Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Uelewe tu kuwa kuna habari ukitoa za uongo tutakurekebisha........
umekurupuka.
tuliza akili, soma post kwa utulivu, digest kile ambacho umekisoma halafu changia maoni yako.

karibu tena ndg.
 
Aisee... Kumbe ndo huyu mwamba.... Dadeki... Pedeshee haswaaa
 
Nilisikia huyu mwamba mali zake zimekamatwa na serikali ya Marekani pamoja na Ufaransa na pia ni kama yupo kizuizini huko Ufaransa,huyu mwamba ndiye amasemekana alinunua ile glove maarufu yenye vimulimuli vya dhahabu aliyokuwa anaivaa Wacko Jacko.
Aisee.... Kama ndiye aliyenunua ile glove, basi jamaa ana ukwasi usiopimika...
 
Huyu abdalah nyumba nyingi,yeye alikua na mishe gani
Kuna mtu kama jina hili alinipigia simu siku chache zilizopita na akajitambulisha kwa jina hilo na akasema kama yupo Tanga na itakuwa yeye ananifahamu sema mie bado sijamkumbuka (Maongezi yetu ilikuwa ni kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo) hapo wakubwa mtakuwa mmeelewa
 
aliyekupigia simu na kujitambulisha kwa hilo jina atakuwa amefanya hivyo ili kumu idolise the original Abdallah Nyumba Nyingi ambaye kwa sasa ni marehemu. alifariki miaka kadhaa iliyopita.

jina lake lilikuwa linaimbwa na bendi ya wana tamtam chini ya mwinyijuma muiminin na band ya twanga pepeta chini ya ally choki.

Abdallah Nyumba Nyingi alikuwa ni mtoto wa mjini aliyekulia mitaa ya temeke. alikuwa mtu wa karibu sana na marehemu Meddy Mpakanjia.

nakumbuka nilihudhuria sherehe ya harusi yake iliyofanyika ktk ukumbi wa chuo cha IFM mjini posta, hiyo ilikuwa mwanzoni miaka ya 2000.

sherehe ilifana sana, ukumbini alikuwepo meddy mpakanjia na rafiki zake. kipindi hicho meddy yupo kwenye ubora wake, pesa anayo halafu ana date na binti maarufu wakati huo, marehemu amina chifupa.

kwa sasa wote ni marehemu. may their souls continue to rest in peace.
 
Mzee malay nlifanya kazi kwake
Za kutumwa hapa na pale upande wa dokomaa....enzi hzo nlikuwa dogo nasoma natafuta pesa
Umenikumbusha aise,alikuwa smart sana ila kuna wakat fulani nlimuona
Alikuwa tofauti nlijisikia vibaya sana

Ova
Naikumbuka hii kampuni ya Malai napokuja mjini ndo Mzee mwenyewe alikuwa ameisha fariki wapo wale wadogo zake ndo wanaiendesha nilipata kuwa karibu na baadhi ya staffs wa hapo nawajua baadhi wa miaka hiyo ambao wengine walikuwa wacheza basketball kuna wale kina Abeid alikuwa sana airport kuna kina mbaga,Otto,Mashele,mwamboma,Efreim,

Mie nikiwa bwana mdogo tu nafundishwa fundishwa mambo ya C&f na jamaa zangu nimetoka kwetu unyamwezini tukiwa kijiwe chetu hapo kwenye hilo jengo lililokuwa linauza vyombo sijui jina Hosco House ,Samora Ave , hapo ni shift tu natumwa tumwa kwenda 'Long room' mara kukagua gari/containers bandarini na kurudi kujibanza hapo 'Hosco House' ndo kuna mihuri ya kugonga ya C&F na kampuni ilikuwa ya mzee wa Kichaga Mzee Mushi jamaa zangu wanakamata kazi lkn mihuri tunatumia ya huyo Mzee ,nae kajaza vijana wake toka Moshi, kina Basil,Frank,Peter Kipara NK

Vijana wa Clearing & Forwarding walipata pesa sana miaka hiyo ya 90+ , namkumbuka kijana mmoja wa kinondoni alikuwa maarufu sana hapo 'long room' anaitwa Ally Kilinda RIP kama sijakosea jina na girlfriend wake Fatuma RIP bila kumsahau Swetu Fundikira RIP na akiniona lazima aniulizie salamu za jamaa zake wa unyamwezini kina Adam

Nakumbuka pia na ushamba wangu huu kuna mzee wangu alitoka nje ya nchi akaja na simu (Alcatel) ya hizi chip/simcard za siku hizi hapo kabla ilikuwa bado hazijaanza kutumika nchini lkn ndo kipindi tunakaribia kutoka analogue kuja digital, mzee wangu akaniambia nikauze hiyo simu nilikuwa nawajua jua vijana baadhi pale Azam kama yule half caste muhindi na muhaya kama sikosei anaitwa Rajesh ndo walikuwa wana zungusha hapo vijiwe vya Azam na vijana wa mjini wengine kina Ukwaju,Dan,Joel,Kinje (siyo yule maarufu zaidi huyu ni ndugu yao alikuwa sana hapo Azam miaka hiyo) dah kweli miaka imeenda

Sema namshukuru Mungu mie nilitaka kuwa maisha yangu yawe ya kawaida 'low key' toka kitambo japokuwa ningetaka kuwa tofauti labda na kuwa hata na ka jina jina hapa mjini fursa zilikuwepo lkn haikuwa kipaumbele changu na hasa kujua wapi nilipotoka na kubwa toka kijana mdogo nilianza kuheshimu kitu kinachoitwa 'Karma' kwa kila ulitendalo ndo utavuna/utalipwa , naingia utu uzima kwa amani tele naomba na mwisho wangu uwe wa amani

Sorry kwa mtoa mada nimeweka yasiyo husiana na mada haha
 
Nashukuru sana kwa kunifahamisha maana mtu kanipigia simu anajitambulisha kwa jina hilo na anasema yupo Tanga ni siku chache tu zimepita,nafikiri huyu alipachikwa jina hilo la huyo muhusika OG ,RIP
 
Nashukuru sana kwa kunifahamisha maana mtu kanipigia simu anajitambulisha kwa jina hilo na anasema yupo Tanga ni siku chache tu zimepita,nafikiri huyu alipachikwa jina hilo la huyo muhusika OG ,RIP
[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]
 

umetema madini ya zamani sana. mimesoma kwa utulivu mno huku niki recall mitkasi yetu ya azam take away.

nimewakumbuka mabroo wa wakati ule na viofisi vyao vya kupiga mishe za ujanja-ujanja nyuma ya club billcanas(siku hizi mitaa ya jengo la Rita).kule nyuma kulikuwa na vijiofisi vingi vya wapigaji.

huyo Ukwaju uliyemtaja kwenye post yako ndio yule jamaa mmoja hivi mfupi mnene kiasi aliyekuwa shabiki mkubwa wa kilimanjaro band(wana njenje)?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…