Tutaachana lini na lugha ya kiingereza?

Tutaachana lini na lugha ya kiingereza?

If you're a government or some sort of supreme leader, one way to sustain power is to control your people's minds by controlling the education you make available to them. To control that education, do so by controlling the language used in providing education. A country full of ignorant and confused people is easier to govern than one with a population that is fully aware of what the government is up to. Sorry! This is supposed to be top secret.
Sasa mtafungwa mbona unajipiga risasi mguuni? Inakuweje wewe tena unaanza kujieleza kwa king'eng'e wakati swali lako ni: Tutaachana lini na lugha ya kiingereza?
 
Sasa mtafungwa mbona unajipiga risasi mguuni? Inakuweje wewe tena unaanza kujieleza kwa king'eng'e wakati swali lako ni: Tutaachana lini na lugha ya kiingereza?

Samahani! Nilikuwa nimeteleza kidogo tu kwa sababu ya hasira lakini sasa nimerudi zizini...:wink2:
 
Samahani! Nilikuwa nimeteleza kidogo tu kwa sababu ya hasira lakini sasa nimerudi zizini...:wink2:
Karibu tena tuiendeleze na kujivunia lugha hii yetu ya Kiswahili ambayo ndio lugha kubwa ya kiafrika hapa duniani ikiwa na chimbuko lake nchini Tanzania. Kiingereza sawa lakini Kiswahili oyeeee!
 
Awali ya yote napenda kuwasalimuni ninyi nyote katika jukwaa hili.

Lugha ya kiingereza ni ngumu kwa wengi wetu lakini bado serikali inasisitiza kwamba iendelee kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Wakati huohuo lugha ya Kiswahili imekukuwa/kuzwa na kufikia kiwango ambacho kinafaa na kutosha kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Kwa nini tusiachane na kiingereza na badala yake tutumie Kiswahili chetu ktk taasisi zetu za elimu? Kwa nini lugha ya kiingereza isibaki tu kama somo la kawaida mashuleni na vyuoni? Maoni yenu tafadhali.

Shukrani za awali.

Mimi ni mwalimu na nitakupa sababu mbili chap chap :

1. Kiingereza ni lugha ya kimataifa, huwezi kufanya biashara ya kimataifa worldwide bila kutumia English (jiulize kwa nini the second largest economy in the world today China wanahimiza matumizi ya English)?

2. Hatuwezi japo kuhakikisha kuwa kuna madawati kwa kila mwanafunzi, tutaweza kutafsiri vitabu vya IT, chemistry, physics, accounting, biology, dentistry etc (na kulipa copyright keeping in mind hatuna vitabu vyetu wenyewe katika taaluma mbali mbali)?

Sababu ni nyingi lakini hebu nijibu hizo mbili tu.
 
Mwalimu Mtoboasiri, huu mtizamo kwa kiwango kikubwa unatokana na hali ya umasikini tuliyonayo. Sidhani kama yote usemayo ni sahihi. Kwa mfano, katika nchi za Ulaya ambako Kiingereza sio lugha ya kitaifa utakuta lugha za kitaifa zimepewa kipaumbele (Sweden, Germany, France, Finland, Italy etc). Hii inatokana, kama usemavyo katika pointi yako namba 2, kwamba nchi hizi zinajiweza kiuchumi. Hao wachina wanahimiza Kiingereza lakini sio kama vile tunavyotaka kufanya sisi (yaani kudunisha Kiswahili na kutukuza Kiingereza). Wachina ni watu wanaotukuza sana utamaduni wao kuliko sisi tulivyo na ndio maana waafrica kwa ujumla ni watu tunaojiona duni kwa sababu tumetelekeza utamaduni wetu na kukumbatia tamaduni za wazungu.

Kwa sisi waafrica, haswa waliotawaliwa na waingereza, juhudi zetu kubwa tunazielekeza kujaribu kufahamu Kiingereza hata zaidi ya mwingereza mwenyewe (kasumba ya ukoloni isiyo na tija). Kwa hali ilivyo sasa wasomi wengi wanaweza kujieleza kwa Kiingereza lakini sio kwa Kiswahili, kwa hiyo mawasiliano yao na watu wa kawaida yanakuwa na vizuizi vingi. Faida hapo iko wapi?

Tunahitaji kukuza na kutukuza Kiswahili (hii haina maana kukisahau Kiingereza) kama tunataka tuondokane na kasumba ya kikoloni. Umasikini wetu usiwe kama ndio sindano ya ganzi inayotufanya tusiweze kuanza mkakati wa kudumisha na kutukuza utamaduni wetu.

Mwandishi Ngugi wa Thiong'o (baada ya kuandika kwa Kiingereza kwa muda mrefu) alikuja kujistukia mwenyewe kwamba haeleweki na hao watu aliokuwa anawalenga na maandishi yake kwa sababu walikuwa hawafahamu anachoandika. Hii ilimtuma kuandika "Decolonizing the mind."

Hata hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere aliwahi kusema "the last stage of human liberation is mental liberation, and that is the hardest of them all!"

Tuendelee kujadili.
 
Wewe ndiwe mtoboa siri maana umetoboa siri yenyewe hasa. Huyu mwalimu wetu mpendwa anayeitwa Mtoboasiri kwakweli hajatoboa siri, na wapo wengi kama yeye katika mfumo wetu wa elimu. Namshauri mtoboa siri aende pale TATAKI (Taasisi ya Taaluma za Kiswahili) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akajionee mwenyewe kazi inayofanywa pale. Kwa kifupi, watanzania tumejiandaa vyakutosha kabisa kwa upande wa lugha ya Kiswahili. Kiswahili kimeendelezwa hadi kufikia ngazi ya juu kiasi kwamba inatosha kutumika katika sayansi, tekinolojia, utafiti wa kisayansi, na pia inatosha kabisa kutumika kama lugha ya kufundishia mashuleni hadi vyuoni. Tuanze kutumia Kiswahili sasa kama lugha mama katika taasisi zetu lakini wakati huohuo tuendelee kujifunza lugha za wengine ili tuweze kuwasiliana nao na kufuatilia kinachoendelea duniani, na pia kutumia lugha hizo tunapokwenda nje masomoni, kwa mfano.

Tusisubiri eti kwanza uchumi wa nchi ukue ndipo tuanze kutumia lugha yetu! Uchumi utakuwa haraka yakiwa ni matokeo ya ubunifu utokanao na utumiaji wa lugha tunayoijua zaidi, ambayo ni Kiswahili. Uchumi huwa haukuwi kwa njia ya kutumia lugha ya kuazima katika elimu kwa sababu lugha ile haiwezi kutosheleza mahitaji ya nafsi na akili kwa ajili ya ubunifu na uelewa wa kutosha. Mwalimu mtoboa siri aangalie mambo haya kwa uangalifu--mtazamo wake unapotosha vizazi vya sasa na kesho.
 
Ni uchaguzi wako ndugu muuliza swali.
Una hiari kukataa kutumia hiyo lugha na kung'ang'ana na kiswahili.
Hebu komaa na kiswahili tu halafu uje hapa utupe matokeo.

Wewe nawe! Sijui wawapi mwenzetu. Ukiijua vizuri lugha yako na kuitumia kuna shida gani? Si mali yako tu jamani? pia kuitawala lugha yako si maana yake kwamba usijifunze lugha za wenzio...uhuru unao. Halafu unaposema uchaguzi ni wangu sikuelewi maana mjadala huu unahusu taifa letu zima, si mimi au wewe tu. Anza kujali kilicho chako kwanza kabla hujaanza kukumbatia vya wenzio!
 
Awali ya yote napenda kuwasalimuni ninyi nyote katika jukwaa hili.

Lugha ya kiingereza ni ngumu kwa wengi wetu lakini bado serikali inasisitiza kwamba iendelee kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Wakati huohuo lugha ya Kiswahili imekukuwa/kuzwa na kufikia kiwango ambacho kinafaa na kutosha kutumika mashuleni na vyuoni kama lugha ya kufundishia. Kwa nini tusiachane na kiingereza na badala yake tutumie Kiswahili chetu ktk taasisi zetu za elimu? Kwa nini lugha ya kiingereza isibaki tu kama somo la kawaida mashuleni na vyuoni? Maoni yenu tafadhali.

Shukrani za awali.
Ukishakuwa tegemezi kwenye uchumi, huwezi tumia lugha unayoitaka wewe......
 
Hata siku moja hatuwezi jifananisha na Uchina na Ufaransa.We need English.Ukienda level ya juu kielimu ambapo kuna research na kuandika kwa sana ndipo utajua umuhimu wa kiingreza.
Tutake tusitake,kiingreza kimetawala dunia na watanzania tunahitaji kiingreza kwa sasa zaidi ya kiswahili.Endeleeni kudanganyana kuwa kiswahili kinatambulisha utaifa...
 
Hapo hakuna ukweli zaidi ya kwamba tatizo ni umasikini wetu na kasumba za kujiona duni.
 
Hapo hakuna ukweli zaidi ya kwamba tatizo ni umasikini wetu na kasumba za kujiona duni.

Kumbe unajua sisi maskini, kwa hiyo unataka tuwe maskini jeuri ati?. Hii kasumba ya kusema eti kuna wadanish, waswedish, wajeruman e.t.c hawajui kiingereza nani kakudanganya?. Hata kama wana lugha yao, kiingereza wanakijua sana tu, wala huwezi fananisha na level ya watanzania wengi. Hata wachina wengi ambao hawajui kitu ndio hao wanakuja kuuza karanga Kariakoo. Wachunguze wanaofanya kazi kwenye mapampuni na mashirika ya kimataifa kama hawakijui kiingereza. Kwa kifupi tu kwa karne hii ya Utandawazi kiingereza ndio kinakua na kupata nguvu zaidi. Karne hii English ndio lugha mama zingine ni mbwembwe tu za kupamba CV na kukupa nafasi kubwa zaidi ya kupata kazi. Kiingereza hakikwepeki, ukikwepa lako jembe LOL!
 
Shaaban Robert: Titi la mama tamu japo la mbwa, Kweli,pia enzi za utandawazi ki english muhimu sana .
 
hakuna aliyenidanganya. ninaishi huku kwa miaka 28 sasa. ninafahamu kile ninachoongea!
 
Kingereza kigumu kinoma aisee coz misingi hatuna ndio maana kinatupiga chenga sana,big up ally kiba ulipohojiwa na spora ulitelemsha kishwahili,kina kanumba igeni mfano huo,kama haujui kingereza ukihojiwa we jibu kishwahili tu na hao wanaokuaji wataweka subtitle tu.

Respect yangu kwa Ally Kiba imeongezeka kwa hili.

Wengi wetu hata Kiswahili hatukijui vizuri.

Zaidi ya yote, ukweli kwamba hatujui Kiingereza unatakiwa kututia motisha zaidi tukijue, kwa sababu kama alivyosema Nyerere Kiingereza ndicho "Kiswahili cha dunia" na kukataa kujifunza Kiingereza ni kukataa kuchangamana na dunia.
 
Shaaban Robert: Titi la mama tamu japo la mbwa, Kweli,pia enzi za utandawazi ki english muhimu sana .
simplemind, nadhani hapa hatukatai kwamba kujifunza na kukielewa Kiingereza ni swala muhimu. Tatizo, kwa upande wangu linakuja pale watu wanapoanza kusema eti Kiswahili hakina tija katika ulimwengu wa leo, ndo hapo nasema haya ni mawazo yenye kasumba ya kikoloni!
 
2. Hatuwezi japo kuhakikisha kuwa kuna madawati kwa kila mwanafunzi, tutaweza kutafsiri vitabu vya IT, chemistry, physics, accounting, biology, dentistry etc (na kulipa copyright keeping in mind hatuna vitabu vyetu wenyewe katika taaluma mbali mbali)?

Hapo ndipo "Miafrika Ndivyo Tulivyo" comes into play.

Kwa nini hatuna textbooks zetu wenyewe? Si tunajidai tuna akili sana....sasa nini kinachotushinda?

Waingereza wako juu sana. Nani anabisha?
 
Hapo ndipo "Miafrika Ndivyo Tulivyo" comes into play. Kwa nini hatuna textbooks zetu wenyewe? Si tunajidai tuna akili sana....sasa nini kinachotushinda? Waingereza wako juu sana. Nani anabisha?
Nyani Ngabu, It makes financial sense most of the times to pay in order to use intellectual property of others. Haina maana kuwa ukichukua uamuzi huo unakuwa huna akili - hata nchi zilizoendelea maamuzi ya namna hiyo hutumika. Si lazima mtu kufanya ugunduzi kwa kitu kilichogunduliwa tayari. Moja ya sababu zinazosababisha elimu yetu kuwa duni ni kuacha kutumia tested and proved methods ili tu kuwa na maamuzi yetu wenyewe. Nitakupa mfano: Nchi nyingi duniani madarasa matatu ya mwanzo hutia mkazo katika kusoma, kuandika na kuhesabu (na ndio mimi nilipitia mfumo huo kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu). Leo hii mtoto wa darasa la kwanza anafundishwa zaidi ya masomo sita (likiwemo somo la sayansi), unategemea mtoto wa miaka sita akae darasani zaidi ya saa tatu na aelewe kitu? Halafu tunashangaa kuwepo kwa wahitimu wa darasa la saba wasiojua kusoma na kuandika! Hili la kutilia mkazo Kiswahili - na sijawahi kuona ushahidi kuwa kiwango cha matumizi ya Kiswahili kinanakua au Kiswahili sanifu kinatumika siku hizi - litachangia kuua elimu kabisa. Ukiniuliza mimi nitakuambia kauli kama hizi ni mbinu ya watawala kudumaza walio wengi ili iweze rahisi zaidi kuwatawala.
 
Ukishakuwa tegemezi kwenye uchumi, huwezi tumia lugha unayoitaka wewe......

Sawa. Ila ungefafanua kidogo hapa. Una maana kwamba mkakati wa kuanza kutumia lugha yetu ktk elimu lazima uendane na mkakati wa kuinua uchumi wetu...au tuanze na uchumi kwanza na halafu tuje kwenye lugha? Pia nadhani ni lazima tukubaliane kwamba tukiamua kutumia lugha yetu saa hizi ktk elimu hakuna taifa litakalokatisha uhusiano wa kibiashara na sisi eti kwa sababu ya lugha. Tukianza harakati hizo, China, Japan, India, Africa Kusini, Brazil, marekani, Korea ya kusini, na wengine ambao ni wadau wakubwa kibiashara hawatakuwa na neno. Labda mwenye kigugumizi atakuwa mwingereza tu...kuna taabu gani hapo? Kwani tunamtegemea mwingereza kiasi kikubwa sana?
 
Hata siku moja hatuwezi jifananisha na Uchina na Ufaransa.We need English.Ukienda level ya juu kielimu ambapo kuna research na kuandika kwa sana ndipo utajua umuhimu wa kiingreza.
Tutake tusitake,kiingreza kimetawala dunia na watanzania tunahitaji kiingreza kwa sasa zaidi ya kiswahili.Endeleeni kudanganyana kuwa kiswahili kinatambulisha utaifa...

Katika mjadala huu, tumefikia makubaliano miongoni mwa wengi wa wachangiaji kwamba lugha za kigeni, ikiwa ni pamoja na kiingereza, tunazihitaji kama watu wengine nchi zingine wanavyohitaji lugha hizi. Tena lazima utambue kuwa huenda kiingereza kikapoteza umaarufu wake muda mfupi ujao. Nani alidhani enzi zile za urumi kilatini kingejiengua na kubaki kama lugha iliyo nje ya matumizi ya kila siku. Kumbuka Kigiriki cha enzi hizo, nk. Usishangae kuona kichina kinaibuka na kuwa lugha muhimu kuliko zote kimataifa...si unajuwa mambo hayo? Halafu lugha ya kiingereza si kwamba ni kila kitu. Hujaona research papers zikiandikwa kwa kijerumani, kichina, kiswahili, kiswidi, nk. Utasema uchumi ni fakta...sawa. Lakini this is not a decisive factor.

Halafu pia katika kongamano letu ndani ya jukwaa hili wengi tumekubaliana kwamba pamoja na kujifunza lugha nyingine, ikiwemo kiingereza, lugha ambayo ni ya kwetu (kiswahili) lazima ipewe kipaumbele cha kwanza. Mtanzania aijue lugha yake vizuri sana na aitumie katika mambo ya msingi yanayomletea maendeleo na utashi kama mtu, ikiwa ni pamoja na kujifunza kwa kutumia lugha yake. Wakati huohuo akazanie sana lugha za kimataifa ili azitumia kwa mfano, katika masomo akiwa nchi nyingine, katika tafiti za kimataifa, makongamano na warsha za kimataifa, biashara za kimataifa, mahusiano ya kidiplomasia, nk. Kwa hiyo, kwa mfano, mwanafunzi anapokuwa shuleni na vyuoni, apate mafunzo kwa lugha yake lakini wakati huohuo alazimike au alazimishwe kujifunza lugha muhimu za kimataifa.

Ni lazima tutambue kwamba lugha ina uhusiano wa karibu sana na ufahamu au utambuzi wa mambo. Kwa mfano, mtu anayemudu sana lugha yake hujifunza lugha nyingine kwa wepesi zaidi. Hii ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisaikolojia zilizokwishafanywa. Tafiti hizo pia zinaonyesha kwamba ili mtu aelewe jambo na limkae vizuri akilini lazima ajifunze kwa lugha aijuwayo zaidi. Umeona watu wanachanganya lugha ya kiswahili na kiingereza wakiwa katika maongezi au hata ktk mikutano rasmi...hiyo ni dalili kwamba kuna taabu ktk matumizi ya lugha na pia ktk kufikiri...in English, when you code-switch languages or even code-mix, it is often an indication that you are inadequate language-wise. It is also an indication that there is lack of cohesion in your thinking machinery (brain or mind). Kwa hiyo usishangae unapoona taabu ya elimu humu nchini mwetu. Kiini cha taabu hiyo ni mapungufu katika lugha ya kujifunzia.

Kwa hiyo huu ni wakati mwafaka (mnisahihishe kiswahili) kwa serikali yetu, hasa wizara inayohusika, kutengeneza muswada unaopendekeza kubadili sera ya lugha ya kufundishia mashuleni na vyuoni. Kiswahili kitumike kama lugha mama ya mafunzo na kiingereza kifundishwe kwa nguvu zote. Lugha nyingine kama kichina zifundishwe pia kwa ajili ya mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia. Muswada huo upelekwe bungeni na ujadidiliwe kwa marefu na mapana huku wadau wengine muhimu wakihusishwa pia ambao ni sisi wananchi.

Wenzetu ktk mfumo wa mahakama wanaandaa muswada kama huo ili kiswahili kitumike katika makama zote, ikiwa ni pamoja na ktk kuhukumu kesi na kuziwekea kumbukumbu. Sasa ni wakati wa kuyaweka mambo yawe yanavyotakiwa kuwa...
 
Back
Top Bottom