Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania


Papaa Fikiri Madinda yupo. Ni dereva serikalini Wizara ya mambo ya nje
 
mrangi ktk ubora wako wa story za mujini na pilikapilika zake.
 
Fikiri Madinda, alikuwa ni dereva wa serikali pale Mifugo na uvuvi kwa sasa Temeke. shughuli yake kubwa ilikuwa ni kufunga mitambo ya bendi. alikuwa anafanya kazi ikifika saa tisa gari imeshapaki anaaga anakwenda kwenye kazi za bendi ambazo mara nyingi ilikuwa inaanza kutumbuiza mida ya jioni.
 
Huu uzi siyo wa wakongwe ni wa vijana wa mjini! Nimesoma kuanzia page ya kwanza mpaka mwisho. Nimejifunza mengi. Kwa upekee kabisa, shukrani kwa wahenga wenzetu mrangi Matola mfianchi Carlitos Way
mbona umesahau kunitaja na mimi ambaye nimeanzisha huu uzi?.nimwagie maua yangu ningali hai kaka.

kama maandiko matakatifu yanaonyesha Mungu anapenda kusifiwa (Zaburi 150:1-6), mimi ni nani nisepende kusifiwa.

au unasubiri mpaka siku nirudishe namba kwa sir God ndio uje uanzishe uzi wa kunisifia?.

kama vipi acha nijifagirie mwenyewe, naitwa papaa smarter, mutu ya mujini, baba yake na janeth.

NB: ni utani tu wadau, msichukulie serious.[emoji1787][emoji1787]
 
Ndugu yangu hebu angalia vizuri andiko langu mpaka mwisho. tena nimekutaja kwa upekee kabisa.
 

Usimsahau Pedeshee Jack Pemba.

Kuna kawimbo kamoja walimuimba "wewe ndiyo baba watoto wangu Jack Peeeeeemba"

Huyu bwana stori yeye ni mutoto ya Upanga, kule kwa akina East Coast akina King Crazy GK, MwanaFA, AY, n.k.

Kule bwana vijana dili zao kuu ilikuwa ni kuzamia Unyamwezini - Marekani au Uingereza.

Sasa bwana Jack Pemba alifanya kitu kimoja ya kipekee ikaacha gumzo kwa waliokuwa wanamjua kabla kajawa maarufu wa kuimbwa na bendi.

Bwana Jack Pemba alipomaliza sekondari akawa anataka kwenda majuu ila hana kitu. Unyamwezini kunahitaji nauli na kunahitaji salio liwe linasoma kwenye bank statement ili upewe viza.

Basi akaitisha harusi bwana. Michango ikafika kama milioni 22 hivi, akazizoa zote ndo ukawa mtaji wake kwa kuwendea Unyamwezini. Harusi ikabaki stori, binti wa watu analia halafu baadae ikabidi acheke tu kutokana na muvi kabamba lililochezwa. Yeye mwenyewe akakubali kwamba sio kwamba hapendwi, bali alikutana na mwanaume mwenye ndoto kubwa sana.

Jamaa akaruka kwenda Uingereza. Kule akachakarika kupata jimama la kizungu Mwingereza mzawa, akamchanganya kwa dozi za kibongo mama akafunga ndoa na Jack Pemba.

Basi kuanzia hapo jamaa mipango yake ikawa imeshatulia kwenye reli. Kupitia jimama lake akafanikisha connection za kuvuta mipunga ya wazungu kwa ajili ya kuja kuanzisha shule za soka "Afrika" (maana wazungu hawajuagi Tanzania).

Ndo akaja Bongo akiwa na pesa alizopewa kuja kufungua shule za soka ila akazigawa kidogo zingine akawamwagia waandishi wa udaku na wanamuziki wa bolingo wampaishe.

Basi ikawa ni bata batani huku jina lake likivuma kila mahali. Kwenye magazeti ya Shigongo yumo, na kwenye sauti za wakongomani wa Kinondoni yumo!

Mara ya mwisho alisikia akiwa Uganda ambapo alionekana akiwa kwenye picha moja na magari ya kifahari aina ya Range Rover wadau tukachukulia kuwa ni yake na kwamba anaendelea kupiga bakora Uganda.

Pia alionekana kwa Mange Kimambi ambapo alimuhonga Mange vidolari vya shopping basi Mange akamposti na kummwagia masifa kibao. Kwa kuwa ilikuwa ni baada ya Mange kuwa ameshatalikiwa na mume wake mzungu wadau wakahitimisha kuwa itakuwa alimmwagia na maziwa ya kiume.
 
nakumbuka aliwahi kuanzisha kampuni ya kijanjanjanja ya kuwafanyia scouting wachezaji wachanga wa mpira hapa bongo. sijui ile kampuni ilifia wapi.
 
nasikia michezo ila cjaelewa ni michezo gan hiyo waliyokuwa wanacheza na kina tra
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…