Askari Kanzu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 4,596
- 1,234
Sasa mtafungwa mbona unajipiga risasi mguuni? Inakuweje wewe tena unaanza kujieleza kwa king'eng'e wakati swali lako ni: Tutaachana lini na lugha ya kiingereza?If you're a government or some sort of supreme leader, one way to sustain power is to control your people's minds by controlling the education you make available to them. To control that education, do so by controlling the language used in providing education. A country full of ignorant and confused people is easier to govern than one with a population that is fully aware of what the government is up to. Sorry! This is supposed to be top secret.
Kwi kwi kwi, teh teh teh.
Sasa mtafungwa mbona unajipiga risasi mguuni? Inakuweje wewe tena unaanza kujieleza kwa king'eng'e wakati swali lako ni: Tutaachana lini na lugha ya kiingereza?
Karibu tena tuiendeleze na kujivunia lugha hii yetu ya Kiswahili ambayo ndio lugha kubwa ya kiafrika hapa duniani ikiwa na chimbuko lake nchini Tanzania. Kiingereza sawa lakini Kiswahili oyeeee!Samahani! Nilikuwa nimeteleza kidogo tu kwa sababu ya hasira lakini sasa nimerudi zizini...:wink2:
Awali ya yote napenda kuwasalimuni ninyi nyote katika jukwaa hili.
Lugha ya kiingereza ni ngumu kwa wengi wetu lakini bado serikali inasisitiza kwamba iendelee kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Wakati huohuo lugha ya Kiswahili imekukuwa/kuzwa na kufikia kiwango ambacho kinafaa na kutosha kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Kwa nini tusiachane na kiingereza na badala yake tutumie Kiswahili chetu ktk taasisi zetu za elimu? Kwa nini lugha ya kiingereza isibaki tu kama somo la kawaida mashuleni na vyuoni? Maoni yenu tafadhali.
Shukrani za awali.
Mwalimu Mtoboasiri, huu mtizamo kwa kiwango kikubwa unatokana na hali ya umasikini tuliyonayo. Sidhani kama yote usemayo ni sahihi. Kwa mfano, katika nchi za Ulaya ambako Kiingereza sio lugha ya kitaifa utakuta lugha za kitaifa zimepewa kipaumbele (Sweden, Germany, France, Finland, Italy etc). Hii inatokana, kama usemavyo katika pointi yako namba 2, kwamba nchi hizi zinajiweza kiuchumi. Hao wachina wanahimiza Kiingereza lakini sio kama vile tunavyotaka kufanya sisi (yaani kudunisha Kiswahili na kutukuza Kiingereza). Wachina ni watu wanaotukuza sana utamaduni wao kuliko sisi tulivyo na ndio maana waafrica kwa ujumla ni watu tunaojiona duni kwa sababu tumetelekeza utamaduni wetu na kukumbatia tamaduni za wazungu.Mimi ni mwalimu na nitakupa sababu mbili chap chap :
1. Kiingereza ni lugha ya kimataifa, huwezi kufanya biashara ya kimataifa worldwide bila kutumia English (jiulize kwa nini the second largest economy in the world today China wanahimiza matumizi ya English)?
2. Hatuwezi japo kuhakikisha kuwa kuna madawati kwa kila mwanafunzi, tutaweza kutafsiri vitabu vya IT, chemistry, physics, accounting, biology, dentistry etc (na kulipa copyright keeping in mind hatuna vitabu vyetu wenyewe katika taaluma mbali mbali)?
Sababu ni nyingi lakini hebu nijibu hizo mbili tu.
Mwalimu Mtoboasiri, huu mtizamo kwa kiwango kikubwa unatokana na hali ya umasikini tuliyonayo. Sidhani kama yote usemayo ni sahihi. Kwa mfano, katika nchi za Ulaya ambako Kiingereza sio lugha ya kitaifa utakuta lugha za kitaifa zimepewa kipaumbele (Sweden, Germany, France, Finland, Italy etc). Hii inatokana, kama usemavyo katika pointi yako namba 2, kwamba nchi hizi zinajiweza kiuchumi. Hao wachina wanahimiza Kiingereza lakini sio kama vile tunavyotaka kufanya sisi (yaani kudunisha Kiswahili na kutukuza Kiingereza). Wachina ni watu wanaotukuza sana utamaduni wao kuliko sisi tulivyo na ndio maana waafrica kwa ujumla ni watu tunaojiona duni kwa sababu tumetelekeza utamaduni wetu na kukumbatia tamaduni za wazungu.
Kwa sisi waafrica, haswa waliotawaliwa na waingereza, juhudi zetu kubwa tunazielekeza kujaribu kufahamu Kiingereza hata zaidi ya mwingereza mwenyewe (kasumba ya ukoloni isiyo na tija). Kwa hali ilivyo sasa wasomi wengi wanaweza kujieleza kwa Kiingereza lakini sio kwa Kiswahili, kwa hiyo mawasiliano yao na watu wa kawaida yanakuwa na vizuizi vingi. Faida hapo iko wapi?
Tunahitaji kukuza na kutukuza Kiswahili (hii haina maana kukisahau Kiingereza) kama tunataka tuondokane na kasumba ya kikoloni. Umasikini wetu usiwe kama ndio sindano ya ganzi inayotufanya tusiweze kuanza mkakati wa kudumisha na kutukuza utamaduni wetu.
Mwandishi Ngugi wa Thiong'o (baada ya kuandika kwa Kiingereza kwa muda mrefu) alikuja kujistukia mwenyewe kwamba haeleweki na hao watu aliokuwa anawalenga na maandishi yake kwa sababu walikuwa hawafahamu anachoandika. Hii ilimtuma kuandika "Decolonizing the mind."
Hata hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere aliwahi kusema "the last stage of human liberation is mental liberation, and that is the hardest of them all!"
Tuendelee kujadili.
Ni uchaguzi wako ndugu muuliza swali.
Una hiari kukataa kutumia hiyo lugha na kung'ang'ana na kiswahili.
Hebu komaa na kiswahili tu halafu uje hapa utupe matokeo.
Ukishakuwa tegemezi kwenye uchumi, huwezi tumia lugha unayoitaka wewe......Awali ya yote napenda kuwasalimuni ninyi nyote katika jukwaa hili.
Lugha ya kiingereza ni ngumu kwa wengi wetu lakini bado serikali inasisitiza kwamba iendelee kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Wakati huohuo lugha ya Kiswahili imekukuwa/kuzwa na kufikia kiwango ambacho kinafaa na kutosha kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Kwa nini tusiachane na kiingereza na badala yake tutumie Kiswahili chetu ktk taasisi zetu za elimu? Kwa nini lugha ya kiingereza isibaki tu kama somo la kawaida mashuleni na vyuoni? Maoni yenu tafadhali.
Shukrani za awali.
Hapo hakuna ukweli zaidi ya kwamba tatizo ni umasikini wetu na kasumba za kujiona duni.Hata siku moja hatuwezi jifananisha na Uchina na Ufaransa.We need English.Ukienda level ya juu kielimu ambapo kuna research na kuandika kwa sana ndipo utajua umuhimu wa kiingreza.
Tutake tusitake,kiingreza kimetawala dunia na watanzania tunahitaji kiingreza kwa sasa zaidi ya kiswahili.Endeleeni kudanganyana kuwa kiswahili kinatambulisha utaifa...
Hapo hakuna ukweli zaidi ya kwamba tatizo ni umasikini wetu na kasumba za kujiona duni.
hakuna aliyenidanganya. ninaishi huku kwa miaka 28 sasa. ninafahamu kile ninachoongea!Kumbe unajua sisi maskini, kwa hiyo unataka tuwe maskini jeuri ati?. Hii kasumba ya kusema eti kuna wadanish, waswedish, wajeruman e.t.c hawajui kiingereza nani kakudanganya?. Hata kama wana lugha yao, kiingereza wanakijua sana tu, wala huwezi fananisha na level ya watanzania wengi. Hata wachina wengi ambao hawajui kitu ndio hao wanakuja kuuza karanga Kariakoo. Wachunguze wanaofanya kazi kwenye mapampuni na mashirika ya kimataifa kama hawakijui kiingereza. Kwa kifupi tu kwa karne hii ya Utandawazi kiingereza ndio kinakua na kupata nguvu zaidi. Karne hii English ndio lugha mama zingine ni mbwembwe tu za kupamba CV na kukupa nafasi kubwa zaidi ya kupata kazi. Kiingereza hakikwepeki, ukikwepa lako jembe LOL!
Kingereza kigumu kinoma aisee coz misingi hatuna ndio maana kinatupiga chenga sana,big up ally kiba ulipohojiwa na spora ulitelemsha kishwahili,kina kanumba igeni mfano huo,kama haujui kingereza ukihojiwa we jibu kishwahili tu na hao wanaokuaji wataweka subtitle tu.
simplemind, nadhani hapa hatukatai kwamba kujifunza na kukielewa Kiingereza ni swala muhimu. Tatizo, kwa upande wangu linakuja pale watu wanapoanza kusema eti Kiswahili hakina tija katika ulimwengu wa leo, ndo hapo nasema haya ni mawazo yenye kasumba ya kikoloni!Shaaban Robert: Titi la mama tamu japo la mbwa, Kweli,pia enzi za utandawazi ki english muhimu sana .
2. Hatuwezi japo kuhakikisha kuwa kuna madawati kwa kila mwanafunzi, tutaweza kutafsiri vitabu vya IT, chemistry, physics, accounting, biology, dentistry etc (na kulipa copyright keeping in mind hatuna vitabu vyetu wenyewe katika taaluma mbali mbali)?
Nyani Ngabu, It makes financial sense most of the times to pay in order to use intellectual property of others. Haina maana kuwa ukichukua uamuzi huo unakuwa huna akili - hata nchi zilizoendelea maamuzi ya namna hiyo hutumika. Si lazima mtu kufanya ugunduzi kwa kitu kilichogunduliwa tayari. Moja ya sababu zinazosababisha elimu yetu kuwa duni ni kuacha kutumia tested and proved methods ili tu kuwa na maamuzi yetu wenyewe. Nitakupa mfano: Nchi nyingi duniani madarasa matatu ya mwanzo hutia mkazo katika kusoma, kuandika na kuhesabu (na ndio mimi nilipitia mfumo huo kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu). Leo hii mtoto wa darasa la kwanza anafundishwa zaidi ya masomo sita (likiwemo somo la sayansi), unategemea mtoto wa miaka sita akae darasani zaidi ya saa tatu na aelewe kitu? Halafu tunashangaa kuwepo kwa wahitimu wa darasa la saba wasiojua kusoma na kuandika! Hili la kutilia mkazo Kiswahili - na sijawahi kuona ushahidi kuwa kiwango cha matumizi ya Kiswahili kinanakua au Kiswahili sanifu kinatumika siku hizi - litachangia kuua elimu kabisa. Ukiniuliza mimi nitakuambia kauli kama hizi ni mbinu ya watawala kudumaza walio wengi ili iweze rahisi zaidi kuwatawala.Hapo ndipo "Miafrika Ndivyo Tulivyo" comes into play. Kwa nini hatuna textbooks zetu wenyewe? Si tunajidai tuna akili sana....sasa nini kinachotushinda? Waingereza wako juu sana. Nani anabisha?
Ukishakuwa tegemezi kwenye uchumi, huwezi tumia lugha unayoitaka wewe......
Hata siku moja hatuwezi jifananisha na Uchina na Ufaransa.We need English.Ukienda level ya juu kielimu ambapo kuna research na kuandika kwa sana ndipo utajua umuhimu wa kiingreza.
Tutake tusitake,kiingreza kimetawala dunia na watanzania tunahitaji kiingreza kwa sasa zaidi ya kiswahili.Endeleeni kudanganyana kuwa kiswahili kinatambulisha utaifa...