Tutawalaumu bure wachezaji Simba

Tutawalaumu bure wachezaji Simba

Matola atatoa ushauri gani kwa kocha anayepiga mateke hadi viti? Simba wakimbakiza huyu kocha nitajua hawana malengo makubwa ya timu kufanya vizuri.

Kocha ni takataka kabisa huyu. Kaua viwango vya wachezaji mshenzi mkubwa huyo.
Yamekuwa hayo tena? Si nyie mlikuwa mnatutambia kwamba kafundisha soka Real Madrid?
 
Hata kina rweymamu wanakaa bench bila kutoa mchango wowote, simba wamefukuza makocha wa makipa na viungo bila sababu wakiacha wapika majungu
Mtalaumu TU mpango wa tajir ulikuwa Ni kupunguza (expenditure) kwa hyo labda tajir hakusema

Wale makocha wa viungo walikuwa wazur Sana lakn tajir aliona anatoboka Sana
 
Wapenzi na mashabiki wa Simba watalaumu kila mtu kwa matokeo mabovu kwenye msimu huu wa ligi japo walikuwa na mafanikio kwenye shirikisho Afrika. Kosa lilianzia kwenye usajili wa msimu uliopita kusajili zaidi vijana wa kiume badala ya kusajili wanaume kamili. Sakho, Banda, Mhilu Mwanuke ni vijana "promising" ambao watakuja kuwa na msaada mkubwa sana kwa Simba miaka miwili/mitatu ijayo. Mfano mzuri Yanga ilisajili msimu uliopita wanaume kama Mayele, Aucho, Bangala na wengineo ndio maana wamekuwa na matokeo mazuri. Mzimu ulikokuwa unamtafuna Azam kwa kung'ang'ania vijana ndio huo unamtafuna Simba sasa hivi. Mfano mdogo tu hao wakina Sakho na Banda wakisukumwa tu kidogo chini wala hawaamki hata kama wana nafasi ya kuamka na kufunga lakini mwenzao Kibu akisukumwa mpaka aende chini ni kazi na akiamka anaamka na mpira wake safari inaendelea kuelekea goli la mpinzani labda tu asikie filimbi ya mwamuzi.

Na iwapo viongozi hawatakuwa makini katika kipindi hiki muhimu cha usajili basi mwakani vilio ndio vitakuwa mara mbili zaidi. Ushauri wangu wa bure kwa viongozi wa Simba wazingatie vigezo vifuatavyo:-
1. Wasajili wachezaji wenye "work rate" kubwa uwanjani kama ilivyokuwa kwa Luis na Dilunga. Yaani hawa utawakuta wapo golini kwa adui
wanashambulia mara ghafla unawaona pembeni kwenye goli lao wamefanya "tackling" kuokoa wakiwasaidia mabeki wao wa pembeni.
2. Wasajili wachezaji ambao hawatembei uwanjani baada ya kunyang'anywa mpira au kupoteza mpira kizembe. Wachezaji kama Bwalya na
Sakho wana vipaji vya hali ya juu lakini vipaji hivyo vinawasaidia wao tu kupata sifa na havina msaada kwa timu kabisa. Mbaya zaidi
wanakaa na mpira muda mrefu miguuni mwao halafu wakinyangánywa na adui wanatembea na kuwaachia wenzao kazi ya kuutafuta
mpira.
3. Wasajili viungo na washambuliaji wenye kasi ambao wataichangamsha timu uwanjani. Sio siri Simba sasa hivi ipo "slow " sana.
Inatengeneza mashambulizi yake taratibu sana kutokea nyuma kiasi wakati timu inapoamua kwenda kushambulia unakuta timu pinzani
zimesha jipanga kuzuia. Hili la kutengeneza mashambulizi kuanzia nyuma halina shida iwapo tu utakuwa na wachezaji wenye "quality" ya
Chama na Luisi kwani wao wawili tu wanaweza kugongeana mpira kuanzia nyuma mpaka golini kwa adui.
4. Wasajili wachezaji wenye maumbo makubwa hii itawasidia pale wanapokutana na timu zinacheza mpira wa nguvu.
5. Mwisho kabisa wasajili wachezaji wapambanaji muda wote wawapo uwanjani kwa dakika zote tisini. Aina ya wachezaji wapambanaji ni
kama Kapombe, Inonga, Kibu na Lwanga (japo huyu amekuwa na changamoto ya majeraha).

Ni mtizamo tu.
 
Tabia za Mwalimu zinamchango mkubwa kwa mwanafunzi kufauru somo. Mwalimu ni kiungo katika kunogesha akili ya mwanafunzi. Mwalimu anaweza kuwa na digriii mia moja, lakini akikosa sifa moja muhimu ya kujuwa kuishi na kukabiliana na mazingira anayofanyia kazi na kusoma maisha na Tabia za mwanafunzi wake, si msaada tena.

Nachelea kusema hata mpira uliotufikisha katika nafasi tulizozipata ni zao la tabia zilizojengwa na waliotangulia.

Mwalimu mkali anaficha madhaifu yake ya kukosa umahili katika kufundisha. Silaha kubwa ya walimu Kama hawa ni kujenga hofu kwa mwanafunzi hali inayompelekea mwanafunzi kukosa confidence na hata kufeli.

Tujiulize Ziko wapi pass milioni zileee!

Wachezaji si walewale!

Leo wachezaji hawaonani, wanapapara, wanakitete hawana nguvu na majeruhi. Kulikoni?

Tutafakari vizuri kwa vile ni kipindi muhimu Cha kujenga au kubomowa timu. Tutaacha wachezaji wazuri kwa kufuata kinachoitwa ripoti ya mwalimu ambae mwenyewe ndio tatizo.

Ni ivyo tuuu.
Hoja yako ni ya msingi kabisa. Lkn hoja inakosa support ya vielelezo vya ndani ya timu, kwamba Pablo ni tatizo hasa ktk nini, Ni nini anafanya, au Ni namna gani anaongoza benchi la fundi ktk hali ulizozitaja. Ni ushuhuda wa wachezaji wenyewe au Ni ushahidi gani ulio nao kutoka ndani ya kambi ya mazoezi ya timu.

Pili kwa mtazamo wangu , naona bado kocha alijitahidi kuifikisha timu hapo ilipo kwa aina ya wachezaji tulio nao. Labda kigezo na kipimo kiwe Ni kocha aliyeondoka yaani Didier Gomez da Rosa.

Technically unataka kusema angekuwepo Gomez timu ingekuwa na performance bora zaidi? Kwa hawa hawa Kagere, bocco na mugalu? Au akija kocha mwingine akapewa kikosi hiki hiki ataperform vzr zaidi? Pengine km siyo Pablo Simba ingeweza kutetea ubingwa?

Kwamba Kagere, Bocco, Mugalu hawafungi kwasababu ya ubovu wa kocha?

Binafsi sina tatizo na Pablo, Cha kufanya Simba ifanye usajili wa maana (wavunje benki),wafanye usajili wa kushindana na klabu kubwa km Berkane,Wydad,( labda tatizo liwe uchumi) Ikiwezekana wamrejeshe Gomez km kocha msaidizi , matola aondoke.

Tumesikia tetesi Simba inawahitaji Adebayor, Azizi Ki, Etouga mfungaji kinara wa Asante Kotoko, Zemanga Soze toka Mazembe, Moses Phiri, lkn inaonekana km Simba hawako siriaz, Sababu tunasikia Adebayor keshasaini Berkane. Hakuna kitu kibaya ktk usajili kama kuhitaji wachezaji fulani halafu ukawakosa, wachezaji ambao wana viwango halafu ukashindwa kuwasajili. Matokeo yake ni kufanya usajili ilimradi.

Wachezaji wa ligi za Afrika Mashariki,Burundi, Rwanda , Uganda, Kenya NK hawawezi kukupa matokeo hasa ktk mechi za kimataifa. Hawa ni wa viwango vya chini na kati, wengi hawana exposure kimataifa.

Tatizo la Simba ni aina ya wachezaji waliopo kwa sasa hasa hawa wa nje. Sidhani km ni kocha. Tunahitaji usajili mkubwa.
 
Kabla hajafika Simba ilikuwa katika hali gani?

Uliionaje Simba iliyopigwa na Jwaneng Taifa?

Alikuwepo Pablo?

Ulionaje Simba mechi 2 za mwanzo?

Alikuwepo Pablo?

Kwanini mnataka kukimbia tatizo la Msingi na kulikimbiza kwa kocha?
Wala tatizo sio Pablo kabisa tangu mwanzo Simba was poor in striking eg mechi ya ngao ya hisani Mugalu kapoteza scoring chances zaid ya 4 kwenda Jwaneng watu wanakabia macho tutaachaje kupigwa!?
Uboreshaji ni muhimu mno ,Kocha apewe muda
 
Sikubaliani katika Hilo.
 
Tabia za Mwalimu zinamchango mkubwa kwa mwanafunzi kufauru somo. Mwalimu ni kiungo katika kunogesha akili ya mwanafunzi. Mwalimu anaweza kuwa na digriii mia moja, lakini akikosa sifa moja muhimu ya kujuwa kuishi na kukabiliana na mazingira anayofanyia kazi na kusoma maisha na Tabia za mwanafunzi wake, si msaada tena.

Nachelea kusema hata mpira uliotufikisha katika nafasi tulizozipata ni zao la tabia zilizojengwa na waliotangulia.

Mwalimu mkali anaficha madhaifu yake ya kukosa umahili katika kufundisha. Silaha kubwa ya walimu Kama hawa ni kujenga hofu kwa mwanafunzi hali inayompelekea mwanafunzi kukosa confidence na hata kufeli.

Tujiulize Ziko wapi pass milioni zileee!

Wachezaji si walewale!

Leo wachezaji hawaonani, wanapapara, wanakitete hawana nguvu na majeruhi. Kulikoni?

Tutafakari vizuri kwa vile ni kipindi muhimu Cha kujenga au kubomowa timu. Tutaacha wachezaji wazuri kwa kufuata kinachoitwa ripoti ya mwalimu ambae mwenyewe ndio tatizo.

Ni ivyo tuuu.
wachezaji wazee sana ww kama kocha utamfundisha nn nyoni,onyango,kagere
 
Biñafsi nakubali Sana kocha wa Azam Yule muethiopia sijui msomali yule
Achana na huyo, hawezi kuipeleka Simba popote.Hana uzoefu na mashindano makubwa.Ni bora wamchukue kocha wa ASEC MEMOSAS aliifanya timu yake kuonyesha upinzani mkubwa kwenye kundi la Simba kwenye CAFCC, au wapambane wamng’oe Ibenge kutoka Berkane.
 
Huyu Kocha akiwepo tu mpaka December basi tukijitahidi msimu ujao ni nafasi ya 3.. Maana kama Pablo angeanza na Simba tokea mwanzo wa msimu ubovu ungekuwa maradufu zaid ya sasa.
 
Hoja yako ni ya msingi kabisa. Lkn hoja inakosa support ya vielelezo vya ndani ya timu, kwamba Pablo ni tatizo hasa ktk nini, Ni nini anafanya, au Ni namna gani anaongoza benchi la fundi ktk hali ulizozitaja. Ni ushuhuda wa wachezaji wenyewe au Ni ushahidi gani ulio nao kutoka ndani ya kambi ya mazoezi ya timu.

Pili kwa mtazamo wangu , naona bado kocha alijitahidi kuifikisha timu hapo ilipo kwa aina ya wachezaji tulio nao. Labda kigezo na kipimo kiwe Ni kocha aliyeondoka yaani Didier Gomez da Rosa.

Technically unataka kusema angekuwepo Gomez timu ingekuwa na performance bora zaidi? Kwa hawa hawa Kagere, bocco na mugalu? Au akija kocha mwingine akapewa kikosi hiki hiki ataperform vzr zaidi? Pengine km siyo Pablo Simba ingeweza kutetea ubingwa?

Kwamba Kagere, Bocco, Mugalu hawafungi kwasababu ya ubovu wa kocha?

Binafsi sina tatizo na Pablo, Cha kufanya Simba ifanye usajili wa maana (wavunje benki),wafanye usajili wa kushindana na klabu kubwa km Berkane,Wydad,( labda tatizo liwe uchumi) Ikiwezekana wamrejeshe Gomez km kocha msaidizi , matola aondoke.

Tumesikia tetesi Simba inawahitaji Adebayor, Azizi Ki, Etouga mfungaji kinara wa Asante Kotoko, Zemanga Soze toka Mazembe, Moses Phiri, lkn inaonekana km Simba hawako siriaz, Sababu tunasikia Adebayor keshasaini Berkane. Hakuna kitu kibaya ktk usajili kama kuhitaji wachezaji fulani halafu ukawakosa, wachezaji ambao wana viwango halafu ukashindwa kuwasajili. Matokeo yake ni kufanya usajili ilimradi.

Wachezaji wa ligi za Afrika Mashariki,Burundi, Rwanda , Uganda, Kenya NK hawawezi kukupa matokeo hasa ktk mechi za kimataifa. Hawa ni wa viwango vya chini na kati, wengi hawana exposure kimataifa.

Tatizo la Simba ni aina ya wachezaji waliopo kwa sasa hasa hawa wa nje. Sidhani km ni kocha. Tunahitaji usajili mkubwa.
Tuchangieni basi usajili ili msimu ukianza tuwe na TIMU tunayoihitaji.
Mie naanza na jero.
 
Achana na Pablo mimi nina hasira na Matola, Matola yupo Simba kwa zaidi ya miaka minne lakini unaona kabisa mchango wake kama kocha msaidizi kwa timu ni sifuri.

Kocha mpaka ligi inaelekea ukingoni hana first eleven wakati Matola ilitakiwa awe msaada kumwambia kocha wachezaji wazuri wa kwenye timu! Matokeo yake kaua kiwango cha Lwanga, Bwalya, Kagere, Bocco na hata Chama ambaye amekuwa hapewi nafasi kabisa.

Ni muda sasa wakuachana na Matola huyo ndio mchawi wetu.
Umeongea kweli first eleven ya misimu iliyopita walikosekana chama na miquison tu na replacement ikafanyika,kwanini wasingepewa kipaombele,haiwezekani viwango vyote vya wachezaji wakali kama vishuke kwa pamoja
 
Back
Top Bottom