Hata huko mbele Ylaya matajiri na wanasiasa wanapeleka watoto wao aina hizi za shule. Ni shule ambazo zina mitaala yao ila kwakweli huku connections, kujua lugha, exposure, n.k. ndio muhimu.
Shule hizi zimejaa Arusha na Moshi kama vile; International School of Tanganyika, International School of Moshi, Braeburn, Kennedy House, St Constantine, n.k.
Kwa hizi shule huwa zinajaa Wazungu lakini pia kuna jamii fulani ya watu wa huko Moshi (waliojaa pia Arusha) huwa wanasomesha watoto wao na nimeshuhudia zile nafasi chache za kudhamini kuwasomesha Watanzania bure wanawekana wao.
Niseme tu ya kwamba hizi shule zina potential kubwa sana kwenye masuala ya ajira, biashara, kujenga connection na maendeleo kwa ujumla.
Watanzania wengi huwa tukiona mtu kwao wakiwa na utajiri wa kipimo flani mfano familia ina gari kama V8 tunaanza kuwaita mambo safi na pengine mtu wa familia hio anaridhika lakini mtoto akienda hizi shule akipata exposure ya kuwajua wenzake wahindi, waarabu na wazungu anaona wenzake kwao zipo Ferarri, Lambogini, n.k, anaanza kujiona ule utajiri wa nyumbani ambao wabongo tunauita mambo safi, si kitu kwa familia za marafiki zake, hii itampa moto wa kutaka kuinua zaidi status ya huko kwao.
Wanafunzi wengi wa hizi shule pindi wakiwa wadogo tu lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, n.k, huwa ni kama kunywa maji.
Mchanganyiko wao na matabaka mengine unasaidia sana wawe na exposure kubwa sana kuliko hata mwanafunzi wa Feza, ama St. Francis ama Makongo.
Wengi wakimaliza hizi shule hupata kazi katika mashirika ya kimataifa kama UN, UNHCR, WHO, SADC, Google, Microsoft, n.k.
Pia kupata mambo kama wawekezaji, hizi huwa washajenga utandu wa comnections inakuwa rahisi pamoja na kupata idea mpya za biashara.