Tuwaelimishe vijana wanaoajiriwa sasa kwenye Utumishi wa Umma kuhusu haki na wajibu wao!

Tuwaelimishe vijana wanaoajiriwa sasa kwenye Utumishi wa Umma kuhusu haki na wajibu wao!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Kwa kawaida Serikali huwa imejipanga vizuri sana inapokuwa imetoa kibali cha ajira kwenye utumishi wa umma kuhusu haki na stahiki za waajiliwa wapya. Lakini huwa kuna tatizo kubwa kwa watendaji watekelezaji wa adhima hiyo ya serikali hasa kuhusu eneo la haki na stahiki za waajiriwa wapya.

Mara nyingi watendaji hao hujikita katika kusisitiza wajibu tu wa waajiriwa hawa wapya bila kuwaelimisha pia kuhusa haki na stahiki zao kama waajiriwa wapya kwenye utumishi wa umma.

Ni kwa nadra sana utakuta maafisa utumishi wakiwaelekeza waajiriwa wapya kuhusu haki zao kama vile posho ya kujikimu kwa idadi ya siku zilizobainishwa kwenye miongozo ya serikali, haki ya kupewa fedha kwa ajili ya kusafirisha mizigo kwenye ajira (maana serikali inajuwa kuwa mtu aliyehama toka kwao alikokuwa anaishi na kuhamia kituo chake cha kazi lazima atakuwa na mizigo kama kitanda, nk).

Naomba tuutumie uzi huu:
1. Kuelimishana kuhusu haki na stahiki za waajiriwa wapya kwenye utumishi wa umma.
2. Kuelimishana kuhusu wajibu wa watumishi wa umma.
3. Kupashana uzoefu jinsi wanavyofanyiwa waajiriwa wapya hasa kushusiana na haki na stahiki zao.

Wenye utaalamu na uelewa katika mambo haya tafadhali karibuni sana hapa tujuzane!! Mimi wakati wangu wakati naajiriwa kwa mara ya kwanza (kwa sasa ni msaafu).

Nililipwa posho ya kujikimu siku 14, nililipiwa gharama ya kusafirisha mizigo (personal effects) tani moja na nusu (1,500kg), kwa parcel rate. Nililipiwa nauli first class (nikiwa graduate wa chuo kikuu) na posho ya kujikimu njiani.

Sina uhakika kwa sasa mambo yakoje au circulars/waraka husika wa serikali unasemaje kuhusu stahiki hizo. Japo hata huo wakati wetu kuna watu walikuwa wanapunjwa na kupewa posho ya kujikimu pungufu kwa kisingizio kuwa hakuna pesa, wakati Serikali huwa inafanya maandalizi kama ya kuruhusu ajira (maandalizi hayo ni pamoja na kuandaa posho zao). Karibuni.
 
Kuhusu wajibu wa watumishi wa umma, kila mwajiriwa aliweke hilo akilini toka siku ya kwanza kuwa mwajiri anategemea TIJA toka kwa mwajiriwa mpya. Watanzania wengi huwa na mawazo ya kutafuta kazi ili tu kupata mshahara utakaokidhi haja yake. Hawakumbuki kuwa mwajiri alikuajiri si kwa ajili ya kukupa mshahara bali kwa ajili ya kusaidia kutekeleza majukumu yatakayoiwezesha taasisi iliyokuajiri kufikia malengo yake. Hakikisha unakuwa mbunifu na mchapa kazi hodari ili kumwezesha mwajiri wako kufikia malengo yake aliyojiwekea!! Kila siku jiulize je utendaji wangu huu utamwezesha mwajiri kufikia malengo yake?? KWA HIYO NI LAZIMA UYAFAHAMU MALENGO NA MATARAJIO YA MWAJIRI WAKO KUTOKA KWAKE. UJIWEKEE VIGEZO VYA KUJIPIMA. Jielimishe zaidi ili kuongeza tija. Vinginevyo utajikuta unafikiri mwajiri wako ni mkorofi!!
 
Sasa kuandika hivyo kuna kosa gani boss.
Jiulize kuna tija ipi kwa msomaji anayefuatilia uzi huu kwa kusoma ulichoandika? Watu wengi huenda makazini kutimiza wajibu tu wa kuhudhuria kazini lakini hawako makini kujiuliza kama wanachokifanya kwa namnna wanavyofanya kazi kama kuna tija yoyote itakayosaidia taasisi iliyowaajiri kufikia malengo yake!!
 
Team work ni ya muhimu sana katika kuleta tija mahali pa kazi!! Usifiche ujuzi na uzoefu wako kwa wengine. Ushauri kwa waajiriwa wapya: Unaweza ukapewa nafasi kubwa zaidi kuliko baadhi ya watumishi uliowakuta aidha kwa sababu una elimu kubwa zaidi yao. Lakini kumbuka kuwa hao wanaijua zaidi taasisi iliyokuajiri kuliko wewe! pia wana uzoefu wa kazi kuliko wewe! Hao waheshimu sana na waweke karibu na wewe watakusaidia sana!! Usione aibu kuwauliza vitu ambavyo huvijui na wao wanavijua kwa mujibu wa uzoefu wao. Na kila wanapokupa ushirikiano washukuru kwa moyo wote!!
 
Kwa kawaida Serikali huwa imejipanga vizuri sana inapokuwa imetoa kibali cha ajira kwenye utumishi wa umma kuhusu haki na stahiki za waajiliwa wapya. Lakini huwa kuna tatizo kubwa kwa watendaji watekelezaji wa adhima hiyo ya serikali hasa kuhusu eneo la haki na stahiki za waajiriwa wapya.

Mara nyingi watendaji hao hujikita katika kusisitiza wajibu tu wa waajiriwa hawa wapya bila kuwaelimisha pia kuhusa haki na stahiki zao kama waajiriwa wapya kwenye utumishi wa umma.

Ni kwa nadra sana utakuta maafisa utumishi wakiwaelekeza waajiriwa wapya kuhusu haki zao kama vile posho ya kujikimu kwa idadi ya siku zilizobainishwa kwenye miongozo ya serikali, haki ya kupewa fedha kwa ajili ya kusafirisha mizigo kwenye ajira (maana serikali inajuwa kuwa mtu aliyehama toka kwao alikokuwa anaishi na kuhamia kituo chake cha kazi lazima atakuwa na mizigo kama kitanda, nk).

Naomba tuutumie uzi huu:
1. Kuelimishana kuhusu haki na stahiki za waajiriwa wapya kwenye utumishi wa umma.
2. Kuelimishana kuhusu wajibu wa watumishi wa umma.
3. Kupashana uzoefu jinsi wanavyofanyiwa waajiriwa wapya hasa kushusiana na haki na stahiki zao.

Wenye utaalamu na uelewa katika mambo haya tafadhali karibuni sana hapa tujuzane!! Mimi wakati wangu wakati naajiriwa kwa mara ya kwanza (kwa sasa ni msaafu).

Nililipwa posho ya kujikimu siku 14, nililipiwa gharama ya kusafirisha mizigo (personal effects) tani moja na nusu (1,500kg), kwa parcel rate. Nililipiwa nauli first class (nikiwa graduate wa chuo kikuu) na posho ya kujikimu njiani.

Sina uhakika kwa sasa mambo yakoje au circulars/waraka husika wa serikali unasemaje kuhusu stahiki hizo. Japo hata huo wakati wetu kuna watu walikuwa wanapunjwa na kupewa posho ya kujikimu pungufu kwa kisingizio kuwa hakuna pesa, wakati Serikali huwa inafanya maandalizi kama ya kuruhusu ajira (maandalizi hayo ni pamoja na kuandaa posho zao). Karibuni.
Umeandika vizuri sana.
Taasisi nyingi wakuu wake wanataka mjue wajibu wenu ila hawataki mjue haki zenu.

Ngoja nikupe mfano katika mfumo wa swali,hivi mkuu wa Chuo akisimama na kusema anashangaa wafanyakazi wanaandika madai ya overtime na extra duties yuko sawa?,

Hii ipo sana vyuo hasa vikuu,hasa Sua kwenye haki za wafanyakazi hawajali kabisa,bila aibu kiongozi wa chuo anasema maneno hayo kwa wafanyakazi walio chini yake.
 
Kuna halmashauri moja kati ya halmashauri pendwa sana za awamu iliyopita hawapendi kutoa stahiki za watumishi wao na wangetamani hata mtumishi asijue kabisa haki zake. Watumishi hasa katika idara ya utawala wanakiona cha moto sana. Ukihoji stahiki zako ni kama vile unafanya uhaini! Kuna maafisa utumishi ni mashetani walio katika sura ya mwanadamu.

Nina jamaa yangu kule utadhani anafanya kazi jehanamu kwa shetani, vilio kila kukicha na akiambiwa kuhama analeta kigugumizi.
 
Ongezea na SUA,kile chuo bana viongozi wake wajitafakari
 
Cha msingi kwenye uzi huu kama kuna mtu anayeweza kutuwekea hapa Standing order inayofanya kazi kwa sasa atakuwa amefanya vizuri sana! Kwa kawaida madai ya stahiki huwa hayadaiwi kwa mdomo bali kwa barua na usisitize maafisa utumishi na wao wakujibu kwa barua!! Unapoomba stahiki yako ni vizuri ukanukuu namba ya waraka wa serikali / Standing order!! Hapo unakuwa umewashika pabaya!!
 
Unatakiwa kujua utumishi wa umma, chini ya Halmashauri ni kazi ya KUJITOLEA.

- Pesa utakayolipwa, utaitumia kufanya kazi za serikali

- Kimshahara hicho hicho kidogo unacholipwa kinawindwa na kila mtu, kuanzia serikali, makampuni ya kukopeshana, bank, makampuni ya Bima ya mchongo, Michango ya mwenge n.k

- Utapanga nyumba ( serikali haina nyumba za watumishi)

- Utatumia pesa zako kununua bando, kusafiri na Kufanya kazi za serikali.

- UTATUMIKA sana, ila siku ukikataa utageuka adui.
 
Vijana ambao tayari mmeajiriwa ndani ya mwaka mmoja uliopita tupeni uzoefu wenu jinsi mlivyopokelewa na stahiki ambazo mlipewa. Je mlipewa posho ya kujikimu kwa siku ngapi na ilichukua muda upi hadi kulipwa posho hiyo? Je kuna aliyefanikiwa kupewa pesa ya mizigo?
 
Naamini humu jamvini wamo maafisa utumishi kibao. Karibuni mtoe elimu ya stahiki na wajibu wa waajiriwa wapya.
 
Kuna maafisa utumishi wengine usiombe!! bUtafikiri pesa anayolulipa anaitoa mfukoni mwake wakati kuna bajeti kabisa kwa ajili ya waajiriwa wapya. Jamani acheni nyongo!!
 
Sijui lolote kuhusu ajira maana sikuona future kwenye ajira hasa ya serikali. Lakini naona wazi ajira hasa ya serikali inamtumia mfanyakazi kwelikweli yaani wanataka ufanye kazi kwelilikweli. Hawaangalii muda unaotumia kufanya kazi bali kiasi cha kazi unachofanya kwa muda uliopewa.
 
Government Standing Orders inayotumika hadi sasa ni ile ya mwaka 2009. Kinachobadilika mara kwa mara ni kiwango cha subsistance allowance/posho ya kujikimu lakini utaratibu na idadi ya siku anazostahili kulipwa mwajiriwa kwa mara ya kwanza zimebaki kuwa siku 14. Hii ni kwa mujibu wa standing order section L.6.

L.6 Subsistence Allowance on arrival on first appointment:
A public servant on arrival on first appointment within Tanzania shall be paid subsistence allowance on the journey from his home or place of engagement to his duty station; and for the first 14 days at his duty station.

Hii iko wazi kabisa! Lakini utakuta kuna maafisa utumishi wengine wanakuambia jaza siku tatu tu maana hakuna fedha, au anakuambia hata mimi nililipwa siku tatu tu. Cha msingi hapa mwajiriwa mpya hahitaji kujadiliana na afisa utumishi ila anahitaji kuandika barua tu ya kuomba hiyo posho ya kujikimu kwa siku 14 halafu unaikabidhi barua masjala ianze kutembea hadi kwa mtendaji mkuu wa ofisi. WAkikujibu kwa mdomo tofauti na malipo ya siku 14 unawaambia wakujibu kwa maandishi. Hapo hawatothubutu kukujibun kwa maandishi kama walipanga kukupunja, vinginevyo watakuwa hawajitaki!!
 
Lakini pia kuna stahiki ya mizigo unaporipoti kwenye ajira kwa mara ya kwanza. unapaswa kulipiwa kati ya tani moja na nusu hadi tani tano kutegemea na ngazi ya mshahara wako uliopangiwa!
 
Kiwango cha posho ya kujikimu kilipanda kuanzia July 2022. Kiwango cha chini ambacho kicho waajiriwa wengi huangukia kilipanda toka sh 80,000/= hadi sh 100,000/=. Kwa hiyo stahiki ya mwajiriwa ni kupewa posho ya kujikimu kwa siku 14 kwa kiwango cha sh 100,000/= hivyo jumla ya posho ya kujikimu ni sh 1,400,000/==. Hii haipaswi kuwa na mjadala na inapaswa ilipwe fasta mara baada ya mwajiriwa kupewa barua ya ajira na kujaza mkataba wake wa kazi!!

Dkt. Ndumbaro amesema kutokana na kibali hicho cha Mhe. Rais, posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma kwa kiwango cha juu imepanda kutoka shilingi 120,000/= hadi 250,000/= na kiwango cha chini kutoka shilingi 80,000 hadi 100,000/=.

Sitaki nizungumzie sana stahiki ya mizigo kwa ajira ya kwanza, hapa naona maafisa utumishi watanuna sana!!
 
Back
Top Bottom