Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Hahahaha umenikumbusha enzi za best angu Amos Makalla enzi hizo mweka hazina wa CCM!!

Makalla ana bahati ya kuzaliwa niishie hapo!!
Tofauti na watu wa kuja wanaomuona Makalla kama mtu wa kuja ,Makalla ni mtoto wa mujini kwelikweli namlinganisha tu na akina Borntown, mtu ukitamba vitongoji vya Mwanayamala basi wewe kidume. Kama wewe ni kijana wa jiji mpenda strehe wa miaka ile na humjui Makalla basi utakuwa ulikuwa unakuja jijini likizo na kufikia kwa kaka au mjomba
 
Kasema wapi? Jiulize kama huyo Hidaya alikuwa Arusha why kwenye wimbo amtafute iwapo alimuona Moro au Arusha, au Mwanza. Ilitengenezwa tu na wabongo.
tulisema huu uzi sio wa watoto wa 2000 tueleweke

KABASELE YAMPANYA aliahidi kuitungia NYIMBO YANGA akirudi CONGO
sasa kipindi anazungumza hayo maneno wewe ulikuwa na miaka mingapi
 
Young millionaire alikua DJ mzuri sana pale Kinondoni kwenye ukumbi wa Lang'ata social hall akisaidizana na Chriss Phabby,

Kama ni huyo ndio kaongelewa hapo.
Sio huyo Young Milionea DJ Lusungu yupo Mwanza miaka mingi kuna wakati alikuwa na studio ya kuuza kanda ,alwatani pale Mwanza,huyu Young Milionea mwingine ni Nshomile Muzamir Katunzi, alikuwa na kaka zake wawili mapacha wa kufanana na mmoja kesha tangulia mbele za haki,hawa mapacha walipata pesa nyingi sana miaka ile kupitia mambo ya kutoa mizigo bandarini, wao walikuwa kama GSM ta miaka ile.
 
Haswaa umemqliza... nimekumbuka enzi za silentinn kwa Rwega...

Siku hizi tusioijua kidimbwi tunaambiwa wa kuja 😂😂
 
Mdogo wao mapacha kato na Kakuru ila huyu ni wa Juzi tu
Hao mapacha mmoja alishafariki na walikuwa na pesa kwelikweli,huyu mdogo wao alikuwa mjinga mjinga tu lakini nae akaja kuwa mjanja akapata pesa nyingi za utapeli, kwa siku hizi sijui kaishia wapi, matapeli wengi walisjamili enzi za Born town,lakini alipoingia Jiwe wengi wao waliishia lupango ma dili za bandarini au madini zikaisha
 
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Papa Msofe alikuwa hachezi mbali ile mitaa wa iliyokuwa Salamander na benki ya Posta na alikuwa napenda kuvaa mashati meupe nadhifu sana na alikuwa na demu wake Benki ya Posta pale karibu na Posta ya zamani nasikia mwishowe alimuo yule mdada
 
Dj omyyyy mutoto wa mujiniiii mutoto wa mujini, Fikiri madinda mutoto wa mujiniii mutoto wa mujini...........
 
Umenikumbusha Haji Mbabe alitusumbuwa sana Sinza enzi hizo
Haji Mbabe mrundi alianzisha bendi yake chini ya gwiji Zahir Ally na haiukudumu alikuwa na kigari amazing ,bandarini kulimtajirisha akaenda Uingereza akajifanya mkimbizi alikuwa na kiofisi chake cha kutoa mizigo bandarini pale kariakoo kwenye nyumba ya mke wa marehemu Mbaraka Mwinshehe, alirudi tena Bongo baada ya kushindwa kubeba box Uingereza .
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna pedeshee Ndunguru na pedeshee Ndomba wa Makongo. Nteze wa Nteze mzee wa kifusi.... dah old good days. Kuna siku niko pale makumbusho, Papaa Msofe akanunua bia kwa kila mtu aliyekuwepo mle ndani nilichoka sana, anakujua hakujui unapewa bia 😅
 
Hidaya alikuwa ni mkaazi wa Arusha tena pale mjini karibu kabisa na Sheikh Amri stadium kwa nyuma ,mitaa ile kuna baa nyingi,nadhani allikuwa na kamadamu ya kisomali kwa mbali bonge la pisi amepanda juu na bonge la guu halafu mtoto wa mjini, udongo huu umechukua wengi zamani kulikuwa na pisi kali kwelikweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…