Yap! Ningetamani kumjua huyo uncle SaleheNa TX Moshi William
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yap! Ningetamani kumjua huyo uncle SaleheNa TX Moshi William
Tofauti na watu wa kuja wanaomuona Makalla kama mtu wa kuja ,Makalla ni mtoto wa mujini kwelikweli namlinganisha tu na akina Borntown, mtu ukitamba vitongoji vya Mwanayamala basi wewe kidume. Kama wewe ni kijana wa jiji mpenda strehe wa miaka ile na humjui Makalla basi utakuwa ulikuwa unakuja jijini likizo na kufikia kwa kaka au mjombaHahahaha umenikumbusha enzi za best angu Amos Makalla enzi hizo mweka hazina wa CCM!!
Makalla ana bahati ya kuzaliwa niishie hapo!!
tulisema huu uzi sio wa watoto wa 2000 tuelewekeKasema wapi? Jiulize kama huyo Hidaya alikuwa Arusha why kwenye wimbo amtafute iwapo alimuona Moro au Arusha, au Mwanza. Ilitengenezwa tu na wabongo.
Sio huyo Young Milionea DJ Lusungu yupo Mwanza miaka mingi kuna wakati alikuwa na studio ya kuuza kanda ,alwatani pale Mwanza,huyu Young Milionea mwingine ni Nshomile Muzamir Katunzi, alikuwa na kaka zake wawili mapacha wa kufanana na mmoja kesha tangulia mbele za haki,hawa mapacha walipata pesa nyingi sana miaka ile kupitia mambo ya kutoa mizigo bandarini, wao walikuwa kama GSM ta miaka ile.Young millionaire alikua DJ mzuri sana pale Kinondoni kwenye ukumbi wa Lang'ata social hall akisaidizana na Chriss Phabby,
Kama ni huyo ndio kaongelewa hapo.
Mrehemu Abbu Semhando mpiga drums maarufu na machachari wa Twanga pepeta na pia Orch MatimilaBaba Diana alikua akitajwa sana na Twanga Pepeta.
Abbu Semhando mpiga drums wa Twanga,kabla alikuwa Matimila na alikuwa na mdogo wake nae akipiga bass Vijana jazz kama sijakoseaHuyu alikua sio pedeshee alikua muimbaji wa bendi nafikiri
Makalla sio kijana aisee.Bado kijana sana ila noti zilimtembelea haraka. Salome alikuwa nyodo sana pia
Haswaa umemqliza... nimekumbuka enzi za silentinn kwa Rwega...Tofauti na watu wa kuja wanaomuona Makalla kama mtu wa kuja ,Makalla ni mtoto wa mujini kwelikweli namlinganisha tu na akina Borntown, mtu ukitamba vitongoji vya Mwanayamala basi wewe kidume. Kama wewe ni kijana wa jiji mpenda strehe wa miaka ile na humjui Makalla basi utakuwa ulikuwa unakuja jijini likizo na kufikia kwa kaka au mjomba
Hao mapacha mmoja alishafariki na walikuwa na pesa kwelikweli,huyu mdogo wao alikuwa mjinga mjinga tu lakini nae akaja kuwa mjanja akapata pesa nyingi za utapeli, kwa siku hizi sijui kaishia wapi, matapeli wengi walisjamili enzi za Born town,lakini alipoingia Jiwe wengi wao waliishia lupango ma dili za bandarini au madini zikaishaMdogo wao mapacha kato na Kakuru ila huyu ni wa Juzi tu
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]mziki wa dansi ulikuwa na mambo matatu
kwanza kulikuwa na mapedeshee hawa watuzaji
ndio hao aliowataja mtoa mada
halafu kulikuwa na mashabiki damu
kama hapo unemtaja
MAMA MINGOI CHESCO MAZEE WA MATUNDA kuna pia Kina MANKA MUSHI
ambao ndo waliikuwa navijiwe vyao au CAMP zao
karanga camp
HOME ALONE
VINGUNGUTI TIMBERLAND
DALADALA CAMP
SWAZI INTER
n CAMP nyingine nyingi sana
ambazo hizo CAMP zina mashabiki haswa na mapedeshee wajanjawajanja ndo zilikiwa maskani zao na watoto wa mjini na wakati mwingine hata wanamuziki wenyewe pia huweka vijiwe katika hizo CAMP
hizo CAMP kulikuwa na mashabiki WAZARENDO
nakumbuka kuna SHABIKI MMOJA wa VINGUNGUTI TIMBERLAND huyo Mdau alikuwa anaipenda sana TWANGA kiasi alikuwa mpk anapanda NDEGE kuifuata TWANGA ikiwa NJE ya MKOA haswa ARUSHA au MWANZA
halafu kundi Jingine sasa ni la wanaofanikisha BENDI kuwa na Mziki bora
mfano HUSSEIN MIUNDOMBINU
huyu alikuwa fundi mitambo(umeme)
Twanga popote itakapopiga huyu alikuwa anahakikisha mambo yote ya umeme yako sawa mziki unatoka vizuri
THABITI MTOTO ILALA huyu alikuwa mkali wa kucheza na Keyboad
lakini pia kulikuwa na mkali mwingine wa KEYBOAD
ukisikia PROFESHENARI TARIBONARI VIctor mkambi huyu mkali wa KEYBOAD hata kama akifa inapaswa TWANGA wamjengee Sanamu lake maana alikuwa PROFESHENO haswa kaipaisha sana twanaga na UFUNDI wake wa KEYBOAD
Ukisikia MCD basi hapo anatajwa SUDI MOHAMED TIMBO(marehemu)
huyu alikuwa mpiga tumba matata sana
halafu ukisikia SHAKASHAKA SHAKUZURU hapa alikuwa anapaishwa MIRAJI SHAKASHIA huyu ni mpiga gitaa matata sana
halafu kulikuwa kulikuwa na mkung'uta DRUM hatari sana BABA DIANA BABAA SHARIFA BABAA ZAITUNI basi alikuuwa anatwaja ABUU SEMHANDO mpiga DRUM hatari
sasa utakuj kugundua kulikuwa na makundi matatu yalikuwa yanatwaja sana kwenye nyimbo
wngine walikuwa mashabiki damu wengine ndi hao watu wa wanamuziki wenyewe
sijui kwanini huwa napenda sana stori za kitambo.za wajanja wa zamani na vituko vyao.Wakati Mustahiki Meya wa Jiji Allan Mulumba Kashama anatuchezesha Dar es salaam kibinda nkoyi ndani ya Silent in Mwenge ulikuwa darasa la ngapi?
Unamjuwa Joseph Rwegasira?
Papa Msofe alikuwa hachezi mbali ile mitaa wa iliyokuwa Salamander na benki ya Posta na alikuwa napenda kuvaa mashati meupe nadhifu sana na alikuwa na demu wake Benki ya Posta pale karibu na Posta ya zamani nasikia mwishowe alimuo yule mdadaumenikumbusha late 90s nimemaliza O-Level, nipo home idol nasubiri majibu yatoke. mshua akanitafutia temporary job mitaa ya mjini posta kwenye ofisi ya rafiki yake.
ofisi ilikuwa mtaa wa jamhuri jirani na ile round about ambayo inakutanisha india street na mkwepu street, almaarufu mitaa ya azam take away.
ilikuwa kila ikifika mida ya saa tatu mpaka saa nne asubuhi, lile eneo walikuwa wanatokea mabroo smart kwelikweli kimuonekano. mkononi wamebeba vi-diary.
walikuwa wanavaa mashati nadhifu, surauli za kadeti na viatu safi vya ngozi. kwa ujumla walikuwa wanapendeza sana, mimi mwenyewe nilikuwa nawa admire.
siku moja nikamuuliza broo mmoja ambaye tulikuwa tunafanya kazi pale, kwamba hawa jamaa ni akina nani,mbona mda mwingi wanautumia kakaa kwenye vijiwe vya shoe shiners, hawana kazi ya kufanya?.
akanijibu ukisikia mission town ndio hao, na hapo kwenye vijiwe vya shoeshiners ndio sehemu zao za kupanga mipango na kupeana deals mbalimbali.
akaniambia kile kipande chote cha mtaa wa mkwepu kinachokatiza club ya billicanas mpaka kule kwenye maungio ya samora avenue, ni territory ya ma-mission town.
hata papaa msofe alianza kujifunzia upigaji mitaa hiyo.
Hidaya alifariki nafikir mwaka jana mwanzoni.Ilikua mama moja pisi kali ya Arusha, pepe kalee alifichwa hadi akanyoosha mikono, nadhani bado yupo alikua na mtoto mmoja wa kike aliuliwa na mume wake walikua wakiishi UK
Haji Mbabe mrundi alianzisha bendi yake chini ya gwiji Zahir Ally na haiukudumu alikuwa na kigari amazing ,bandarini kulimtajirisha akaenda Uingereza akajifanya mkimbizi alikuwa na kiofisi chake cha kutoa mizigo bandarini pale kariakoo kwenye nyumba ya mke wa marehemu Mbaraka Mwinshehe, alirudi tena Bongo baada ya kushindwa kubeba box Uingereza .Umenikumbusha Haji Mbabe alitusumbuwa sana Sinza enzi hizo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mtawali-Yadi yake ya Magari inatazamana na Ostabay Police- alikuwa matata kwa totoz! Ila aliwai kutwa na skendo ya kufumaniwa na mke wa jamaa mmoja hivi ambae nae alikuwa mtoto wa Mujini .Ilimfanya siku moja anunue magazeti yote yaliokuwa na hii storyNchi nzima?? Ilikuwaje?? Siku nyingine[emoji23]
Hidaya alikuwa ni mkaazi wa Arusha tena pale mjini karibu kabisa na Sheikh Amri stadium kwa nyuma ,mitaa ile kuna baa nyingi,nadhani allikuwa na kamadamu ya kisomali kwa mbali bonge la pisi amepanda juu na bonge la guu halafu mtoto wa mjini, udongo huu umechukua wengi zamani kulikuwa na pisi kali kwelikweli.Acha ubishi mzee mwenyeji wa Arusha wote hakuna asie mjua Hidaya tena alikua maarufu kwa jina la Hidaya Wa pepe kale kafariki mwaka jana , Hidaya ni miongon mwa wanawake matajiri wa Arusha enzi hizo, ameishi pia france ninavyo kueleza kafariki mwaka jana elewa hivyo
Alafu mi nazungumzia wimbo wa pepe kale Hidaya hiyo ya kwako ya Hedaya mimi siijui