Tusiwabeze wanaosomesha watoto shule za Tsh. Milioni 40

Tusiwabeze wanaosomesha watoto shule za Tsh. Milioni 40

View attachment 2697860

Shule hizi kwa miji ya Arusha na Moshi zipo kama International School of Moshi, Arusha Meru international school, Sunflower international school, ccis, Tanganyika schools, Jaffery academy, Braeburn, Kennedy House, St Constantine, n.k.

Shule hizi kwa nchi nzima zinaweza zisifike 30, Kwa Dar zipo nyingi, inayofahamika zaidi ni Internationa school of Tanganyika ada milioni 85 imejaa wazungu, waarabu na wahindi ngumu sana kukuta mtz wa asili, lakini ukiachana na Dar, sehemu pekee yenye idadi ya kuridhisha ni katika miji inayokaribiana ya Arusha na Moshi, nje ya hapo ni nadra sana na zipo mikoa michache tu, Mwanza ipo Isamilo International na Mwanza international. Iringa ipo iringa international, Morogoro ipo Morogoro international.

Ni shule zenye mifumo yao inayofanana, hata uende Marekani ama nchi za Ulaya kuna shule za serikali na private ambazo watoto wengi huenda lakini huwa kuna international schools za wachache tu (ni gharama kubwa ) zinafuata mfumo moja bila kujali nchi, hata mtu anesoma international school huko Marekani akihamia leo Tanzania, kesho anaendelea na shule, hapa Tanzania hawaingiliani na Necta iwe ni mitihani, Likizo, masomo, n.k. Mtaala wanaotumia ni Cambridge unatambulika dunia nzima, ni rahisi kupenya vyuo vizito kama Havard na hawaombwi mambo mengi linapokuja suala la kuapply vyuo na ni rahisi kusoma hata kwa kufadhiliwa (scholarships)

hizi shule huwa zinajaa watoto wa mabalozi wa nchi za ulaya wanaolipiwa na bajeti za serikali zao lakini nje ya hapo mzazi inabidi awe na mpunga wa maana, hapa wazazi wengi huwa matajiri wa kizungu, wahindi na waarabu wanaoishi hapa Tanzania mfano kina Mo na bakhresa, n.k. lakini pia kuna matajiri wa Moshi waliojaa pia Arusha wenye mwamko wa kielimu huwa wanasomesha watoto wao huku, wengine walishasomeshwa hizo shule wanaendeleza utamaduni kusomesha watoto wao, nimeshuhudia pia huwa kuna nafasi chache sana za kudhamini kusomesha watanzania bure, huwa wanawapigia connection watoto wao ama ndugu zao.

Wanafunzi wa hizi shule tangu watoto lugha za Kiingereza, Kifaransa, n.k, huwa ni kama kunywa maji, najua kuna hizi english medium za bei nafuu ila huku kiingereza ni kile cha kufundishwa kuandikia essay, kusomea vitabu, kujibia mitihani ama kutoa speech ambayo ilishaandikwa, lafudhi ya hizi shule za english medium imekazwa sana imekaa kibantu bantu, kutamka neno "the" mtu anasema "ze", temperature akiitamka anakaza sana ulimi, na ndio mana hata walimu wa hizi shule wanapata wakati mgumu wakikutana na mzungu wa marekani ama uingereza, ukitaka kuamini nachosema muite mwanafunzi wa hizo english medium muwekee mziki hata wa chris brown aandike mashairi yote mpe hata dakika 10 arudie rudie, akimaliza ingia google usechi hayo mashairi anza kumsahisha.

Wengi wakimaliza shule wanapata njia nyepesi kuingia moja kwa moja vyuo vikubwa kidunia kama Havard, Oxford, Cambridge, n.k. huku wanazidi kuongeza connection na uzito wa status.

wakihitimu vyuo wanapata wepesi wa kuaminiwa na mashirika ya Kimaifa kama UN, UNHCR, UNICEF, connection huwa zinawasaidia sana lakini pia hizi shule mtu anaweza awe na uwezo wa kawaida darasani lakini anazungumza lugha tatu tofauti na zote ni kimataifa, chuo kasoma huko oxford, field kafanya mashirika makubwa huko ulaya na marekani, hapa kupenya inakuwa fasta. na sidhani kama kuna hasara endapo mtoto akisoma shule hizi na akaja kupata ulaji hapa hapa Tanzania sehem kama benki kuu, bandarani, ikulu, tanapa, n.k.

Watanzania wengi huwa tukiona mtu kwao wakiwa na utajiri wa kipimo flani mfano familia ina biashara za kuwafanya wawe wanatembelea v8 na range tunaanza kuwaita mambo safi na pengine mtu wa familia hio anaridhika lakini mtoto akienda hizi shule akipata exposure ya kuwajua wenzake wahindi, waarabu na wazungu anaona wenzake kwao zipo Ferarri, Lambogini, n.k, anaanza kujiona ule utajiri wa nyumbani ambao wabongo tunauita mambo safi, si kitu kwa familia za marafiki zake, hii itampa moto wa kutaka kuimarisha zaidi biashara ya familia iwe hata kimataifa, kama mihogo walikuwa wanawauzia wahindi elf 10 lwa debe wao wanaenda kuuza laki 2 huko ulaya, connections zinaweza kumsaidia ajue namna ya kuuza moja kwa moja ulaya.

Pia kupata mambo kama connections za wawekezaji inakuwa rahisi pamoja na kupata idea mpya za biashara. mfano kama huyu Fenandes mwenye App ya Nala wabongo wengi tulimshangaa anakataa mshahara wa milioni 40 kila mwezi kumbe jamaa kapitia hizi shule ashapata exposure na connections, Leo hii ana app yake ya kawaida tu lakini mara kwa mara utasikia kapata wafadhili wamemwaga pesa, kapewa ruzuku, kampuni yake imeshinda kitu flani imezawadiwa pesa, n.k. ujue nyuma ya pazia jamaa anatumia exposusure na connections zake kufanikisha hizi mambo, sio bahati.
Andiko murua kabisa.... ndo mana mimi nna suruali mbili tuu ili wanangu wasome private school kwakuanzia 🙏
 
Mshahara wa NAPE aufiki zaidi ya 15m mpaka marupurupu pamoja na uwaziri wake hata akimpokea rais wa US kama mfukoni hakusomi vyema .Kuna mashirika hapa Tz yanalipa mpaka 15-40m na ni mtu wa kawaida tu ila ana exposure kubwa sana
Kwenye maisha huna exposure utakosa vitu vingi sana ndo maana watanzania wengi waafrika kinachowafelisha hawana exposure
 
Kwahiyo ukienda shule zenye mitaala ya Cambridge HAKUNA watu wengine, Ni wachagga tu??

Kampuni gani za ndege, sema tu Precision. Haya makampuni yana Siri zake. Kwahiyo Fastjet ilikuwa inamilikiwa na Masha msukuma??

98% ya wachagga bado wachuuzi tu na biashara za Bar.

Uchumi wa nchi hii unamilikiwa na Wahindi.

=====

DAR = wote.

Dodoma = Shabiby + Gulamali

Shinyanga = Jambo.

Iringa = Asas

Morogoro = Abood.

Tanga = Binslum.

Singida = Mo Dewji.

Ninyi kazi yenu kubweka bweka na vibiashara vyenu vya Bar, maduka ya bidhaa za wizi na wizi serikalini.
Wachaga walikufanyaje,
 
Mtu akiweza kusomesha mtoto hizo shule kimsing maisha kashayamudu kiuchumi hata miaka 50+ ijayo. Hana haja ya connections wala nn, fursa zitamfuata yeye alipo.
 
Mtu akiweza kusomesha mtoto hizo shule kimsing maisha kashayamudu kiuchumi hata miaka 50+ ijayo. Hana haja ya connections wala nn, fursa zitamfuata yeye alipo.
Ishu ni kutoridhika na kuyamudu maisha, inabidi watoto wawe zaidi ya ulipo, kufikiria nje ya box,

Unaweza ukawa na connections na deals hapa bongo unaingiza milioni 100 kila mwezi ila kuna vitu ukicheki kama lugha za kimataifa, exposure, connections za nje, unakuta huna. hapa ndio inabidi upeleke watoto hizo shule.
 
Hakuna tofauti yeyote kati ya st Constantine na braeburn, wote wanafanya Cambridge curriculum. Hata Ada wametofautiana sio pakubwa ki hivyo. Na wasiwasi kama unauelewa mpana kuhusu hizi shule ungekuwa nao usingesema mtoto mmoja wa Braeburn anasomesha watoto 10 wa St Constantine. Upande wa IST ni kweli wanafanya mfumo tofauti kidogo na huu wa Cambridge ndio maana bei zao zipo juu kuliko shule zingine za Cambridge .
NB sio kila mnayemuona anakaa arusha ama moshi ni mchaga. Take a chill pill ...

Kavae 2nd🥸🥸🥸 usome vizuri tofauti ya hizo school fees hacha kujipa Moyo, hiyo ni sawa na kusema Gucci na Zara ni sawa 🥵🥵
 
View attachment 2697860

Shule hizi kwa miji ya Arusha na Moshi zipo kama International School of Moshi, Arusha Meru international school, Sunflower international school, ccis, Tanganyika schools, Jaffery academy, Braeburn, Kennedy House, St Constantine, n.k.

Shule hizi kwa nchi nzima zinaweza zisifike 30, Kwa Dar jiji kuu zipo kama 15 hivi, inayofahamika zaidi ni Internationa school of Tanganyika ada milioni 85 ila imejaa Foreigners maana hata bei tu imekaa kwa wageni pengine wasiojua kuna shule zingine za nusu bei. ukiachana na Dar, sehemu pekee yenye idadi ya kuridhisha ya hizi shule ni katika miji inayokaribiana kama pua na mdomo ya Arusha na Moshi, nje ya hapo ni nadra sana kuzikuta kwengine, Mwanza ipo Isamilo International na Mwanza international. Iringa ipo iringa international, Morogoro ipo Morogoro international.

Ni shule zenye mifumo yao inayofanana, hata uende Marekani ama nchi za Ulaya kuna shule za serikali na private ambazo watoto wengi huenda lakini huwa kuna international schools za wachache tu (ni gharama kubwa ) zinafuata mfumo moja bila kujali nchi, hata mtu anesoma international school huko Marekani akihamia leo Tanzania, kesho anaendelea na shule, hapa Tanzania hawaingiliani na Necta iwe ni mitihani, Likizo, masomo, n.k. Mtaala wanaotumia ni Cambridge unatambulika dunia nzima, ni rahisi kupenya vyuo vizito kama Havard na hawaombwi mambo mengi linapokuja suala la kuapply vyuo na ni rahisi kusoma hata kwa kufadhiliwa (scholarships). Hizi shule zilizojaa hapa hapa bongo kama saint mary wameongezea neno "internatinal school" nadhani huwa ni fasheni tu maana hazikidhi vigezo.

hizi shule huwa zinajaa watoto wa mabalozi wa nchi za ulaya wanaolipiwa na bajeti za serikali zao lakini nje ya hapo mzazi inabidi awe na mpunga wa maana, exposure na uwe mwamko wa kielimu. hapa wazazi wengi wanaosomesha huku huwa ni matajiri wa kizungu, wahindi na waarabu mfano kina Mo na bakhresa, n.k. lakini pia katika darasa la wanafunzi 20 wanaweza kuwepo wanafunzi wanne wenye asili ya hapa kwetu na mara nyingi huwa ni watoto wa matajiri wa hukohuko Moshi waliojaa pia Arusha, wengine walishasomeshwa na wazazi hizo shule nao wamekuwa wakubwa wanasomesha huku watoto, nimeshuhudia pia huwa kuna nafasi chache sana kwenye shule hizi kusomesha watanzania bure, ni watu wa hukohuko wanapigia connection aidha watoto wao ama ndugu zao.

Wanafunzi wa hizi shule tangu watoto lugha za Kiingereza, Kifaransa, n.k, huwa ni kama kunywa maji, najua kuna hizi english medium za bei nafuu ila huku kiingereza ni kile cha kufundishwa kuandikia essay, kusomea vitabu, kujibia mitihani ama kutoa speech ambayo ilishaandikwa, lafudhi ya hizi shule za english medium imekazwa sana imekaa kibantu bantu, kutamka neno "the" mtu anasema "ze", temperature akiitamka anakaza sana ulimi, na ndio mana hata walimu wa hizi shule wanapata wakati mgumu wakikutana na mzungu wa marekani ama uingereza, ukitaka kuamini nachosema muite mwanafunzi wa hizo english medium muwekee mziki hata wa chris brown aandike mashairi yote mpe hata dakika 10 arudie rudie, akimaliza ingia google usechi hayo mashairi anza kumsahisha.

Wengi wakimaliza shule wanapata njia nyepesi kuingia moja kwa moja vyuo vikubwa kidunia kama Havard, Oxford, Cambridge, n.k. huku wanazidi kuongeza connection na uzito wa status.

wakihitimu vyuo wanapata wepesi wa kuaminiwa na mashirika ya Kimaifa kama UN, UNHCR, UNICEF, connection huwa zinawasaidia sana lakini pia hizi shule mtu anaweza awe na uwezo wa kawaida darasani lakini anazungumza lugha tatu tofauti na zote ni kimataifa, chuo kasoma huko oxford, field kafanya mashirika makubwa huko ulaya na marekani, hapa kupenya inakuwa fasta. na sidhani kama kuna hasara endapo mtoto akisoma shule hizi na akaja kupata ulaji hapa hapa Tanzania sehem kama benki kuu, bandarani, ikulu, tanapa, n.k.

Watanzania wengi huwa tukiona mtu kwao wakiwa na utajiri wa kipimo flani mfano familia ina biashara za kuwafanya wawe wanatembelea v8 na range tunaanza kuwaita mambo safi na pengine mtu wa familia hio anaridhika lakini mtoto akienda hizi shule akipata exposure ya kuwajua wenzake wahindi, waarabu na wazungu anaona wenzake kwao zipo Ferarri, Lambogini, n.k, anaanza kujiona ule utajiri wa nyumbani ambao wabongo tunauita mambo safi, si kitu kwa familia za marafiki zake, hii itampa moto wa kutaka kuimarisha zaidi biashara ya familia iwe hata kimataifa, kama mihogo walikuwa wanawauzia wahindi elf 10 lwa debe wao wanaenda kuuza laki 2 huko ulaya, connections zinaweza kumsaidia ajue namna ya kuuza moja kwa moja ulaya.

Pia kupata mambo kama connections za wawekezaji inakuwa rahisi pamoja na kupata idea mpya za biashara. mfano kama huyu Fenandes mwenye App ya Nala wabongo wengi tulimshangaa anakataa mshahara wa milioni 40 kila mwezi kumbe jamaa kapitia hizi shule ashapata exposure na connections, Leo hii ana app yake ya kawaida tu lakini mara kwa mara utasikia kapata wafadhili wamemwaga pesa, kapewa ruzuku, kampuni yake imeshinda kitu flani imezawadiwa pesa, n.k. ujue nyuma ya pazia jamaa anatumia exposusure na connections zake kufanikisha hizi mambo, sio bahati.

Tukatae tukubali connection na exposure ni kitu kikubwa sana kwenye maisha, Kama huna connection au exposure sio kwamba hutafanikiwa, unaweza ukafanikiwa ila either kwa kutumia nguvu kubwa sana au uwe mtu wa bahati sana
Nimemkumbuka Noreen Mollel wa SCIS

kichwa balaa
 
Kavae 2nd🥸🥸🥸 usome vizuri tofauti ya hizo school fees hacha kujipa Moyo, hiyo ni sawa na kusema Gucci na Zara ni sawa 🥵🥵
Sio kwa ubaya nakwambia nikwamba Nina uhakika nachokisema sio kwa maneno ila kwa vitendo . Naiishia hapa kwa sasa
 
Kavae 2nd🥸🥸🥸 usome vizuri tofauti ya hizo school fees hacha kujipa Moyo, hiyo ni sawa na kusema Gucci na Zara ni sawa 🥵🥵
IST wameweka ada ndefu sababu ki;a mtu anataka apeleke mtoto hapo wana brand kubwa, wanaweza weka haya milioni 100 watu wataenda tu [ia wamefanya hivi ili shule isijae, hao sana sana wana jeuri ya brand ila kuhusu elim mtaala ule ule
 
Mshahara wa NAPE aufiki zaidi ya 15m mpaka marupurupu pamoja na uwaziri wake hata akimpokea rais wa US kama mfukoni hakusomi vyema .Kuna mashirika hapa Tz yanalipa mpaka 15-40m na ni mtu wa kawaida tu ila ana exposure kubwa sana
Hujaelewa tulia uelewe, umejibu kwa makasiriko.
 
Kwahiyo ukienda shule zenye mitaala ya Cambridge HAKUNA watu wengine, Ni wachagga tu??

Kampuni gani za ndege, sema tu Precision. Haya makampuni yana Siri zake. Kwahiyo Fastjet ilikuwa inamilikiwa na Masha msukuma??

98% ya wachagga bado wachuuzi tu na biashara za Bar.

Uchumi wa nchi hii unamilikiwa na Wahindi.

=====

DAR = wote.

Dodoma = Shabiby + Gulamali

Shinyanga = Jambo.

Iringa = Asas

Morogoro = Abood.

Tanga = Binslum.

Singida = Mo Dewji.

Ninyi kazi yenu kubweka bweka na vibiashara vyenu vya Bar, maduka ya bidhaa za wizi na wizi serikalini.
Wachuuzi wa bar.😃😃😃😃😃
 
Yaani unataka kulinganisha kusoma Feza, International school Tanganyika, havard, na kusoma udom temeke secondary!?
We jamaa acha utani,hizo shule na vyuo vya kishua vina miundombinu Bora na waalimu wenye weredi. Mtoto anapata mafunzo kwa vifaa Bora,
Sisi tulijifunza practical physics, chemistry kwa nadharia tu, chemical hakuna, huwezi kulinganisha na wanaosoma na vifaa duni.
Ukiwa DIT,practicals unafanya na mashine za kizamani zilizotolewa msaada na Soviet Union, ukienda field tanesco,unaishia kufunga service line, harafu unataka Uwe engineer kama aliyetoka havard!
Yeah umeongea fact.
Hasahasa hapo kwenye practical tunatumia vifaa vibovu vilivyonunuliwa mwaka 1940 ni ngumu kumaster unakuta unachonga chuma kwa kutumia lathe machine chuma kinazunguka huku kinakata mauno huwezi kupata accuracy wakati wenzetu wanatumia computerised/CNC machine kazi inaisha fasta.
 
Hakuna Mchagga, Mmasai, Mmeru, Mpare, Mwarusha anaeweza kusomesha mtoto ktk hizo shule, huko Moshi na Arusha jtk hizo shule wapo watoto wa kuhundi, kizungu labda na Waarabu.
Mchagga wa kumpeleka mtoto shule mill 85 hajazaliwa, Mchagga anaijua pesa, Mchagga anamuandaa mtoto wake kuwa mfanyabiashara na sio teller.
Unasema? Wakati niko sekondari ya serikali zamani hizo, jirani yetu Massawe alikuwa na watoto watatu wanasoma IST Masaki. Majina yao yanaanzia M,A,J. M wa kike, A na J wakiume.

Jirani mwingine mchagga Kirei alikuwa na watoto wawili mapacha wa kike na kiume J na J hapo hapo IST Masaki. Mwingine mama Mary watoto watatu IST Masaki.
 
Back
Top Bottom