Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Hahaha naona bado mtambo Ana office yake pale nyuma ya tomato kino
Aise,umenikumbusha jamaa ashanifanyia kazi 1,2 ,3 sema hanaga longolongo kwenye hela alikuwa
Alafu mkimyaaa, mtaratibuuu

Ova
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Umenikumbusha kwenye nyimbo nyingi za marehemu Madilu System, amemtaja sana Pedeshee Emmanule Sammuele.... Mpaka Kuna wimbo nadhani unaitwa hivyo... Naupenda sana wimbo huu.....
Nipo naisikiliza nyimbo hiyo, madilu kaua sana humo
 
Ni mtoto wa nje wa Kapuya
 
"tendaaa wemaaa uusingoje shukrani sema na watu wotee"[emoji445][emoji444]"",,Muzamiriii Katunziii,,,"[emoji444]
"bibi yangu alinambia chekaaa na watu,,,uvae viatu heee[emoji445].
,,wekaa bastola chini,,bastola chini.bastola chini hee[emoji344]

Muzamiri Katunzi ya mfalme wa masauti Christian Bella a.k.a Obamaaaa[emoji350]
 
Mshua Rais,mtoto Makamu wa Rais! Nchi hatari sana hiyo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Nyimbo inaitwa candidate na biso Mobutu, maana yake mgombea watu ni Mobutu
 
Hatari sana, sasa hivi hawana kitu hao wote...

Tumebakia sisi tu...

Kino star na sinza star tumebaki wachache Mrangi asharudisha mpira kwa kipa yuko madale john baptist kajificha kihesa mjini wanakwambia kuna kelele sana bora akae anapofuga hata vikuku vya kienyeji ajilie supu. Basi wakiowaona watoto wanaojifanya kutamba na muda wanasonya wanajiuliza hawa vijana wangejua
 
Nilisikia huyu mwamba mali zake zimekamatwa na serikali ya Marekani pamoja na Ufaransa na pia ni kama yupo kizuizini huko Ufaransa,huyu mwamba ndiye amasemekana alinunua ile glove maarufu yenye vimulimuli vya dhahabu aliyokuwa anaivaa Wacko Jacko.
 
Nimekulia Sinza ile ya akina Remi ndio wanatamba na Volkswagen imeandikwa.''mambo kwa soksi'' tulikuwa tunajua karibu vijana wote, hivi sasa Sinza imebadirika ni Sinza ya magorofa,mahoteli,vijana wote wa zamani ama wamerudisha namba kwa Sir God ama wamehamia sehemu nyingine nje ya mji,nyumba nyingi tulizokuwa tunapanga chumba kimoja kimoja zimebomolewa na kujengwa mahekalu, nakumbuka pale sinza madukani kulikuwa na mbabe wa kikurya Lucky baba yake alikuwa usalama wa Taifa,namkubuka bibi Uliye alikuwa na mabinti kama 10 hatari sana, nakumbuka akina Banza stone wakiwa wadogo wakicheza disco mtaani, nakumbuka Vatican City ikiwa hotel kumbwa Sinza na Simba walikuwa wakiweka kambi hapo, namkumbuka Fred Mwalasha akiwa ametoka Ulaya na mke wa kizungu ikawa yeye ni bangi na bangi na yeye hadi mwanamke wa kizungu akamkimbia, siku hizi sinza yamejaa madangulo na wazee wale waliokuwa na nyumba ambazo tulikuwa tumepanga nao hatunao duniani ila zile nyumba walizoacha watoto wao wameziuza kwa matajiri na kwenda kunywea pombe na kula sembe. Sinza ya sasa si ile tuliyokuwa tunaitimba, ama kweli siku hazigandi.
 
Nasikia hata Mpaka reli alikuwa mwizi wa funguo akiwa hotelini utamuona wa maana kumbe ana yake na yale mambo ya gereji nasikia ilikuwa kisingizio tu
 

Siku hizi madukani hadi whiteinn watu wanapanda bodaboda ujue, kweli wewe sinza star, hapo nilitania tu wengi walioshtuka mapema wako zao madale, kibaha hadi kongowe kuna wana wa kino walienda kujiweka huko na maisha yanasonga, vatican, kijiweni, kwa remi duuu siku zinakimbia acha tutulie tu hatuna namna vunja mfupa meno bado iko ndio hivo
 
josee maina, dr Said Mabera, juliana Augustino na haruna furgerson( sijui kama nimeliandika kwa usahihi) yalikuwa yakitajwa sana na msondo ngoma jazz band
 
Nilisikia huyu mwamba mali zake zimekamatwa na serikali ya Marekani pamoja na Ufaransa na pia ni kama yupo kizuizini huko Ufaransa,huyu mwamba ndiye amasemekana alinunua ile glove maarufu yenye vimulimuli vya dhahabu aliyokuwa anaivaa Wacko Jacko.
ni kweli, baadhi ya property zake huko europe zilikuwa seazed na baadhi zimeshapigwa mnada, hususani gari zake za kifahari.

ila haijaweza kumfilisi, bado ana fedha nyingi sana. ni mtu wa showoff, kila mara huwa anatupia picha au video kwenye page zake kuonyesha namna anavyokula bata nchi mbalimbali kwenye exotic beaches and five star hotels.eneo analolipenda sana ni visiwa vya carribbean.

kumbuka jamaa ni makamu rais wa equatorial guinea, lakini mda anao spend nje ya nchi kula bata ni mwingi kuliko mda anaotumia kubaki nchini kwake kuwahudumia wananchi.
View attachment 2279959
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…