Tuungane kukemea ajali hizi, nyingi zina uzembe ndani yake

Hizi gali za serikali nchi nzima ndio vinara wa kusababisha ajali, kwanza hawajali kabisa sehemu yapaswa kutembea mwendo mdogo wao spidi zote wanamaliza alafu hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na polisi wamekaa tu, iyo ajali ya jana ni uzembe matokeo yake watu wamepoteza wapendwa wao bila sababu za msingi eti wanaenda kukagua miradi maspidi makubwa ambayo ayana tija yoyote matokeo yake miajali
Kuna siku walikuwa wanafanya ligi STK Vs SM aisee ilikuwa balaa maana wote walikuwa wamewasha taa full alafu pale kwenye dashboard kuna kimulimuli...
Dodoma - morogoro ndiyo kipande Chao cha kufanya ligi
 
Dah hii kitu mkuu inauma pale utaposikia kuwa wamesababisha umauti wa watu wengine ni bora wafe wao wanaoshindana ligi za barabarani ambazo ni za kijinga na kipuuzi mana wanasababisha vifo vya watu wengine ambao hawana hatia sijui serikali haioni au makusudi tu
 
Huwa wanakimbilia wapi, je kwa mwendo wa kawaida tu hawatafika?

Ona sasa damu hizi zimemwagika za watanzania ambao wote walikuwa na malengo ya maisha yao.

Hiyo gari iliyoingia kwenye msafara ndo kama ile ya yule mkimbizi aliyevamia msafara ya Sokoine.

RIP good souls.
 
Kuna ile ajali ya TRA, yaani wanaona wao ndo wana haki ya kuwahi,wanatanua wanawasha mataa ole wako usipishe?
Unategemea hawa ndi madereva kutoka NIT wanaujuzi wote lakini ndo majanga zaidi.
Kunakipindi kampuni zinazohusika na kujaza mafuta kwenye minara ya simu ziliweka namba za simu na maneno yameandikwa "Ninaendeshaje?" . Baada ya muda mfupi madereva wote walikuwa wanaendesha kwa nidhamu.
Naona hata hili litumike pawe na namba tureport pia polisi wafanye kazi yao.
Lawama zote zimfikie Jiwe popote alipo
 
Dah hii kitu mkuu inauma pale utaposikia kuwa wamesababisha umauti wa watu wengine ni bora wafe wao wanaoshindana ligi za barabarani ambazo ni za kijinga na kipuuzi mana wanasababisha vifo vya watu wengine ambao hawana hatia sijui serikali haioni au makusudi tu
Mnaachwa yatima halafu unaachiwa wategemezi kibao
 
Ni takribani mwezi na Kidogo tangu gari ya serikali ipate ajali mbaya sana na kuwamaliza abiria wote. Ilikua STL iliyoaminika kuwa ilikua ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Leo Tena gari ya serikali imeondoka na roho 14 za Watanzania ambao ni nyuma Yao wanategemewa na familia zao na ndugu zao.

Kuna tukio lingine (sikumbuki vyema) la gari la Jeshi kusababisha ajali.

Hii ni mifano michache tu inayoumiza saana maana tunavyoandika muda huu Kuna watoto tayari wameshakua yatima... inaumiza sana!

Chanzo Cha ajali nyingi za magari ya serikali ni mwendokasi na kutokujali alama za barabarani huku Askari waliokabidhiwa ada ya kusimamia Sheria na kanuni wakiishia kuwabana Maderava wa magari binafsi.

Magari ya Polisi, Serikali, Jeshi, Mahakama na wengine wa dizaini Yao ndio wanaongoza kwa kuvunja Sheria na kanuni za matumizi ya Barabara bila kuchukuliwa hatua.

Mfano, Leo ni gari ngapi za Polisi ambazo hazina usajili kamili? Zinatumia namba za Malaysia na nchi nyingine as if ni sahihi, mambo kama haya ndio wahalifu kama Akina Sabaya walitumia namba bandia kuvamia makazi ya Mbowe.

STL, STK, STJ, SU, JW na wengine hakuna anayeona kibao Cha 50km/hr Wala Zebra crossing 🚸. Wakitaka kupita Wala hawaangalii Wala kuchukua tahadhari yoyote matokeo yake ajali ikitokea Polisi wanakubebesha wewe, rejea ajali ya Tanga ambapo RTO Tanga aliandika maelezo ya uongo.

Wakuu, tumezika sana inatosha, tumelia sana inatosha! Polisi waache kuwaogopa, wasimamie haki.

Pia sio lazima misafara ya Viongozi iendeshwe kwa speed Hali Barabara zetu na magari yetu havina ubora huo. Rejea ajali ya DC wa Moro na yule Mkurugenzi Binti wa Morogoro sikumbuki wilaya.

Nyingi ni uzembe, TUANZE KUWARIPOTI POLISI AMBAO HAWAWACHUKULII HATUA MADEREVA WA SERIKALI wanaovunja Sheria ikiwa ni pamoja na abiria wao kutokufunga mikanda wawapo safarini.

Tujifunze kwa International NGOs Tena hapa bongo ambapo kama Boss au Abiria hajafunga belt dereva anaruhusiwa kutokuondosha gari Hadi ufunge.

Madereva wabaya kabisa wasiokuwa na chembe ya uheshimu wa sheria barabarani ni wa magari uliyoyataja. Ila wahanga wa kusumbuliwa na polisi mabaradhuli ni wale madereva bora kabisa yaani wa malori na mabasi.

No wonder polisi Tanzania wenye heshima zaidi ni kina Kingai, Goodluck, Mahita na kina Jumanne wakikimbilia kusikojulikana na kina Tito Magoti, Kabendera na kina Ben. Kama vile haitoshi leo wako mahakamani kujaribu kumfunga Mh. Mbowe miaka 30.

Wapigwe Vita Polisi kunyang'anya madereva leseni
 
Madereva wabaya kabisa wasiokuwa na chembe ya uheshimu wa sheria barabarani ni wa magari uliyoyataja. Ila wahanga wa kusumbuliwa na polisi mabaradhuli ni wale madereva bora kabisa yaani wa malori na mabasi.

No wonder polisi Tanzania wenye heshima zaidi ni kina Kingai, Goodluck, Mahita ba kina Jumanne wakimkimbia na kina Tito Magoti, Kanendera na kina Ben. Kama vile haitoshi leo wako mahakamani kujaribu kumwunga Mh. Mbowe miaka 30.

Wapigwe Vita Polisi kunyang'anya madereva leseni
Dah! Juzi kati Kuna dogo wa Boda kapata ajali kwa kugonga gari ambayo ilisimama ghafla bila ishara yoyote, kumbe ni gari ya Askari.

Kwa kifupi, Dogo aligeuziwa kosa na maelezo yakaandikwa ambayo yangeenda mbele au yule abiria kama angekufa basi dogo alikua anabebeshwa Zigo kubwa sana, anyway ndio maisha tuliyoyachagua
 
Ni takribani mwezi na Kidogo tangu gari ya serikali ipate ajali mbaya sana na kuwamaliza abiria wote. Ilikua STL iliyoaminika kuwa ilikua ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Leo Tena gari ya serikali imeondoka na roho 14 za Watanzania ambao ni nyuma Yao wanategemewa na familia zao na ndugu zao.

Kuna tukio lingine (sikumbuki vyema) la gari la Jeshi kusababisha ajali.

Hii ni mifano michache tu inayoumiza saana maana tunavyoandika muda huu Kuna watoto tayari wameshakua yatima... inaumiza sana!

Chanzo Cha ajali nyingi za magari ya serikali ni mwendokasi na kutokujali alama za barabarani huku Askari waliokabidhiwa ada ya kusimamia Sheria na kanuni wakiishia kuwabana Maderava wa magari binafsi.

Magari ya Polisi, Serikali, Jeshi, Mahakama na wengine wa dizaini Yao ndio wanaongoza kwa kuvunja Sheria na kanuni za matumizi ya Barabara bila kuchukuliwa hatua.

Mfano, Leo ni gari ngapi za Polisi ambazo hazina usajili kamili? Zinatumia namba za Malaysia na nchi nyingine as if ni sahihi, mambo kama haya ndio wahalifu kama Akina Sabaya walitumia namba bandia kuvamia makazi ya Mbowe.

STL, STK, STJ, SU, JW na wengine hakuna anayeona kibao Cha 50km/hr Wala Zebra crossing 🚸. Wakitaka kupita Wala hawaangalii Wala kuchukua tahadhari yoyote matokeo yake ajali ikitokea Polisi wanakubebesha wewe, rejea ajali ya Tanga ambapo RTO Tanga aliandika maelezo ya uongo.

Wakuu, tumezika sana inatosha, tumelia sana inatosha! Polisi waache kuwaogopa, wasimamie haki.

Pia sio lazima misafara ya Viongozi iendeshwe kwa speed Hali Barabara zetu na magari yetu havina ubora huo. Rejea ajali ya DC wa Moro na yule Mkurugenzi Binti wa Morogoro sikumbuki wilaya.

Nyingi ni uzembe, TUANZE KUWARIPOTI POLISI AMBAO HAWAWACHUKULII HATUA MADEREVA WA SERIKALI wanaovunja Sheria ikiwa ni pamoja na abiria wao kutokufunga mikanda wawapo safarini.

Tujifunze kwa International NGOs Tena hapa bongo ambapo kama Boss au Abiria hajafunga belt dereva anaruhusiwa kutokuondosha gari Hadi ufunge.
Ajali zinatumaliza.
 
Dah hii kitu mkuu inauma pale utaposikia kuwa wamesababisha umauti wa watu wengine ni bora wafe wao wanaoshindana ligi za barabarani ambazo ni za kijinga na kipuuzi mana wanasababisha vifo vya watu wengine ambao hawana hatia sijui serikali haioni au makusudi tu
Yaani ni Bora wafe wenyewe tu kuliko kusababisha na wengine wapoteze uhai kwajili ya uzembe wao
 
Kuna haya ma Iveco ya jeshi la wananchi, yenyewe yakikugonga hawanaga hata muda wa kusimama sijui wao sheria haziwahusu!?
Aisee nilishuhudia miezi 2 iliyopita bus la jeshi limempiga pasi jamaa mwenye Toyota premio pale mitaa ya mission- mbagala lakini cha ajabu bus la jeshi halikusimama likaishia zake,usiombe hawa watu serikali wakugonge Bana!!!hiyo kesi itageuzwa kwakooo
 
Back
Top Bottom