Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Enzi hizo concert za wanafunzi zinafanyika Diamond jubilee,..... wakati wa fashion show kajala alipanda stejini alipofika katikati ya steji akavua khanga aliyojifunga kiunoni akabaki mtupu..[emoji17]..[emoji17].... ukumbi wote ulizizima.....
Naona safari yake ya kuvua nguo stejini ndio ilianziaga hapo.....ikawa kila concert lazima awepo na lazima avue nguo[emoji26]
katika huo msiba, marehemu moody mas pia alikuwepo, ni kama alijipeleka kwenda kuagana na marafiki zake.
nimemuona papaa madenge akiwa anapiga story na tajiri davis mosha. hakika msiba uliwakutanisha wototo wa mjini.
Aisee RIPa legend, a brother, mtoto wa mjini, borntown, mwana dar es salaam has gone. rest in peace moody mas.
watoto wa mjini bila shaka mnamkumbuka vizuri huyu brother. alikuwa anashinda sana mitaa ya somora. pia walikuwa na duka lao la nguo jirani na jm mall.
ni msiba uliogusa hisia za wengi hususani watoto wa mjini wa ile generation iliyosumbua sana mitaa ya samora avenue,mkwepu street na lumumba.
copy to mrangi and others.
View attachment 2363142
MkuuAise na kulikuwa na huu msiba
Kuna mwamba anaitwa Abdul bagdera, baharia fulani alifia nje
Aliletwa kuzikwa kisutu
Huu msiba ulikuwa na watoto wa mjini
Wengi wa zamani
Ova
View attachment 2363158
Pole sanaAisee RIP
Siamini mpaka sasa hivi, Moody tumesoma wote Jite.
Aisee, sikuamini nilivyosikia....RIP mate...
Wote tuko njia moja, wewe umetangulia....
marehemu moody kafariki akiwa around 40s. inawezekana wewe ni agamate wangu cos kwa sasa nacheza kwenye early 40s.Mkuu
Hii inakumbusha kwamba sasa nimezeeka, nimeona washkaji kibao nimesoma nao
Na RIP Moody ...dah....sio mchezo..
naam,ndio huyo....msiba uliwakutanisha vijana wa zamani....makontao wa jiji.
Aisee..kweli mkuumarehemu moody kafariki akiwa around 40s. inawezekana wewe ni agamate wangu cos kwa sasa nacheza kwenye early 40s.
vijana wengi wa umri wetu wamesharudisha namba, wengine wanaishi kwa matumaini.
tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kufikia umri huu tukiwa wazima kiafya, mashababi, hatuna maradhi kama kisukari, Bp na hatumezi vile vidonge vya kufubaza naniliyu.
generation yetu ime survive mabalaa mengi sana.
Mwinjuma alimzingua JK kwa sifa zake akamtolea mbavuniMwinjuma muuminu anazuza kuku wa kukaanga mtoni kwa kindande temeke
Huyo Ally Kitobo na mbwembwe zote hadi leo anapanga majuzi tu kidogo apigwe risasi mitaa ya Mbezi Beach alikwenda kumfanyia unyoko mzee mmoja wa mjini anaitwa Fadhil Mganga(walikuwa jela wote na Msofe). Kwa sasa Kitobo anaishi kama digidigi na hasa ukichukulia hana shuleMsofe nilikuwa naonana sana na Mpambe wake mmoja akiitwa Ally Kitobo mdogo wake Ally aliitwa Nuhuh huyu ndiye tuliyekua karibu sana tukiishi wote Magomeni Makuti Akachube Road kipindi bado pakiitwa Somanga pamoja na jamaa zangu Yahya na Danny Malumbo (Mungu amrehemu Yahaya tumemzika kwao Kondoa Feb mwaka huu alipata ajali Tanga na IST akielekea Holili) kila ijumaa pale makutano ya mitaa ya Livingston &Amani kuna bibi alikuwa anaitwa Bi Jang’ombe alikuwa mpishi wa biriani tamu sana so tulikuwa tunaenda kula biriani la offer kutoka kwa Msofe ila jamaa sikuwahi kumuona.
Huyo Ally dereva wake ndiye aliyekuwa mshika pesa ilikuwa siyo ajabu kumkuta anashuka na 2Mill kwenye gari kwa ajili ya matumizi mbalimbali,hela yake unaifadi akikupa kazi aisee nilikuwa naamkia shikamoo nyiingi mwisho naondoka na 50K maisha yanaenda kuna siku alinipa 100,000/= ya kununua Big G original kwa ajili ya kulia mirungi sasa packet sikumbuki exactly ilikuwa bei gani ila haikuzidi Tsh 12,000/= nikajiuliza ninunue ngapi sasa nikamuuliza mdogo’ake Nuhuh ninunue ngapi akaniambia chukua moja tu change tukagawana then hakuna aliyeuliza.
Jamaa hata kama hela zao zilikuwa chafu Ila mtaa waliuchangamsha kweli kweli,Msofe kabla hajang’ang’aniwa na mamlaka alikuwa na BMW X3 metallic gold kali sana haizimwi muda wote ipo on.
Ilikuwa enzi za JK zile Msofe alikaa sana Keko hadi akawa mweusi.. Mzee Massawe alikimbilia ughaibuni sijui kama amerudi..mwisho wa siku Msofe aliachia ile nyumba plus na riba na usumbufu kwa mjane.Ile nyumba ipo mitaa ya Mikocheni.Ni Papaa Msofe na marehemu alikuwa muuza madini!
Ila Msofe yeye alikuwa hana mambo ya bunduki alijichanganya kwa Mchagha Masawe Alex akanunua nyumba iliyokuwa dhamana ya mkopo kati ya marehemu na Masawe so Mchagha alivyopokea hela akavunja uwa akaenda South huku nyuma Msofe akamtaka mmiliki wa awali ahame achukue nyumba yake jamaa akagoma akataka kupeleka kesi mahakamani Masawe kusikia hivyo na kuogopa kuambiwa arudishe hela akarudi akatuma kikosi kazi kikammaliza jamaa ilikuwa mapema tu saa 19:50 usiku.
Msofe aliunganishwa kwenye kesi kutokana na simu ya marehemu kukutwa na chatting kutoka # yake zilizoonyesha kutofautiana na jamaa muda mfupi kabla ya kifo chake.
Hebu tupe story kidogo MkuuMwinjuma alimzingua JK kwa sifa zake akamtolea mbavuni
Davis Mosha ndio kaachia minywele na midevu vile?