Tuwaadhibu walioharibu miundombinu yetu

Tuwaadhibu walioharibu miundombinu yetu

Wanaomshauri Mama afanye maridhiano na hahaini wanaompinga wanamwingiza kwenye mkenge, hatatoka humo. Maridhiano hayo yatakwenda kumdhoofisha na kumbagaza Mama badala ya kumjenga. Anaotaka kufanya maridhiano nao ni wale ambao walipinga Samia asiwe Rais baada ya JPM kuaga dunia. Walikuwa wanapinga kwa sababu na maslahi yao ambayo hata wakati wa uteuzi wa nani agombee kupitia CCM walimpiga asiteuliwe na hata sasa ni chanzo cha uhaini huu.

Kwenye maridhiano hayo bila shaka Samia atakwenda kuambiwa aiondoe DP world, awarejeshee wapigaji machimbo yao pale bandarini. Atakwenda kupewa masharti kibao yanayolirudisha taifa lilikotoka.
 
Kwa hiyo walioharibi miundombinu wasishughulikiwe kisheria kisa kuna watu waliuawa, hizo akili au tope?.. ndivyo mnavyoambiana kanisani!?..maana ukitajwa uharibifu mnakimbilia waliouawa,wangetulia kwao wangeuawa?
Hizo ni Akili za Misikitini mnazofundishwa na Masheikhe Ubwabwa wenu??
Mnafikiria miundombinu ni bora kuliko maisha ya watu ama kweli Misikitini mnalishwa Matango-Pori!!!
 
Kama tuna ushahidi kuwa miundombinu yetu na ya watu binafsi iliharibiwa kwenye vurugu za Oktoba 29 lazima walioiharibu na waliopanga uharibifu wakamatwe na kuadhibiwa mara moja ili iwe fundisho kwa wengine.

Yatakuwa makosa makubwa kama watu hawa wataachwa bila kuadhibiwa, itaacha kumbukumbu mbaya kwa taifa.

Kama serikali ikishindwa kuwachukulia hatua watu waliofanya makosa makubwa kama haya tutaiondoa madarakani kwa kushindwa kulinda kodi zetu ipasavyo. Haifai kuendesha nchi. Nchi haiendeshwi kwa kutumia moyo na utashi, bali Katiba na sheria za nchi. Uchaguzi na namna unavyoendeshwa uko ndani ya katiba na sheria zetu ambazo viongozi waliapa kuilinda. Hakuna mtu angeweza kuvunja Katiba kwa kufanya uchaguzi ulio nje ya Katiba hadi hapo Katiba nyingine itakapoandikwa na kupitishwa kutumika. Hivyo, aliyetaka kusimamisha uchaguzi alikuwa anakwenda kinyume na katiba. Kwanini serikali isiwachukulie hatua watu waliochoma vituo vya kupigia kura? Ndiyo kuilinda katiba huko?

Utafanye maridhiano na watu waliovunja Katiba (kuchoma vituo vya kupigia kura) na kuchoma mali za wananchi? HUo ni woga au kushindwa kuongoza nchi? Wakati tunafanya maridhiano wale wote waliopanga na kutekeleza kuchoma vituo vya kupigia kura na mali nyingine lazima waende jela kwa mujibu ya sheria zetu.
Juzi mwaka mpya hapa Uholanzi kulikuwa na mashambulizi ya kufa mtu, waandanamaji walikuwa wanashambulia polisi kwa mabomu ya petrol na baruti. Magari yalichomwa moto. Hakuna polsi aliyeua bali walitumia utaalam wao kuzima ghasia. Wewe unatetea polisi waliokuwa wanaua makusudi na waliojeruhiwa anafuatiliwa hospital kumalizwa?
 
hakuna mtu anaweza kukudhuru kama hujafanya kosa lolote haswa kwa tanzania ni nadra sana kutokea, hivo mlicho kitafuta mmekipata, however ni kosa kubwa kulitumia kisiasa kwan kila mtu aliona kabisa uizi uliofanyika pamoja na kuchoma miundo mbinu

hivo basi wewe kuanza kutetea kilichotokea ni kutetea ujinga, however sisi tunajua kabisa mnaitumia kisiasa hivo tunajua namna ya kudeal na tukio kama hilo!

Mngekua mmegusa sana na kilichotokea mngekua mmenda kutoa msaada na pole kwa familia ila kwa kua mmeona njia ndo hio hio basi watu walishawashtukia mda mrefu sana
Ngoja wakikufikia na wewe kisha ujitokeze kuja kuongea utopolo huo unaoongea sasa hivi.
Mali zinatafutwa,wewe tangu uzaliwe ushawahi kuona duka la kuuza roho za watu?
 
Hao ni wachache kati ya waliouawa kimakosa ambao wanafahamika ,wengi hawana majina na wameuawa kimakosa ,wahalifu wengi waliochoma na kuiba mali hawakuuawa....Ninaweza kukuthibitishia 30% waliouawa ni kati ya hao wahalifu ila 70% wameuawa kimakosa.
Collateral damage! Ikifikia Hali kama hiyo unayekutwa kwenye tukio ndiyo unalipia gharama...kwani hao wahalifu walikuwa na badge maalum kwamba polisi anapowatawanya anajuwa huyu ni mhalifu na huyu anaandamana Kwa amani?
 
Ulipokuwa unafyatulia risasi za vichwa wananchi ulikuwa unatekeleza hukumu gani ya mahakama?
Ulitaka wachome na mahakama zote ziishe ndo aanze kupiga. Yaani kuna watu humu JF ni kama watoto wa darasa la pili, ushaambiwa duniani hakuna maandamano ya Aina ile unaanzaje kuandamana Kwa kufanya vandalism? Kupitia Yale maandamano niligundua Kenya wanatuacha mbali Sana kwenye uwezo wa kufikiri.

Halafu kuna wale mnaona vituo vinachomwa halafu mpo mnashangaa kama nyumbu hamjui hatari ya kukaa eneo hilo? mimi sililaumu jeshi la polisi wala vikosi vya ulinzi walikuwa sahihi kabisa na bila kufanya hivyo Leo labda tungekuwa tunabakwa na wanyarwanda kama Congo.
 
Juzi mwaka mpya hapa Uholanzi kulikuwa na mashambulizi ya kufa mtu, waandanamaji walikuwa wanashambulia polisi kwa mabomu ya petrol na baruti. Magari yalichomwa moto. Hakuna polsi aliyeua bali walitumia utaalam wao kuzima ghasia. Wewe unatetea polisi waliokuwa wanaua makusudi na waliojeruhiwa anafuatiliwa hospital kumalizwa?
Ndo muende mkaishi kwenye nchi za hivyo ambazo mtakata wapiga kura vidole na kuchoma miundombinu halafu mchekewe 🤣🤣 hapa kwetu inaitwa mwana ukome na nadhani somo lilishaeleweka ndo maana mentor wenu anatangaza Tu mara D9 mara J1 ila hakuna nyumbu aliyethubutu
 
Tungeanza kwanza na wale waliosababisha hao vijana kupandwa na hasira kiasi cha kufikia hiyo hatua ya kuharibu hiyo miundombinu.

Unadhulumu watu haki zao za msingi mchana kweupe kwa kuwateka, kuwaua, kuwaibia kura zao, kuwaengua kugombea kwenye uchaguzi, kuiuza nchi yao kwa wageni, kuwahamisha kinguvu kwenye maeneo yao ya asili ili kuwapa hayo maeneo wajomba zako, kuwafunga kwa kesi feki za ugaidi na uhaini, nk. halafu unategemea wabakie kondoo milele!

Kwanza hakuna ushajidi wowote kuwa hso vijana ndiyo waliochoma moto magari na vituo vya mafuta. Inawezekana kabisa ilikuwa ni kazi ya watu wa ndani kutafuta sababu ya kunalizana nao.
 
Ndo muende mkaishi kwenye nchi za hivyo ambazo mtakata wapiga kura vidole na kuchoma miundombinu halafu mchekewe 🤣🤣 hapa kwetu inaitwa mwana ukome na nadhani somo lilishaeleweka ndo maana mentor wenu anatangaza Tu mara D9 mara J1 ila hakuna nyumbu aliyethubutu
We are not going anywhere; we will remain right here in our country and make sure that all the killers are brought to justice and that the nation gets leaders who are truly elected by the people
 
Watanzania wengi kama sio wote wako nyuma ya serikali yao, serikali ilichofanya kuzima uharibifu ule kilikuwa sawa kabisa na kinaungwa mkono na watanzania wengi. Kama wananchi wasingekuwa nyuma yake ungeshaona maandamano ya nchi nzima kila nyumba, kila kitongoji, kila mtaa, kila barabara kote kuanzia kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi taaifa watu wanampinga kupinga mauaji. Ukiona wahalifu wamedhibitiwa kirahisi namna ile maana yake walikuwa hawaungwi mkono na wananchi walio wengi; walikuwa wavuta bangi wachache waliostahili kudhibitiwa haraka kabla hawajachoma mali zetu nyingi.

Yani wewe ukikuta mkeo anabakwa utamlaumu mkeo kwa kuwa na uchi na matiti yaliyomvutia mbakaji?

Waliochoma nchi sio wananchi bali wahuni wachache tu, maana hakuna jeshi duniani linaloweza kuzuia maandamano ya wananchi wake waliokasirikia serikali.

Na kama wananchi wangekuwa wamekasirishwa na mauaji yale basi mitaa yote ingefurika wananchi wanaolaani mauaji ya ndugu zao. Kifupi wananchi wako nyuma ya serikali yao.
😂😂😂😂
 
Kwanza hakuna ushajidi wowote kuwa hso vijana ndiyo waliochoma moto magari na vituo vya mafuta. Inawezekana kabisa ilikuwa ni kazi ya watu wa ndani kutafuta sababu ya kunalizana nao.
Wewe una akili sana. Mimi mwenyewe kuna eneo fulani nilishuhudia wenyeji wakisema kabla ya kutokea uharibifu wa kuvamia maduka na kuchoma ofisi za ccm na kituo kimoja cha Lake Oil, walitokea vijana kama 7 wenye mwonekano wa ukakamavu wakisafiri kwa pikipiki! Walipofika stendi ya ule Mji walianza kuwafokea vijana wa bodaboda kwa nini wamezubaa tu! Ndani ya dakika chache vurugu zikaanza! Na walikichoma kituo cha mafuta ndani ya muda mchache tu!

Je, uzoefu waliupata wapi? Na wale vijana wageni wenye maumbo ya ukakamavu walitoka wapi? Je, ilikuwaje wakasafiri kutoka eneo moja kwenda lingine pasipo kukamatwa kwenye check points zilizotapakaa kote nchini?
 
Kuna video moja inayomuonyesha kijana akichoma kituo cha mwenfo kasi. Mbona mpaka leo hawajamtambua na kumhoji badala yake wameng"ang'ana na watu wa mtandaoni akina Niffer...!!? Mimi hawa akina Muliro na Mafwele siwaamini kabisa.
 
Kama tuna ushahidi kuwa miundombinu yetu na ya watu binafsi iliharibiwa kwenye vurugu za Oktoba 29 lazima walioiharibu na waliopanga uharibifu wakamatwe na kuadhibiwa mara moja ili iwe fundisho kwa wengine.

Yatakuwa makosa makubwa kama watu hawa wataachwa bila kuadhibiwa, itaacha kumbukumbu mbaya kwa taifa.

Kama serikali ikishindwa kuwachukulia hatua watu waliofanya makosa makubwa kama haya tutaiondoa madarakani kwa kushindwa kulinda kodi zetu ipasavyo. Haifai kuendesha nchi. Nchi haiendeshwi kwa kutumia moyo na utashi, bali Katiba na sheria za nchi. Uchaguzi na namna unavyoendeshwa uko ndani ya katiba na sheria zetu ambazo viongozi waliapa kuilinda. Hakuna mtu angeweza kuvunja Katiba kwa kufanya uchaguzi ulio nje ya Katiba hadi hapo Katiba nyingine itakapoandikwa na kupitishwa kutumika. Hivyo, aliyetaka kusimamisha uchaguzi alikuwa anakwenda kinyume na katiba. Kwanini serikali isiwachukulie hatua watu waliochoma vituo vya kupigia kura? Ndiyo kuilinda katiba huko?

Utafanye maridhiano na watu waliovunja Katiba (kuchoma vituo vya kupigia kura) na kuchoma mali za wananchi? HUo ni woga au kushindwa kuongoza nchi? Wakati tunafanya maridhiano wale wote waliopanga na kutekeleza kuchoma vituo vya kupigia kura na mali nyingine lazima waende jela kwa mujibu ya sheria zetu.
Wewe kweli kondoo
 
We are not going anywhere; we will remain right here in our country and make sure that all the killers are brought to justice and that the nation gets leaders who are truly elected by the people
Then be a nice citizen ( with rights which goes parallel with responsibilities) .
 
Mkuu pamoja na mapungufu yote upande wa serikali lakini wako makini kuliko unavofikiri wewe yote hayo wanajua wao pia wanatamani kutumia hizo sheria lakini wanaangalia taifa linaendaje. Ndomana wakawaachia waliokamatwa sina hakika kama wote kuna Shemu lazima uangalie mazingira yaliyopo mkuu kwa hali tunayoiona mtaani tunahitaji busara sana ndomana waziri Mkuu juzijuz akasema hakutakuwa namshindi kwenye hali hii
 
Back
Top Bottom