Tabia za Mwalimu zinamchango mkubwa kwa mwanafunzi kufauru somo. Mwalimu ni kiungo katika kunogesha akili ya mwanafunzi. Mwalimu anaweza kuwa na digriii mia moja, lakini akikosa sifa moja muhimu ya kujuwa kuishi na kukabiliana na mazingira anayofanyia kazi na kusoma maisha na Tabia za mwanafunzi wake, si msaada tena.
Nachelea kusema hata mpira uliotufikisha katika nafasi tulizozipata ni zao la tabia zilizojengwa na waliotangulia.
Mwalimu mkali anaficha madhaifu yake ya kukosa umahili katika kufundisha. Silaha kubwa ya walimu Kama hawa ni kujenga hofu kwa mwanafunzi hali inayompelekea mwanafunzi kukosa confidence na hata kufeli.
Tujiulize Ziko wapi pass milioni zileee!
Wachezaji si walewale!
Leo wachezaji hawaonani, wanapapara, wanakitete hawana nguvu na majeruhi. Kulikoni?
Tutafakari vizuri kwa vile ni kipindi muhimu Cha kujenga au kubomowa timu. Tutaacha wachezaji wazuri kwa kufuata kinachoitwa ripoti ya mwalimu ambae mwenyewe ndio tatizo.
Ni ivyo tuuu.
Hoja yako ni ya msingi kabisa. Lkn hoja inakosa support ya vielelezo vya ndani ya timu, kwamba Pablo ni tatizo hasa ktk nini, Ni nini anafanya, au Ni namna gani anaongoza benchi la fundi ktk hali ulizozitaja. Ni ushuhuda wa wachezaji wenyewe au Ni ushahidi gani ulio nao kutoka ndani ya kambi ya mazoezi ya timu.
Pili kwa mtazamo wangu , naona bado kocha alijitahidi kuifikisha timu hapo ilipo kwa aina ya wachezaji tulio nao. Labda kigezo na kipimo kiwe Ni kocha aliyeondoka yaani Didier Gomez da Rosa.
Technically unataka kusema angekuwepo Gomez timu ingekuwa na performance bora zaidi? Kwa hawa hawa Kagere, bocco na mugalu? Au akija kocha mwingine akapewa kikosi hiki hiki ataperform vzr zaidi? Pengine km siyo Pablo Simba ingeweza kutetea ubingwa?
Kwamba Kagere, Bocco, Mugalu hawafungi kwasababu ya ubovu wa kocha?
Binafsi sina tatizo na Pablo, Cha kufanya Simba ifanye usajili wa maana (wavunje benki),wafanye usajili wa kushindana na klabu kubwa km Berkane,Wydad,( labda tatizo liwe uchumi) Ikiwezekana wamrejeshe Gomez km kocha msaidizi , matola aondoke.
Tumesikia tetesi Simba inawahitaji Adebayor, Azizi Ki, Etouga mfungaji kinara wa Asante Kotoko, Zemanga Soze toka Mazembe, Moses Phiri, lkn inaonekana km Simba hawako siriaz, Sababu tunasikia Adebayor keshasaini Berkane. Hakuna kitu kibaya ktk usajili kama kuhitaji wachezaji fulani halafu ukawakosa, wachezaji ambao wana viwango halafu ukashindwa kuwasajili. Matokeo yake ni kufanya usajili ilimradi.
Wachezaji wa ligi za Afrika Mashariki,Burundi, Rwanda , Uganda, Kenya NK hawawezi kukupa matokeo hasa ktk mechi za kimataifa. Hawa ni wa viwango vya chini na kati, wengi hawana exposure kimataifa.
Tatizo la Simba ni aina ya wachezaji waliopo kwa sasa hasa hawa wa nje. Sidhani km ni kocha. Tunahitaji usajili mkubwa.