Mapema Leo wakati Rais Samia yupo Tegeta jimbo la Kawe kwa Mchungaji Gwajima akiongea na wananchi na wakazi wa Kawe waliojitokeza kumsikiliza ameongea mengi lakini kati ya hayo ni pale aliposema "Gwajiboy oyeee, tunachanja, hatuchanji? Haya mheshimiwa gwajima endelea"
Your browser is not able to display this video.
Kwa kauli hii Spika na Waziri wa Afya wako na hali gani kwa sasa?
Je, tuendelee kutegemea hatua zozote kutoka kwenye chama (CCM) dhidi ya Gwajiboy?
Leo wakati Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akielekea Bagamoyo kurecord filamu ya kutangaza utalii wa Tanzania alisimama kwenye jimbo la Kawe ili kusalimia wananchi.
Rais alimsimamisha Mbunge wa Kawe ili kutoa neno lakini kabla ya kumsimamisha aliwauliza wananchi wa Kawe kama watachanja au la kama video inavyoonyesha hapa chini.Katika hali ya kustaajabisha na ya kushangaza wananchi walimwambia Rais bila ya kupepesa macho kuwa hawatachanja kama video hii inavyoonyesha hapa chini.
Nimejiuliza maswali mengi sana.Kwa nini Rais aulize swali hilo kwenye jimbo ambalo mbunge wake hakubaliani na mambo ya chanjo?Ina maana Rais hajui kwamba kazi kubwa ambayo walifanya katika awamu ya tano ya kupinga chanjo ilifanikiwa sana hasa ukizingatia kuwa kazi hiyo ilifanyika katika Taifa lenye umasikini mkubwa sana wa akili?
My take:
Kwa sasa hivi serikali ya CCM inapata shida sana kula matapishi yake yenyewe ambayo waliyatapika katika awamu ya tano.Ni vyema serikali ikiri mbele ya wananchi kuwa Rais Magufuli hakuwa sahihi na alipotosha sana uma ili wananchi waanze upya kuelimishwa juu ya gonjwa la Corona na chanjo.
Ule ni mchezo tu niliwaandikia hapa kwamba CCM na bunge lao hawana uwezo wa kumfukuza hata mbunge mmoja,yaani afukuzwe mbunge ? aloo wanatafuta mboga kumwagwa walichokitifua kwenye uchaguzi mkuu uliopita ni jambo baya sana sana sana,si raisi si wabunge inabidi walindane tu na kusitiriana.
Sema hii serikali haieleweki...ikumbukwe Ndugai kasema Aajibishwe endapo haitokua hivo Wazari wa mambo ya Ndani ataitwa Na sijui hadi mda huu ile kamatai ya ndugai nayo inajisikiaje kwa kweli inafikia wakati Mama unamwacha aende anavyoenda tu.