Naikumbuka hii kampuni ya Malai napokuja mjini ndo Mzee mwenyewe alikuwa ameisha fariki wapo wale wadogo zake ndo wanaiendesha nilipata kuwa karibu na baadhi ya staffs wa hapo nawajua baadhi wa miaka hiyo ambao wengine walikuwa wacheza basketball kuna wale kina Abeid alikuwa sana airport kuna kina mbaga,Otto,Mashele,mwamboma,Efreim,
Mie nikiwa bwana mdogo tu nafundishwa fundishwa mambo ya C&f na jamaa zangu nimetoka kwetu unyamwezini tukiwa kijiwe chetu hapo kwenye hilo jengo lililokuwa linauza vyombo sijui jina Hosco House ,Samora Ave , hapo ni shift tu natumwa tumwa kwenda 'Long room' mara kukagua gari/containers bandarini na kurudi kujibanza hapo 'Hosco House' ndo kuna mihuri ya kugonga ya C&F na kampuni ilikuwa ya mzee wa Kichaga Mzee Mushi jamaa zangu wanakamata kazi lkn mihuri tunatumia ya huyo Mzee ,nae kajaza vijana wake toka Moshi, kina Basil,Frank,Peter Kipara NK
Vijana wa Clearing & Forwarding walipata pesa sana miaka hiyo ya 90+ , namkumbuka kijana mmoja wa kinondoni alikuwa maarufu sana hapo 'long room' anaitwa Ally Kilinda RIP kama sijakosea jina na girlfriend wake Fatuma RIP bila kumsahau Swetu Fundikira RIP na akiniona lazima aniulizie salamu za jamaa zake wa unyamwezini kina Adam
Nakumbuka pia na ushamba wangu huu kuna mzee wangu alitoka nje ya nchi akaja na simu (Alcatel) ya hizi chip/simcard za siku hizi hapo kabla ilikuwa bado hazijaanza kutumika nchini lkn ndo kipindi tunakaribia kutoka analogue kuja digital, mzee wangu akaniambia nikauze hiyo simu nilikuwa nawajua jua vijana baadhi pale Azam kama yule half caste muhindi na muhaya kama sikosei anaitwa Rajesh ndo walikuwa wana zungusha hapo vijiwe vya Azam na vijana wa mjini wengine kina Ukwaju,Dan,Joel,Kinje (siyo yule maarufu zaidi huyu ni ndugu yao alikuwa sana hapo Azam miaka hiyo) dah kweli miaka imeenda
Sema namshukuru Mungu mie nilitaka kuwa maisha yangu yawe ya kawaida 'low key' toka kitambo japokuwa ningetaka kuwa tofauti labda na kuwa hata na ka jina jina hapa mjini fursa zilikuwepo lkn haikuwa kipaumbele changu na hasa kujua wapi nilipotoka na kubwa toka kijana mdogo nilianza kuheshimu kitu kinachoitwa 'Karma' kwa kila ulitendalo ndo utavuna/utalipwa , naingia utu uzima kwa amani tele naomba na mwisho wangu uwe wa amani
Sorry kwa mtoa mada nimeweka yasiyo husiana na mada haha