Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Fomu za kuomba viza kina Mtambo si ndio dili yao kuwajazia watu?
Kuna vitu vingine ni ipuuzi mtupu, mimo nilikuwa na Boss wangu mzungu alikuwa hakai Tanzania zaidi ya wiki mbili, kwahiyo kiswahili chake ni Jambo jambo na kuibia maneno machache, lakini baada ya baba yake kuwa mtu mzima sana alimpa kuw Rais wa makampuni yao cheo ambacho kitamlazimu awe anakaa Tanzania muda mwingi hivyo akaniomba nimtamfutie mwalimu wa kiswahili alikuwa anatenga mud ofisini anakuja kumfundisha.

My point mtu kuwa na exposure mpaka mamtoni halafu hujui kusoma na kuandika sasa hata vile vikadi airport akujazie nani? driving license amepataje US? au ndio zile za Wanubi? Too good to be true.
Hahaha naona bado mtambo Ana office yake pale nyuma ya tomato kino
Aise,umenikumbusha jamaa ashanifanyia kazi 1,2 ,3 sema hanaga longolongo kwenye hela alikuwa
Alafu mkimyaaa, mtaratibuuu

Ova
 
Huyu alikua mtoto wa kigogo mbunge wa Kisarawe enzi hizo. Mdingi wake licha ya kua Mbunge alishawahi kua kiongozi mkubwa wa bandari ya DSM pale. Na ana mjengo mkali uingereza kuna baadhi ya wanawe wanaishi huko.. Mzee Janguo alikua na ukwasi saaaana..

Iddi Janguo alikua anamiliki limousine nyeusi ilisumbua saaana mjini wakati ule na alikua anaishi ktk jumba la ghorofa kule mitaa ya Jangwani seabreeze la mshua wake.. Alifanya fujo nyingi mjini wkt ule miaka ya 2005 kushuka chini.. Enzi nipo sekondary nilikuaga natamani nikiwa mkubwa niwe japo na nusu ya mkwanja aliokua nao.. Zile zama watoto wa vigogo walituvimbia sana. Naskia siku hizi yupo Kinondoni ametulia hana tena zile pesa kama wkt ule..

Na alikua anang'oa pisi kali sana. Unaukumbuka ule wimbo wa Dudubaya unaitwa Mashaka kuna mstari aliimba, "Warembo wazuri acheni kugombana, sina chaguo kama IDDI JANGUO, lakini kwa leo warembo nyongeni.. Atakaeshinda ntaondoka nae.. Mshike kiuno (uyoo) mlambe unyayo (uyoo) mshike mabega (uyoo) mkalie kwa juu!!!" [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Umenikumbusha kwenye nyimbo nyingi za marehemu Madilu System, amemtaja sana Pedeshee Emmanule Sammuele.... Mpaka Kuna wimbo nadhani unaitwa hivyo... Naupenda sana wimbo huu.....
Nipo naisikiliza nyimbo hiyo, madilu kaua sana humo
 
baraka kapuya alikuwa anatajwa sana na wanamuziki wa kundi la akundo sound.

mmiliki wa akudo alikuwa ni prof. juma kapuya ambaye wakati fulani aliwahi kuwa waziri wa elimu na mbunge.

inawezekana huyu baraka ni family member au mtoto wa mzee kapuya. wajuzi wa mambo watajazia nyama.
Ni mtoto wa nje wa Kapuya
 
"tendaaa wemaaa uusingoje shukrani sema na watu wotee"[emoji445][emoji444]"",,Muzamiriii Katunziii,,,"[emoji444]
"bibi yangu alinambia chekaaa na watu,,,uvae viatu heee[emoji445].
,,wekaa bastola chini,,bastola chini.bastola chini hee[emoji344]

Muzamiri Katunzi ya mfalme wa masauti Christian Bella a.k.a Obamaaaa[emoji350]
 
kuna rhumba moja kali sana ya madilu system inaitwa vice versa.

ktk verse ya kwanza ya track hiyo, madilu anataja jina la Teodoro Obiang Nguema ambaye ni mtoto wa rais wa equatorial guinea, mzee Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

Teodoro au maarufu teddynguema kama anavyofahamika kwenye social media, kwa sasa ni makamu wa rais wa taifa hilo.

maisha anayoishi huyu teddy yanaakisi kwa kiwango kikubwa maisha halisi ya kipedeshee, ana pesa nyingi sana za kula bata.

anasafari maeneo mbalimbali duniani ktk kujipa raha na huwa hafichi kitu, picha zake za kula bata huwa anaziweka kwenye kurasa zake za social media.

baba yake yupo ktk orodha ya marais ambao wapo madarakani kwa mda mrefu duniani. yeye na baba yake wanaitawala equatorial guinea kwa mkono wa chuma kweli kweli.

View attachment 2279163View attachment 2279164View attachment 2279165View attachment 2279168
Mshua Rais,mtoto Makamu wa Rais! Nchi hatari sana hiyo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Franco alikuwa Sungura inasemekana alikuwa na bifu na Rais Mobutu akakimbilia Ufaransa, basi uchaguzi ulipokaribia ndio Franco akatowa hiyo nyimbo ya kumsifu kumpamba na kumuabudu mobutu.

Mobutu baada ya kusikia hiyo nyimbo alimpigia simu Franco na kumuomba arudi nyumbani azunguke naye kwenye kampeni kama Kapteni Komba na CCM.
Baada ya Franco kukubali proposal ya Mobutu basi alitumiwa ndege kubwa Ufaransa kwa heshima yake imrudishe nyumbani Zaire.
Nyimbo inaitwa candidate na biso Mobutu, maana yake mgombea watu ni Mobutu
 
Hatari sana, sasa hivi hawana kitu hao wote...

Tumebakia sisi tu...

Kino star na sinza star tumebaki wachache Mrangi asharudisha mpira kwa kipa yuko madale john baptist kajificha kihesa mjini wanakwambia kuna kelele sana bora akae anapofuga hata vikuku vya kienyeji ajilie supu. Basi wakiowaona watoto wanaojifanya kutamba na muda wanasonya wanajiuliza hawa vijana wangejua
 
kuna rhumba moja kali sana ya madilu system inaitwa vice versa.

ktk verse ya kwanza ya track hiyo, madilu anataja jina la Teodoro Obiang Nguema ambaye ni mtoto wa rais wa equatorial guinea, mzee Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

Teodoro au maarufu teddynguema kama anavyofahamika kwenye social media, kwa sasa ni makamu wa rais wa taifa hilo.

maisha anayoishi huyu teddy yanaakisi kwa kiwango kikubwa maisha halisi ya kipedeshee, ana pesa nyingi sana za kula bata.

anasafari maeneo mbalimbali duniani ktk kujipa raha na huwa hafichi kitu, picha zake za kula bata huwa anaziweka kwenye kurasa zake za social media.

baba yake yupo ktk orodha ya marais ambao wapo madarakani kwa mda mrefu duniani. yeye na baba yake wanaitawala equatorial guinea kwa mkono wa chuma kweli kweli.

View attachment 2279163View attachment 2279164View attachment 2279165View attachment 2279168
Nilisikia huyu mwamba mali zake zimekamatwa na serikali ya Marekani pamoja na Ufaransa na pia ni kama yupo kizuizini huko Ufaransa,huyu mwamba ndiye amasemekana alinunua ile glove maarufu yenye vimulimuli vya dhahabu aliyokuwa anaivaa Wacko Jacko.
 
Kino star na sinza star tumebaki wachache Mrangi asharudisha mpira kwa kipa yuko madale john baptist kajificha kihesa mjini wanakwambia kuna kelele sana bora akae anapofuga hata vikuku vya kienyeji ajilie supu. Basi wakiowaona watoto wanaojifanya kutamba na muda wanasonya wanajiuliza hawa vijana wangejua
Nimekulia Sinza ile ya akina Remi ndio wanatamba na Volkswagen imeandikwa.''mambo kwa soksi'' tulikuwa tunajua karibu vijana wote, hivi sasa Sinza imebadirika ni Sinza ya magorofa,mahoteli,vijana wote wa zamani ama wamerudisha namba kwa Sir God ama wamehamia sehemu nyingine nje ya mji,nyumba nyingi tulizokuwa tunapanga chumba kimoja kimoja zimebomolewa na kujengwa mahekalu, nakumbuka pale sinza madukani kulikuwa na mbabe wa kikurya Lucky baba yake alikuwa usalama wa Taifa,namkubuka bibi Uliye alikuwa na mabinti kama 10 hatari sana, nakumbuka akina Banza stone wakiwa wadogo wakicheza disco mtaani, nakumbuka Vatican City ikiwa hotel kumbwa Sinza na Simba walikuwa wakiweka kambi hapo, namkumbuka Fred Mwalasha akiwa ametoka Ulaya na mke wa kizungu ikawa yeye ni bangi na bangi na yeye hadi mwanamke wa kizungu akamkimbia, siku hizi sinza yamejaa madangulo na wazee wale waliokuwa na nyumba ambazo tulikuwa tumepanga nao hatunao duniani ila zile nyumba walizoacha watoto wao wameziuza kwa matajiri na kwenda kunywea pombe na kula sembe. Sinza ya sasa si ile tuliyokuwa tunaitimba, ama kweli siku hazigandi.
 
Hao wote hamna kitu wote ni watu wa kuongeza 0
Hiuo mwingine sjui nani na m#m
Wote wezi tu wa ufunguo walikuwa
Mtu anaenda dubai utasema anaenda kufunga mzg,kmbe wez wa ufunguo,wanatumia kadi kuwaibia watu mahotelini
Mtu kutwa,kutunza hela kwenye bendi
Hapohapo mtoto wake anadaiwa ada nk,sasa hyo akili matope

Ova
Nasikia hata Mpaka reli alikuwa mwizi wa funguo akiwa hotelini utamuona wa maana kumbe ana yake na yale mambo ya gereji nasikia ilikuwa kisingizio tu
 
Nimekulia Sinza ile ya akina Remi ndio wanatamba na Volkswagen imeandikwa.''mambo kwa soksi'' tulikuwa tunajua karibu vijana wote, hivi sasa Sinza imebadirika ni Sinza ya magorofa,mahoteli,vijana wote wa zamani ama wamerudisha namba kwa Sir God ama wamehamia sehemu nyingine nje ya mji,nyumba nyingi tulizokuwa tunapanga chumba kimoja kimoja zimebomolewa na kujengwa mahekalu, nakumbuka pale sinza madukani kulikuwa na mbabe wa kikurya Lucky baba yake alikuwa usalama wa Taifa,namkubuka bibi Uliye alikuwa na mabinti kama 10 hatari sana, nakumbuka akina Banza stone wakiwa wadogo wakicheza disco mtaani, nakumbuka Vatican City ikiwa hotel kumbwa Sinza na Simba walikuwa wakiweka kambi hapo, namkumbuka Fred Mwalasha akiwa ametoka Ulaya na mke wa kizungu ikawa yeye ni bangi na bangi na yeye hadi mwanamke wa kizungu akamkimbia, siku hizi sinza yamejaa madangulo na wazee wale waliokuwa na nyumba ambazo tulikuwa tumepanga nao hatunao duniani ila zile nyumba walizoacha watoto wao wameziuza kwa matajiri na kwenda kunywea pombe na kula sembe. Sinza ya sasa si ile tuliyokuwa tunaitimba, ama kweli siku hazigandi.

Siku hizi madukani hadi whiteinn watu wanapanda bodaboda ujue, kweli wewe sinza star, hapo nilitania tu wengi walioshtuka mapema wako zao madale, kibaha hadi kongowe kuna wana wa kino walienda kujiweka huko na maisha yanasonga, vatican, kijiweni, kwa remi duuu siku zinakimbia acha tutulie tu hatuna namna vunja mfupa meno bado iko ndio hivo
 
josee maina, dr Said Mabera, juliana Augustino na haruna furgerson( sijui kama nimeliandika kwa usahihi) yalikuwa yakitajwa sana na msondo ngoma jazz band
 
Nilisikia huyu mwamba mali zake zimekamatwa na serikali ya Marekani pamoja na Ufaransa na pia ni kama yupo kizuizini huko Ufaransa,huyu mwamba ndiye amasemekana alinunua ile glove maarufu yenye vimulimuli vya dhahabu aliyokuwa anaivaa Wacko Jacko.
ni kweli, baadhi ya property zake huko europe zilikuwa seazed na baadhi zimeshapigwa mnada, hususani gari zake za kifahari.

ila haijaweza kumfilisi, bado ana fedha nyingi sana. ni mtu wa showoff, kila mara huwa anatupia picha au video kwenye page zake kuonyesha namna anavyokula bata nchi mbalimbali kwenye exotic beaches and five star hotels.eneo analolipenda sana ni visiwa vya carribbean.

kumbuka jamaa ni makamu rais wa equatorial guinea, lakini mda anao spend nje ya nchi kula bata ni mwingi kuliko mda anaotumia kubaki nchini kwake kuwahudumia wananchi.
View attachment 2279959
IMG_20220703_155314.jpg
 
Back
Top Bottom