Tuwaelimishe vijana wanaoajiriwa sasa kwenye Utumishi wa Umma kuhusu haki na wajibu wao!

Nashauri mwajiriwa yeyote wa mara ya kwanza akilipwa posho ya kujikimu pungufu ya siku 14 na kwa kiwango pungufu ya sh 100,000/= kwa siku, tupia hapa wadau wataona jinsi ya kukushauri ili ulipwe stahiki yako!! Kumbuka wapo watumishi wa umma ambao kazi yao ni kuona tiu kuwa hakuna mwajiri au boss anayejifanya mungu mtu kuonea watu!!
 
Kutokana na teknolojia kukua utazijua nyingi hata ambazo waajili walitaka wakufiche usizijue.
 
Mkuu katika mchakato wa menejimenti ya rasilimali watu kuna kitu kinaitwa "orientation stage" na hii ni wakati mfanyakazi mpya katika ajira anapokasimiwa majukumu yake ya kazi kwa mara ya kwanza. Hapa huonyeshwa na wazoefu kuhusu mazingira yake halisi ya kazi kwa vitendo.

Tatizo huanzia kwa wale ambao humuelekeza afanye nini. Endapo hawatamsisitizia kuhusu masuala muhimu ya kuzingatia, mathalani uadilifu, utii wa maadili mema,, uwajibikaji n.k. naye atajikuta akiishi kwa mazoea kama vile ambavyo amewakuta wenyeji wake wakifanya hivyo.
 
Tatizo la wengi huwa ni kwamba kabla hajafanikiwa kupata ajira na hana pesa zimekuwa adimu kwake, mara nyingi hutumia nguvu na muda mwingi sana kupata hata hicho kidogo anachofanikiwa kupata. Tumeshuhudia graduates wengi wakibembeleza kazi hata kwa mshahara wa 200,000/= tu.
Akipata kazi ghafla ataanza kuona mshahara wake ni mdogo sana!! haukidhi kabisa haja na matarajio yake! Hilo huwafanya wasiwe na tija mahali pa kazi. Ushauri: Chapa kazi kwa bidii sana na usitarajie mafanikio ya haraka. Viongozi wako watakuona lakini zaidi sana Mungu atakuona na atakubariki. Mafanikio na kupanda kutakuja tu ukiwa mchapa kazi. Ni kweli miaka ya kuvumilia ni lazima itakuwepo lakini kaza uzi, Mungu ni mwaminifu. Usikubali kabisa njia za mkato kama wizi na ufisadi, huo utakuharibia kabisa maisha yako. Lakini pia jifunze kuweka akiba hata kama ni kidogo!! Kinachoitafutwa hapa ni TABIA ya kujuwekea akiba.
 
Waajiriwa wapya sikieni, kujiwekea akiba ni tabia na siyo kuwa kujiwekea akiba ni kwa sababu ya kipato kikubwa. Tabia hujengwa ili iwe endelevu. Usipojijengea tabia ya kujiwekea akiba wakati una kipato kidogo hutaweza kujiwekea akiba hata kama kipato kitakuwa kikubwa!! Hakikisha kila mwezi unajiwekea akiba hata kama ni sh 5,000/= tu kwa mwezi. Ukifanikiwa hapo utahamasika kujiwekea akiba kubwa kipato kikiongezeka maana tayari ulishajijengea tabia ya kujiwekea akiba!
 
Karibuni wenye uelewa na wazoefu wa mambo ya kazini tuwajenge vizuri waajiriwa wapya kwenye utumishi!!
 
Uaminifu kazini unalipa sana hata kama itachukua muda kuona malipo ya uaminifu wako. Mungu ni mwaminifu lazima utafanikiwa kazini ukiwa mwaminifu, mtiifu na mchapa kazi!! Usijiunge na makundi ya walalamishi!!
 
Mkuu kama una pdf ya Standing Order nitumie.
 
Ukisoma standing order utashangaa sana. Wakubwa hujinufaisha sana kwa kuitumia hii standing order, lakini kwa wengine kwa kiasi kikubwa huwa haitekelezwi. Kwa mfano mwajiriwa wa kwanza ambaye huanzia TGS D anapaswa alipwe pesa ya mizigo tani 5 wakati anaripoti kituoni kwake kwa mara ya kwanza. Mtoto wa mkubwa atafanyiwa hivyo kihalali kabisa lakini kwa wengine haiingii akilini kuwa unaweza kulipwa pesa za mizigo tani tano wakati wa kuajiriwa. Japo wakati wa kustaafu huwa wanalipwa.
 
Haya ndiyo masaibu na matatizo wanayokutana waajiriwa wapya: Mtu anapewa barua ya uthibitisho kutoka sekretarieti ya ajira kuwa amefaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi. Barua inamtaka aripoti kwa mwajiri wake ndani ya siku 14 toka kupokea barua hiyo. Hii inatoa picha kuwa mwajiriwa akisharipoti kwa mwajiri wake basi tangu hapo atakuwa mikononi mwa mwajiri huyo. Lakini nhaiko hivyo!!!

Niwape mfano hai: Mwajiriwa mpya anasafiri toka Dar hadi dodoma kufuata barua yake ya kupangiwa kituo. Amepangiwa kuripoti Halmashauri mojawapo ya mkoa wa Tabora. Kijana fasta akaenda kuripoti. Alipofika huko akapokelewa na kuonesha vyeti vyake original na kuambiwa " Subiri tutakapokuwa tumejiridhisha na usahihi wa vyeti vyako tutakupigia simu ili uje upewe sasa barua ya ajira"!! Hakurudishiwa nauli aliyotumia kusafiri toka Dar hadi Tabora, hakupewa pesa yoyote ya kumsaidia kujikimu maana bado hajaajiriwa rasmi kwa maana ya kupewa barua ya ajira! Kwa kuwa kijana hana namna ya kuishi tabora wakati anasubiria kupigiwa simu ili kuitwa kazini na mwajiri wake, akalazimika arudi tena nyumbani Dar!! Hao ndio miungu watu wanavyosumbua waajiriwa wapya!

Sasa najiuliza, wakati wa usaili aliwasilisha vyeti vyake halisi vikahakikiwa tena mara mbili maana usaili upo mara mbili! Kwa kuchaguliwa kwake maana yake sekretarieti ya ajira imejiridhisha na vipengele vyote ikiwemo uhalali wa vyeti vyake! Kwa nini usumbufu wote huo!! Kwa nini mwajiri asigharimie malazi na chakula cha huyu mwajiriwa mpya wakati wanafanya mchakato wa kujiridhisha maana ni wao walimwita tena kwa kitisho cha kuripoti ndani ya siku 14 vinginevyo atapoteza nafasi yake!!

Kuna mwingine ameripoti hivi majuzi kwenye manispaa mojawapo ya jiji la Dar es salaam. Naye amerudishwa nyumbani asubiri kuitwa tena kwa simu na hakupewa pesa yoyote! Je huo ndio utaratibu uliokubalika rasmi?
 
Duhhh! Mimi mwaka wa 6 huu sijalipwa hata mia. Nilidai hadi nikachoka
 
Kuna maafisa utumishi wengine usiombe!! bUtafikiri pesa anayolulipa anaitoa mfukoni mwake wakati kuna bajeti kabisa kwa ajili ya waajiriwa wapya. Jamani acheni nyongo!!
Kuna watu wana roho mbaya ajabu!
 
Wadau naomba msahada Kwa hili jamani,sisi tumepewa laki tatu tu ela ya kujikimu,tumeripoti kazini Mwezi wa 01/09/2023.leo ndo tumelipwa Tena laki tatu jamani ndugu zangu tusaidie I kama Utumishi upo ivi ,hali hii siyo nzuri Kwa waajiriwa, hapa bariadi dc ndo ela tuliopokea Leo,Kwa Mwenye kutusemea juu ,maana hatuna hata namba za viongozi tusaidieni.tumesaini milioni alafu unapewa laki tatu kweli inauma Tena sana.naomba msahada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…