Celebrities matajiri kwa ngazi za mikoa.
Ni kweli asilimia kubwa ya Matajiri wapo Dsm lakini nako mikoani sio kwa kuwachukulia poa, uzi huu unawahusu wenye mawe yao huko mikoani.
Wahindi na waarabu tuwaweke pembeni kidogo ni ligi za kimataifa, iwe ligi yetu ya watanzania wa asili.
Kwa uchache naowajua ni hawa ila tuzidi kujuzana kupitia comments
SONGEA -
Super Feo - Biashara yake ni ya mabasi, Kakamata route nyingi za Songea na Njombe.
MBEYA -
Achimwene - Biashara yake ni mabasi, anazidi kuleta mafuriko ya mabasi kila baada ya miezi kadhaa
Sugu - Mwana aliezeeka sio wa kumchukulia poa, nae kimtindo yumo yumo katika madon maaraufu wa Mbeya
MANYARA
Laizer - huyu mzee alipiga mshindo mzito sana na kujipatia umaarufu kupitia madini ya Tanzanite