Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Reila hajachuana na hadija kopa...maana nafikiri reila ameimba taarab akiwa na mzee yusuf labda ungesema nasma khamis kidogodogo
reilah khatibu( RIP),hakuwahi kuimba taarabu na mzee yusufu. unless unamzungumzia reilah mwingine, naruhusu kusahihishwa.
 
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Reila hajachuana na hadija kopa...maana nafikiri reila ameimba taarab akiwa na mzee yusuf labda ungesema nasma khamis kidogodogo
Mjuu wa bi nasma ni Doctor turkey ila kwake maisha ya kawaida mno
 
Shaban Ngalawa nilisomava tuition kwake wiki moja tu.

Pale mitaa ya kimara resort (vidudu)na tulikuwa tunafanya mitihani kwake enzi hizo.

Alikuwa mfupi hivi anapiga panki kifuani anaacha vishikizo viwili juu wazi na cheni inabembea na bonge la mustache.
 
Hakua na issue yoyote aliku anakaa kwao kota mpk anazeeka..
Nakumbuka alipigwa ridandasi nbc ela za mafao ndio akaweka heshima bar.
Shabiki kindakindaki wa wajelajela gwa
Kuba mwana mmoja alikuwa jirani yetu hapo dar somewhere alikuwa anatupa stori kuwa jimmy chocolate alikuwa anawambato sana maduu wa kino enzi zake.
 
Tunamkumbuka kama Shujaa wetu na mtu mwenye mapenzi ya kweli na kisarawe alikuwa mkurugenzi wa Bandarini ila Faida yake mpk Leo baadhi vizazi bado ipo sio yule bwana waziri anafaida yeyote zaidi ya kuongeza wake... Tunamsubiri kwa Hamu 2025...
Nilishaona mzee Mohamed said akimsfia kwenye moja ya nyuzi zake huku.

Pamoja na yule dr dau wa nssf ambaye alianzia huko bandarini.

Uliposema mtoto wa mzee janguo yuko Nssf leo

Yes the dot is connected.

Kwaheri[emoji2]
 
Mzee inawezekana tulikulia mtaa mmoja.

Yeah Shaban Ngalawa alikua mfupi haswa, enzi zile wanafunzi tulimpaga jina la utani "Mwalimu Kiroba"

Mda unaenda kwa kasi sana...
 
ninachoupendea huu uzi tangu nilipoupandisha haujawahi kupoa. kila ikifika mida ya jioni(east african time)mida ya ku relax na kupata moja moto moja baridi, uzi unaamka upya. mnanipa faraja sana wadau.

nipo zangu hapa arusha ktk bar moja maarufu nalainisha koo huku napitia comment zenu na kusikiliza rhumba kali zilizotamba miaka ya 2000-2010, honestly it's 100% a vibe.

halafu ninachojifunza ktk huu uzi, wote wanaozungumziwa walitafuta pesa kwa nguvu zao legally and illegally, hakuna uchawa. hii ichukuliewe kama lesson kwa nyinyi vijana wa generation ya instagram, tiktok na platform zingine za kijamii.

ma-senior wenzangu, mmesikia kwamba wenge bcgb ile ya Werrason na JB mpiana inarudi tena?. binafsi nawasubiri kwa hamu kubwa hawa magwiji. wapo studio kurecord nyimbo zao mpya. haya wenye mziki wao wa rhumba na seben wanarudi upya. i can't wait.
 
Sikujua kuwa pacha mmoja alishatutoka! Maskini
Toka 2019.

Alifariki kwa ajali ya gali hapo Mbezi, usiku anaingia barabara kuu akiwa maji kidogo kumbe kuna fuso imejaa nyanya inatokea Afrikana ikamvaa kuja mjini, biashara ikaishia hapo.
 
Hem
Hemedi Bakayoko alikua waziri mkuu wa Ivory Coast na alifariki mwaka jana kwa Kansa.

Kabla ya kua waziri mkuu alikua meya wa Mji wa Abijan kwa muda mrefu na ni alikua mpenzi sana wa muziki wa kongo toka Extra Musica wanamuiba akiwa kijana mdogo miaka ya 90.

Ni mtu alikua na mpunga mkubwa miaka mingi tu.

Amefariki mwaka jana akiwa na miaka 55.
 
Kweli huyu bakayoko kwnye twanga fotoo nimesikia jina lake
Amefariki mwaka jana alikua waziri Mkuu wa Ivory Coast.

Ni mdau wa muziki wa Congo miaka mingi sana.

Amefariki akiwa na miaka 55. Alikua meya wa Abijan kwa miaka mingi na pia waziri.

Ukisikiliza hata extra Musica walikuimba miaka ya 1998.
 
Kilivyoingia chuma pale Ikulu ndio ikawa mwisho wa hao watu. Huku ikisemekana walijipatia ukwasi nje ya mstari sahihi.

Na ndio ikawa mwisho wa mziki wa dance hapa nchini hadi sasa. Maana walitegemea udhamini wa hao watu.
Jiwe aliua mziki wa dansi,
mapedeshee walimwaga pesa Sana mtaani[emoji4]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…