Tutamkumbuka kwa lipi Ummy Mwalimu?

Tutamkumbuka kwa lipi Ummy Mwalimu?

Zaidi ya kutuonyesha meno 34 yale hana la ziada, waziri gani wa afya umezidi meno ya kawaida
 
Kama mkwere yupo pale basi naachana na hii nia yangu.
Alikaa kitambo sana ila si unajua hawala hana talaka? kipindi kile ticha wa moto hatari anang'aa balaa mkwere na ticha walikutana ubalozi flani hapa tz...Mzee handsome akamuingiza kwenye siasa huku akiwa anakula tunda hizo ni za ndaaaani kabisa.
 
Ummy kashindwa kuidhibiti NHIF, NHIF watu wanaiba sana mpaka hpspitali hazilipwi. Aga Khan wamefunga, Hospitali zingine mfano Tiba, sasa hivi hawapokei bima za NHIF.

NHIF kuna pesa nyingi sana lakini kuna madudu ya kufa mtu, kama haijapewa kampuni binafsi kuiendesha, itawaondosha wengi sana.

Madudu NHIF na Madudu MADAWA ni ya kufa mtu.
Kuna ripoti ya CAG inayofichua uchotwaji fedha kutoka NHIF, sasa badala ya Waziri kuahughulikia hati chafu, akaja na scheme ya kuwalazimisha Watanzania wote kulipia bima ya afya huku akichezea bango kitita ya huduma za NHIF.

Hakuwa anamsaidia Rais, bali alikuwa kama kwenye mission ya kumfarakanisha rais na wapigakura wake
 
Kuna kitu hufahamu kuhusu NHIF, na watu wengi wamekaririshwa. Ngoja nikupe shule kidogo.

NHIF ni suala mtambuka kwa 100%, japokuwa inafanya kazi chini ya wizara ya afya lakini uratibu wake uko chini ya Rais na baraza la mawaziri kwa sababu uendeshaji wake unahitaji pesa nyingi kutoka wizara ya fedha na utumishi. Waziri wa Afya hawezi kutunga sheria wala sera za uendeshaji wake, hawezi kuteua wala kutengua mtendaji yoyote wa NHIF.
Suala la NHIF ni sawa sawa na suala la bodi ya mikopo (HESLB), Mifuko ya Pension, TANROAD, EWURA, REA. Waziri hawezi chochote linapokuja suala la kisera au sheria za uendeshaji wake. Ukiona kikotoo cha wastaafu kinawapunja wastaafu usikimbilie kumlaumu waziri husika maana hata yeye hana mamlaka ya kubadili chochote zaidi ya kupambana kusimamia utekelezaji wake.
Unaleta hearsay yaani hadithi za kusadikika.

Soma vizuri sheria inayounda NHIF.

Pia elewa kuwa Bima ya Afya inaendeshwa na michango ya waliolipia huduma ya afya.

Mnapoona kibubu kimejaa, mnashindwa kutafakari mara mbili mna chota tu
 
Laana ya mama inamkabili big time.

Alimsusa alipougua hadi kufariki na akalazimishwa na mashosti ndani ya chama akashiriki msiba...

Roho yake na sura yake ni kama afande Hamduni kwa namna anavyosifiwa sasa
Mama yupi jamani
 
Uteuzi uliofanywa na Mhe. Rais SSH tatehe 14 Agosti 2024 umemtema nje bi Ummy Mwalimu kutoka Wizara ya Afya.

Kutokana na unyeti wa Wizara ya Afya, umuhimu wake ni mkubwa kwenye jamii. Pamoja na kusimamia sera ya Afya nchini lakini ndiyo wizara inayosimamia taaluma ya wahudumu wa Afya.

Je tuna lipi la kumkumbuka dada Ummy kama mchango wake kwenye kuimarisha ama kuidhoofiaha sekta ya afya nchini

Pia soma: Ummy Mwalimu atenguliwa Uwaziri wa Afya
Zaid ya asilimia 50 za viongozi wanaoshika Aidha kwa kuteuliwa au kushinda kimagumashi katika chaguzi mbalimbali nchini vichwani mwao ni watupu yani wana uwezo mdogo kiakili.

Kuna waziri alitia aibu kushindwa kuelezea maana ya trab na trat huyo ndo kapewa dhamana ya kuiongoza wizara nyeti kabisa hapa nchini.

Huo ni mfano mmoja tu, mstue nape nauye asubuhi asubuhi katoka kuamka mulize nini tofaut ya network na internet, mulize satellite zinakazi gani katika mawasiliano akikujibu njoo nikupe million 10
 
Back
Top Bottom