Tuwaadhibu walioharibu miundombinu yetu

Tuwaadhibu walioharibu miundombinu yetu

TEC ndiyo wanaowateka mchana kweupe na kwenda kuwatesa au kuwaua, kuwafunga kwa kesi za mchongo, kuwaibia kura zao kwa kuwatangaza washindi feki, kuwaengua kwenye uchaguzi kwa hila, kuuza raslimali kwa waarabu, nk!! Ok.
Hakuna aliyechoma miundombinu na kuiba mali za watu kisa watu kutekwa
Waliofanya vurugu walifanya kutimiza no reforms no election ambayo lissu alishauriwa na viongozi wa dini
 
Watanzania wengi kama sio wote wako nyuma ya serikali yao, serikali ilichofanya kuzima uharibifu ule kilikuwa sawa kabisa na kinaungwa mkono na watanzania wengi. Kama wananchi wasingekuwa nyuma yake ungeshaona maandamano ya nchi nzima kila nyumba, kila kitongoji, kila mtaa, kila barabara kote kuanzia kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi taaifa watu wanampinga kupinga mauaji. Ukiona wahalifu wamedhibitiwa kirahisi namna ile maana yake walikuwa hawaungwi mkono na wananchi walio wengi; walikuwa wavuta bangi wachache waliostahili kudhibitiwa haraka kabla hawajachoma mali zetu nyingi.

Yani wewe ukikuta mkeo anabakwa utamlaumu mkeo kwa kuwa na uchi na matiti yaliyomvutia mbakaji?

Waliochoma nchi sio wananchi bali wahuni wachache tu, maana hakuna jeshi duniani linaloweza kuzuia maandamano ya wananchi wake waliokasirikia serikali.

Na kama wananchi wangekuwa wamekasirishwa na mauaji yale basi mitaa yote ingefurika wananchi wanaolaani mauaji ya ndugu zao. Kifupi wananchi wako nyuma ya serikali yao.
Naona unapenda sana kuongelea habari za kubakwa! Vipi, umeshawahi kufanyiwa hivyo vitendo? Maana mfano wako naona ni irrelevant.
 
Kwa hiyo walioharibi miundombinu wasishughulikiwe kisheria kisa kuna watu waliuawa, hizo akili au tope?.. ndivyo mnavyoambiana kanisani!?..maana ukitajwa uharibifu mnakimbilia waliouawa,wangetulia kwao wangeuawa?
Kaka wameshikwa pabaya safari hii. Wakipelekwa mahakamani wanajitahidi kuweka mapingamizi wasishitakiwe, tume ya uchunguzi/ugunduzi/ufichuaji ikiundwa wanakimbilia mahakani kupinga isifanye kazi maana watafahamika wote. Kote huko ni kupayapaya. Lazima tuwaadhibu kwa kuharibu mali zetu, kutuzuia kupata haki zetu za kupewa huduma kwenye miundombinu (usafiri, polisi, TRA, serikali za mitaa, sheli, nk) waliyoharibu, kututia taharuki, usumbufu na hasara kwenye biashara zetu.

Haki zao haziwezi kuingilia hali zetu. Kwani wanaCCM hawajui ziliko mali za wanachadema? mbona wao hawakwenda kuziharibu kulipa kisasi?
 
hii tabia lazima ikome, kuharibu miundo mbinu iwe death penalty
Kama wananchi wanamuua kibaka aliyewapora simu sembuse hawa wakora waliochoma mwendokasi wao unaowasaodia kwenda feri kuchukua samaki? Hawa ni vibaka sana na panyaroad lazima tuwasake na kuwapa adhabu.
 
Naona unapenda sana kuongelea habari za kubakwa! Vipi, umeshawahi kufanyiwa hivyo vitendo? Maana mfano wako naona ni irrelevant.
Mfano ni sahihi kabisa kwakuwa wewe unadai kuna watu waliosababisha vijana waende kuchoma nchi yao. Hakuna sababu halali itakayomfanya mtu akachome kituo cha polisi, TRA, mahakama, barabara, ofisi za serikali, nk. Yaani ukimkasirisha mwanao anaenda kulipiza kwa kutembea na mke wako (mama yake)?
 
Kama tuna ushahidi kuwa miundombinu yetu na ya watu binafsi iliharibiwa kwenye vurugu za Oktoba 29 lazima walioiharibu na waliopanga uharibifu wakamatwe na kuadhibiwa mara moja ili iwe fundisho kwa wengine.

Yatakuwa makosa makubwa kama watu hawa wataachwa bila kuadhibiwa, itaacha kumbukumbu mbaya kwa taifa.

Kama serikali ikishindwa kuwachukulia hatua watu waliofanya makosa makubwa kama haya tutaiondoa madarakani kwa kushindwa kulinda kodi zetu ipasavyo. Haifai kuendesha nchi. Nchi haiendeshwi kwa kutumia moyo na utashi, bali Katiba na sheria za nchi. Uchaguzi na namna unavyoendeshwa uko ndani ya katiba na sheria zetu ambazo viongozi waliapa kuilinda.
Je walioua ndugu zetu nao tuwafanyaje?
 
Tungeanza kwanza na wale waliosababisha hao vijana kupandwa na hasira kiasi cha kufikia hiyo hatua ya kuharibu hiyo miundombinu.

Unadhulumu watu haki zao za msingi mchana kweupe kwa kuwateka, kuwaua, kuwaibia kura zao, kuwaengua kugombea kwenye uchaguzi, kuiuza nchi yao kwa wageni, kuwahamisha kinguvu kwenye maeneo yao ya asili ili kuwapa hayo maeneo wajomba zako, kuwafunga kwa kesi feki za ugaidi na uhaini, nk. halafu unategemea wabakie kondoo milele!
Naani kijana akishikwa na nyege kwa kumuona mwanamke mwenye matako makubwa anaruhusiwa kumbaka? Hovyoo!!!
 
hao ndo pekee wanaostahili maridhiano, vp wale wachomaji?
Hao ni wachache kati ya waliouawa kimakosa ambao wanafahamika ,wengi hawana majina na wameuawa kimakosa ,wahalifu wengi waliochoma na kuiba mali hawakuuawa....Ninaweza kukuthibitishia 30% waliouawa ni kati ya hao wahalifu ila 70% wameuawa kimakosa.
 
Back
Top Bottom