Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Kuna mtu mmoja nimemwambia kwenye uzi huu, asidhani kwa kuwa siku hizi baadhi ya majina ya mapedeshee hayasikiki, basi wamefilisika, la hasha.

Bado ambao wanapesa ya kutosha ila wameamua tu ku lay-low. hawataki tena shobo za umaarufu na kutajana majina.

Lakini wapo wengine ambao waligundua umaarufu ulikuwa uwatengenezea hali ya kufatiliwa maisha yao na mamlaka, hususani kipindi cha mwendazake.

Siku hizi wanafanya mambo yao kimyakimya legally and illegally. Mwendo ni uleule.
 
Umenikumbusha Haji Mbabe alitusumbuwa sana Sinza enzi hizo
 
Bila kimtaja Mohamed Mpakanjia huu uzi haunogi
 
Unaujua ule wimbo
Nimepoteza kipenzi changu hapa tanzaniaaa🎶
Nimepoteza mkanda wa kiuono🎶
Nitarudii kwa Hidayaa🎶 hidayaaa hidayaaa🎶

Unaambiwa Hidaya alikua ni mrembo vibaya sana enzi za uhai wake akiwa kijana
Pepe Kale hakumuimba Hidaya mwanamke, aliimba HEDAYA wema na mapokezi makubwa aliyoyapata Tanzania (Kule Arusha, Kule Morogoro, Kule Mwanza). Alitumia kiswahili sanifu tu. Na huo wimbo hakuutunga Tanzania ila aliuandaa na mahsusi baada ya ziara ya Tanzania. Kumbuka kipindi hicho haikuwa rahisi kuipata bendi au mwanamuziki wa Congo (Pepe Kale, Boziboziana, BongoMan, Loketo/ Aurlus Mabel), Papa Wemba, Wenge Musica BCBG nk). Kumbuka soko lao lilikuwa Afrika yote hasa Afrika Magharibi. It was so amazing!!
 
Yeye mwenyewe kasema alimuimbia Hidaya na alimrudia hadi kuzaa amezaa na huyo Hidaya Kama hujui ndo ujue leo
Hidaya alikua anaishi Arusha na kafariki mwaka jana
 
Uncle Salehe ni mwandishi alikuwaga bbc swahili baadae akawa mbunge
Uncle Saleh huyo sidhani kama ni Ali Saleh mwandiahi wa habari. Huyu alikuwa akiitwa Saleh Jabir??, (kama nimepatia jina la ubini wake) maarufu uncle Saleh mtangazaji wa TVZ enzi hizo akitangaza kipindi cha miziki na dada mmoja akiitwa princess Selme.
 
Yeye mwenyewe kasema alimuimbia Hidaya na alimrudia hadi kuzaa amezaa na huyo Hidaya Kama hujui ndo ujue leo
Hidaya alikua anaishi Arusha na kafariki mwaka jana
Kasema wapi? Jiulize kama huyo Hidaya alikuwa Arusha why kwenye wimbo amtafute iwapo alimuona Moro au Arusha, au Mwanza. Ilitengenezwa tu na wabongo.
 
Ruge na kusaga walishiriki kikamilifu kuua mziki wa dansi tena kwa fitina za wazi, kama mradi wa kujiongezea kipato kibwanyenye.
Ruge alitoka USA na maono hayo.
Mziki ni kama chakula, unawalisha watu unachotaka tu hadi wanaamin ndo kitamu.
Pia kuliibuka saikolojia ya mziki mfupi dk 4 ndo upigwe radio na tv wakat kwa dansi unaua utam wote.
Pia gharama za kuendesha dansi kwa faida zikawa juu kuliko bongo fleva, ikampa standing point mfitini wa dansi.
Umarekan na uniga wa akina sugu, na prof j, nature, sele n.k nao ukachukua hatam.
Lakin ukiachilia mbali suala la gharama bado dansi ndo mziki kabsa kabsa kwa walio wengi. Bas tu, tunalishwa tunachopikiwa bila menu!
Ndo maana likipigwa sebene hata nikki wa pili atajitingisha tu!
 
Kasema wapi? Jiulize kama huyo Hidaya alikuwa Arusha why kwenye wimbo amtafute iwapo alimuona Moro au Arusha, au Mwanza. Ilitengenezwa tu na wabongo.
Acha ubishi mzee mwenyeji wa Arusha wote hakuna asie mjua Hidaya tena alikua maarufu kwa jina la Hidaya Wa pepe kale kafariki mwaka jana , Hidaya ni miongon mwa wanawake matajiri wa Arusha enzi hizo, ameishi pia france ninavyo kueleza kafariki mwaka jana elewa hivyo
Alafu mi nazungumzia wimbo wa pepe kale Hidaya hiyo ya kwako ya Hedaya mimi siijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…