajaa Wazungu, wahindi, waarabu, wakorea, n.k. lakini pia kuna jamii fulani ya watu wa huko Moshi (waliojaa pia Arusha) huwa wanasomesha watoto wao na nimeshuhudia zile nafasi chache za kudhamini kuwasomesha Watanzania bure wanawekana wao.
Hata huko mbele Ulaya matajiri , wanasiasa, wafalme, n.k. wanapeleka watoto wao aina hizi za shule. Ni shule ambazo zina mitaala yao ila kwakweli huku connections, kujua lugha, exposure, n.k. ndio muhimu.
Niseme tu ya kwamba hizi shule zina potential kubwa sana kwenye masuala ya ajira, biashara, kujenga connection na maendeleo kwa ujumla.
Wanafunzi wengi wa hizi shule pindi wakiwa wadogo tu lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, n.k, huwa ni kama kunywa maji.
Wengi wakimaliza shule wanapata njia nyepesi kuingia moja kwa moja vyuo vikubwa kidunia kama Havard, Oxford, Cambridge, n.k. huku wanazidi kuongeza connection na uzito wa status.
wanapata wepesi wa kuaminiwa na mashirika ya Kimaifa kama UN, UNHCR, UNICEF, connection na kujuana na wenzao watoto wa wazito wa nchi mbalimbali zinawasaidia sana hapa, sidhani kama kuna hasara endapo mtoto akisoma shule hizi na akaja kupata ulaji TANAPA,TPDC,BOT,TPA.
Kibiashara hasa biashara za familia inasaidia pia, Watanzania wengi huwa tukiona mtu kwao wakiwa na utajiri wa kipimo flani mfano familia ina biashara za kuwafanya wawe wanatembelea v8 na range tunaanza kuwaita mambo safi na pengine mtu wa familia hio anaridhika lakini mtoto akienda hizi shule akipata exposure ya kuwajua wenzake wahindi, waarabu na wazungu anaona wenzake kwao zipo Ferarri, Lambogini, n.k, anaanza kujiona ule utajiri wa nyumbani ambao wabongo tunauita mambo safi, si kitu kwa familia za marafiki zake, hii itampa moto wa kutaka kuimarisha zaidi biashara ya familia iwe hata kimataifa, kama mihogo walikuwa wanawauzia wahindi elf 10 lwa debe wao wanaenda kuuza laki 2 huko ulaya, connections zinaweza kumsaidia ajue namna ya kuuza moja kwa moja ulaya.
Pia kupata mambo kama wawekezaji, hizi huwa washajenga utandu wa comnections inakuwa rahisi pamoja na kupata idea mpya za biashara.