Hata siku moja hatuwezi jifananisha na Uchina na Ufaransa.We need English.Ukienda level ya juu kielimu ambapo kuna research na kuandika kwa sana ndipo utajua umuhimu wa kiingreza.
Tutake tusitake,kiingreza kimetawala dunia na watanzania tunahitaji kiingreza kwa sasa zaidi ya kiswahili.Endeleeni kudanganyana kuwa kiswahili kinatambulisha utaifa...
Katika mjadala huu, tumefikia makubaliano miongoni mwa wengi wa wachangiaji kwamba lugha za kigeni, ikiwa ni pamoja na kiingereza, tunazihitaji kama watu wengine nchi zingine wanavyohitaji lugha hizi. Tena lazima utambue kuwa huenda kiingereza kikapoteza umaarufu wake muda mfupi ujao. Nani alidhani enzi zile za urumi kilatini kingejiengua na kubaki kama lugha iliyo nje ya matumizi ya kila siku. Kumbuka Kigiriki cha enzi hizo, nk. Usishangae kuona kichina kinaibuka na kuwa lugha muhimu kuliko zote kimataifa...si unajuwa mambo hayo? Halafu lugha ya kiingereza si kwamba ni kila kitu. Hujaona research papers zikiandikwa kwa kijerumani, kichina, kiswahili, kiswidi, nk. Utasema uchumi ni fakta...sawa. Lakini this is not a decisive factor.
Halafu pia katika kongamano letu ndani ya jukwaa hili wengi tumekubaliana kwamba pamoja na kujifunza lugha nyingine, ikiwemo kiingereza, lugha ambayo ni ya kwetu (kiswahili) lazima ipewe kipaumbele cha kwanza. Mtanzania aijue lugha yake vizuri sana na aitumie katika mambo ya msingi yanayomletea maendeleo na utashi kama mtu, ikiwa ni pamoja na kujifunza kwa kutumia lugha yake. Wakati huohuo akazanie sana lugha za kimataifa ili azitumia kwa mfano, katika masomo akiwa nchi nyingine, katika tafiti za kimataifa, makongamano na warsha za kimataifa, biashara za kimataifa, mahusiano ya kidiplomasia, nk. Kwa hiyo, kwa mfano, mwanafunzi anapokuwa shuleni na vyuoni, apate mafunzo kwa lugha yake lakini wakati huohuo alazimike au alazimishwe kujifunza lugha muhimu za kimataifa.
Ni lazima tutambue kwamba lugha ina uhusiano wa karibu sana na ufahamu au utambuzi wa mambo. Kwa mfano, mtu anayemudu sana lugha yake hujifunza lugha nyingine kwa wepesi zaidi. Hii ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisaikolojia zilizokwishafanywa. Tafiti hizo pia zinaonyesha kwamba ili mtu aelewe jambo na limkae vizuri akilini lazima ajifunze kwa lugha aijuwayo zaidi. Umeona watu wanachanganya lugha ya kiswahili na kiingereza wakiwa katika maongezi au hata ktk mikutano rasmi...hiyo ni dalili kwamba kuna taabu ktk matumizi ya lugha na pia ktk kufikiri...in English, when you code-switch languages or even code-mix, it is often an indication that you are inadequate language-wise. It is also an indication that there is lack of cohesion in your thinking machinery (brain or mind). Kwa hiyo usishangae unapoona taabu ya elimu humu nchini mwetu. Kiini cha taabu hiyo ni mapungufu katika lugha ya kujifunzia.
Kwa hiyo huu ni wakati mwafaka (mnisahihishe kiswahili) kwa serikali yetu, hasa wizara inayohusika, kutengeneza muswada unaopendekeza kubadili sera ya lugha ya kufundishia mashuleni na vyuoni. Kiswahili kitumike kama lugha mama ya mafunzo na kiingereza kifundishwe kwa nguvu zote. Lugha nyingine kama kichina zifundishwe pia kwa ajili ya mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia. Muswada huo upelekwe bungeni na ujadidiliwe kwa marefu na mapana huku wadau wengine muhimu wakihusishwa pia ambao ni sisi wananchi.
Wenzetu ktk mfumo wa mahakama wanaandaa muswada kama huo ili kiswahili kitumike katika makama zote, ikiwa ni pamoja na ktk kuhukumu kesi na kuziwekea kumbukumbu. Sasa ni wakati wa kuyaweka mambo yawe yanavyotakiwa kuwa...