Tuungane kukemea ajali hizi, nyingi zina uzembe ndani yake

Pamoja na hilo ila bado tuna sheria mbovu sana za usalama barabarani pia rushwa kuwa kubwa, ukitaka kujua hivyo tembelea nchi ya rwanda suala la ajili liko chini sana kwa sababu ya sheria kali na usimamizi wa sheria hizo, tanzania mtu akiisha jua tu kuendesha gari basi ndo imeisha hivyo
 

Sheria mbovu na tutaisha sana

Hao police waliisharuhusiwa kula hongo
Yaani Rais mzima anapanga sheria zake eti hela ya brush
Siwezi kuendesha huko kabisa
 

Ukweli mchungu polisi wakiwamo wa usalama barabarani hawafai, hawana ujuzi, ni mzigo na utendaji kazi wao ni manufaa yao binafsi:

Dharau za polisi usalama barabarani

Ukisikia watu wanahojiwa na kuwasifia kwenye zikiwamo kadhia zao nyingi, ni katika kukwepa visasi vyao tu:

Rais Samia: Polisi hawatakiwi kutisha watu wanapowakamata
 
Msafara wa POTUS hauzidi 100kph. Huu wetu wanatembea 120+ mjini wanawahi nini?
 

unagonga mtu kwa kusimama ghafla na unataka kutetewa!!!!

huu udereva wa wapi??ukiwa barabarani usalama wako dhidi ya chombo cha mbele yako ni juu yako.

story za alisimama ghafla,alikata kona ghafla,alifungua mlango ghafla,sijui aliangusha kopo la maji hazipo.
muachie 3m na zaidi kwa mwendo wa tahadhari,sio unamnusa nyuma kama beberu anatafuta stimu kwa jike.
 
Sheria mbovu na tutaisha sana

Hao police waliisharuhusiwa kula hongo
Yaani Rais mzima anapanga sheria zake eti hela ya brush
Siwezi kuendesha huko kabisa

mkuu wacha kukimbia tatizo kwa kumsingizia rais au mtu mwingine.

polisi wanachukua rushwa kwa matatizo yako,sio yao.wewe umekosa kujitambua halafu mzigo akabebeshwe traffic!!!magu hakuwa mnafiki na ndio dawa ya matatizo.

unashikwa na traffic kwa tyre kipara unampa 5k shida iko kwa magu au kichwa chako kibovu!!!hao madereva wa STL na ndugu zao ni jamii hii hii ya watz wasiojitambua,tofauti kwao ni kwamba hawatoi rushwa zinazowauma wengine kutoa.
 
Haya yote kasababisha Rais Samia pale tu alipo kemea polisi wa barabarani kutokutumia makosa ya barabarani kama moja ya chanzo cha mapato ,hivyo kusababisha wenye magari na madereva kutokujali chochote maana kipindi cha magufuli ajali zilipungua kwa zaidi ya asilimia 76% kutokana na traffic kuwa wakali na makini kutafuta kila makosa ila sasa ajali zimeongezeka ×3 ya alivyo acha JPM
 
Kwenye kadhia hii yapo pia magari ya DFP, DFPA Mkuu.
 

Rushwa ni mfumo mliotengeneza wote na haitaisha sio njaa bali ndio way of life in most countries

Mimi siishi huko kwa miaka zaidi ya 40 sasa ila nachangia tu
Nilipo sheria zimetungwa na zinafuatwa
Huwezi kuletewa leseni ofisini kama huko, huwezi kusimamishwa ukakutwa umelewa ukaachiwa kisa una hela

Hakuna wa kulaumiwa zaidi ya sheria zinazovunjwa na serikali ikijua hilo
Huku sijavunja sheria kwa zaidi ya miaka 30 na kila leo niko barabarani naendesha na sijawahi kusimamishwa na police unajua kwanini? Sheria kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…