Tuungane kukemea ajali hizi, nyingi zina uzembe ndani yake

Kuna siku walikuwa wanafanya ligi STK Vs SM aisee ilikuwa balaa maana wote walikuwa wamewasha taa full alafu pale kwenye dashboard kuna kimulimuli...
Dodoma - morogoro ndiyo kipande Chao cha kufanya ligi
 
Kuna siku walikuwa wanafanya ligi STK Vs SM aisee ilikuwa balaa maana wote walikuwa wamewasha taa full alafu pale kwenye dashboard kuna kimulimuli...
Dodoma - morogoro ndiyo kipande Chao cha kufanya ligi
Dah hii kitu mkuu inauma pale utaposikia kuwa wamesababisha umauti wa watu wengine ni bora wafe wao wanaoshindana ligi za barabarani ambazo ni za kijinga na kipuuzi mana wanasababisha vifo vya watu wengine ambao hawana hatia sijui serikali haioni au makusudi tu
 
Huwa wanakimbilia wapi, je kwa mwendo wa kawaida tu hawatafika?

Ona sasa damu hizi zimemwagika za watanzania ambao wote walikuwa na malengo ya maisha yao.

Hiyo gari iliyoingia kwenye msafara ndo kama ile ya yule mkimbizi aliyevamia msafara ya Sokoine.

RIP good souls.
 
Lawama zote zimfikie Jiwe popote alipo
 
Mnaachwa yatima halafu unaachiwa wategemezi kibao
 

Madereva wabaya kabisa wasiokuwa na chembe ya uheshimu wa sheria barabarani ni wa magari uliyoyataja. Ila wahanga wa kusumbuliwa na polisi mabaradhuli ni wale madereva bora kabisa yaani wa malori na mabasi.

No wonder polisi Tanzania wenye heshima zaidi ni kina Kingai, Goodluck, Mahita na kina Jumanne wakikimbilia kusikojulikana na kina Tito Magoti, Kabendera na kina Ben. Kama vile haitoshi leo wako mahakamani kujaribu kumfunga Mh. Mbowe miaka 30.

Wapigwe Vita Polisi kunyang'anya madereva leseni
 
Dah! Juzi kati Kuna dogo wa Boda kapata ajali kwa kugonga gari ambayo ilisimama ghafla bila ishara yoyote, kumbe ni gari ya Askari.

Kwa kifupi, Dogo aligeuziwa kosa na maelezo yakaandikwa ambayo yangeenda mbele au yule abiria kama angekufa basi dogo alikua anabebeshwa Zigo kubwa sana, anyway ndio maisha tuliyoyachagua
 
Ajali zinatumaliza.
 
Yaani ni Bora wafe wenyewe tu kuliko kusababisha na wengine wapoteze uhai kwajili ya uzembe wao
 
Kuna haya ma Iveco ya jeshi la wananchi, yenyewe yakikugonga hawanaga hata muda wa kusimama sijui wao sheria haziwahusu!?
Aisee nilishuhudia miezi 2 iliyopita bus la jeshi limempiga pasi jamaa mwenye Toyota premio pale mitaa ya mission- mbagala lakini cha ajabu bus la jeshi halikusimama likaishia zake,usiombe hawa watu serikali wakugonge Bana!!!hiyo kesi itageuzwa kwakooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…