Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Daaah,kipindi cha Magu walipoteana hao hakukuwa na kutajana tena 🤣🤣🤣

Kila mtu alipambania hali yake hakuna cha papaa msofe, wala papaa nani 🤣🤣🤣
 
wee jamaa takuwa nakufahamu hio miaka na hao watu uliowataja karibu wote nawafamu, hivi mzee Mushi yupo?? ulivyomtaja Swetu Fundikira-rip ukamsahau na aliemfundisha kazi ya C&F jamaa akiitwa Charles Sanga - rip. wakati huo long room tunaondoka na mifuko ya rambo imejaa pesa zingine tunapitia kitumbini kwa mzee Zakaria-rip. Wakati huo Kinondoni inawaka moto haswaa haswa hapo kwa manyanya na PR Camp. maisha hayaaaa...
 
Kijiwe cha azam kuna jamaa mmoja akiitwa Peter alikua sana pale na kina Amani, huyu Peter alikua mwajiriwa wa bima halafu akapigwa redanduncy akawa mission town hapo kijiweni. ulevi wake ulikua pale kontena opposite na soko la ma TX. kitambo sana hio.
 
Charles sanga alifariki nakumbuka tulikuwa tunapiga mvinyo hapo kwa ashura macheni,usiku mnene
Kama pumzi ikambana....
Ila mpaka naondoka hapo Charles nlimuacha...badaye nasikia jamaa ntolee
Office yake ilikuwaga nyuma ya shule ya forodhani pale

Ova
 
Alikuwepo omary urembo naye clearing agent,ma clearing wengi walikuwa wazushi wazushi tu
Ila omary urembo naye alivuta miaka kama 7, hv nyuma

Ova
 
Kontena pale kwa mama propser
Kilikuwa kijiwe haswa...
Support asubuhi watu wote wanajaa opposite na kinondoni makaburini
Watu wanapiga supu wanaenda mzigoni

Ova
 
Dah wakina kilinda nawajua wote
Familia yao pia nko nayo karibu tu
Nimeishi pia mitaa ya kule kwao sana

Yah,malay alikuwa na office kubwa na wakat ule watu walipiga hela maana mteja hajui chochote kilichopo kwenye system,anakadiria malipo tu na agent....
Malay vijana wengi enzi hizo aliwaingiza kazini,jamaa hakuwa mchoyo wa kutoa fursa
Sema wakat ule sisi ule utoto,ujana sana ulitusumbua wengine maana kutulia ilikuwa 0

Ova
 
Tam tam band ilimtaja Papa Alex Massawe A.M
 
Alikuwepo omary urembo naye clearing agent,ma clearing wengi walikuwa wazushi wazushi tu
Ila omary urembo naye alivuta miaka kama 7, hv nyuma

Ova
Daaah na wewe takua nakujua maana hio mitaa ya kinondoni ndio ilikua yetu enzi, Omary Urembo nafikiri ndio yule tulikua tukimuita Omari kichwa nasikia na yeye alivuta pia, Sanga nae story yake nilisikia hivyo hivyo ulivosema. Mie nilivoona bongo miyeyusho mpunga niliovuta long room nikaona nitambae kwa Joe Biden mpaka leo nikija huko ni vacation tu week 2/3 narudi zangu. bongo ya sasa imejaa waturutumbi wengi haisomeki.Huyo Peter ndio simsikii kabisa. Kinondoni ilikua motoooo.
 
Hahaha kinondoni ilikuwa moto
Sema si haba angalau wengine tumeacha legacy tu [emoji1]
Makazi ya kudumu +nlihamia madale
Ila bado kinondoni nai respect maana
Ilitujengaaa sana,kutupa uthubutu

Yah omary urembo alivuta alienda kenya huko akaugua gafla, alikuwa mtu wa kamali sana na starehe
Ukimpa kazi lazima kuwe na maneno maneno kalenda nyingi...
Ile kutokuwa mwaminifu inakuaribia soko mwisho wa siku wateja wote wanakukimbia
Ma clearing wengi walikuwa wanavimba na hela za wateja wao tu
Huo ndy ukweli
Ndomana miaka ilivyokuwa inaenda wakaingia watu wa kazi kweli kwenye field hyo na kuwaulia soko lao

Ova
 
Exactly [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ubalozi wa south uko mjini Kati kabisa sheikh,sio masaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…