Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Nadhani hizi FM station kidogo zilishindwa ku promote muziki wa dance.

Mussa mzee wa korosho huyu ndio babake na Jux mwimbaji. Huyu maarehemu

Dr Ayoub siki hizi nadhani ni Profesa Ayoub wa magonjwa ya akili

Pedeshee Ndama Mtoto wa Ngombe aka Akayesu huyu bado tajiri sana

Papa musofe chuma cha reli mbongo wa kwanza mjanja kuvaa pure gold nyingi mkimya kwa haiba lakini ana akili za kimafia za hela hatari. Huyu kuna sehemu akifika na gari hashuki hapendi macho ya watu sana.

Papa Davis Mwangaba mzee wa Temeke huyu alikuwa anatembea na millioni kadhaa kwemye buti la gari. Kaka yake ndio mwenye mbumba ya hatari mzee Mwangaba tajiri wa Temeke

Papa Muddy mas mzungu wa roho kawasafirisha washikaji kibao kwenda ulaya waliokuwa wana hustle town na hawakuwa na uwezo wa safari kwenda kujilipua ulaya

Wazee wa TCC kuna mwamba mmoja walikuwa wanamuita Abrahamovich naye alikuwa na mbumba za kusumbua kiumeni TMK area.
Kuna mtu mmoja nimemwambia kwenye uzi huu, asidhani kwa kuwa siku hizi baadhi ya majina ya mapedeshee hayasikiki, basi wamefilisika, la hasha.

Bado ambao wanapesa ya kutosha ila wameamua tu ku lay-low. hawataki tena shobo za umaarufu na kutajana majina.

Lakini wapo wengine ambao waligundua umaarufu ulikuwa uwatengenezea hali ya kufatiliwa maisha yao na mamlaka, hususani kipindi cha mwendazake.

Siku hizi wanafanya mambo yao kimyakimya legally and illegally. Mwendo ni uleule.
 
Maisha Kitendawili, Dr Rama, Abdala Nyumba nyingi, Bitebo saloon, Songolo, Haji mbabe mwanamanyema, somebody Miundombinu, utajiju Camp, Daladala camp, Andrew Trader, Side Mkuluma,Freedom Camp, Salumu na Merelani, Home alone camp, Salum masim, Chikago matelephone nk
Umenikumbusha Haji Mbabe alitusumbuwa sana Sinza enzi hizo
 
awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. itabidi msome kimya kimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity liwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

mwaka 2002 mpaka 2012, mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

kwa uchache tu, band zilizotamba ni fm academia, akudo impact, twanga pepeta na diamond musica. zingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

umuarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.
kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa john young millionaire muzee ya range rover[emoji3][emoji3].

haya twende kazi:
Pedeshee Mychoisi na Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko mbeya, watu wa mbeya mtatusaidia.

Braza K na Tunduma:
watu wa tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya mikocheni barabara ya rose garden. those days she was very pretty. kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnana:
bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV. baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za catering. shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana.sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. fm academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
alikuwa mmiliki wa band ya daimond musica kwa kuwezeshwa na mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages. watu wa zamani wanaelewa. juddy alikuwa mrembo si kitoto. kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
sina haja ya kumuelezea , ni mtu maarufu wa nyakati zote. wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Billgate Muzamil Katunzi:
Christian bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la muzamir katunzi. i don't know him personally, but it's told he was financially very successful.

Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa papaa msofe. itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana. halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
ni marehemu kwa sasa. huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya Fm Academia. nilikuwa namfahamu personally.licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer ktk Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi mpya za gari mtaa wa agrey kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiriwa kwa jina la general supply. ktk biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

pedeshee David Kabunga:
sifahamu alikuwa ni nani. jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Papaa Ali Kileo:
he was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe Big Boss:
anafahamika vizuri. jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero:
kwa sasa ni RC wa dar. jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: anafahamika vizuri, wajanja wa wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk mkoa wa morogoro. sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za lumumba.

Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba Kali...
?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Ntenze wa Ntenze....?
Bila kimtaja Mohamed Mpakanjia huu uzi haunogi
 
Unaujua ule wimbo
Nimepoteza kipenzi changu hapa tanzaniaaa🎶
Nimepoteza mkanda wa kiuono🎶
Nitarudii kwa Hidayaa🎶 hidayaaa hidayaaa🎶

Unaambiwa Hidaya alikua ni mrembo vibaya sana enzi za uhai wake akiwa kijana
Pepe Kale hakumuimba Hidaya mwanamke, aliimba HEDAYA wema na mapokezi makubwa aliyoyapata Tanzania (Kule Arusha, Kule Morogoro, Kule Mwanza). Alitumia kiswahili sanifu tu. Na huo wimbo hakuutunga Tanzania ila aliuandaa na mahsusi baada ya ziara ya Tanzania. Kumbuka kipindi hicho haikuwa rahisi kuipata bendi au mwanamuziki wa Congo (Pepe Kale, Boziboziana, BongoMan, Loketo/ Aurlus Mabel), Papa Wemba, Wenge Musica BCBG nk). Kumbuka soko lao lilikuwa Afrika yote hasa Afrika Magharibi. It was so amazing!!
 
Pepe Kale hakumuimba Hidaya mwanamke, aliimba HEDAYA wema na mapokezi makubwa aliyoyapata Tanzania (Kule Arusha, Kule Morogoro, Kule Mwanza). Alitumia kiswahili sanifu tu. Na huo wimbo hakuutunga Tanzania ila aliuandaa na mahsusi baada ya ziara ya Tanzania. Kumbuka kipindi hicho haikuwa rahisi kuipata bendi au mwanamuziki wa Congo (Pepe Kale, Boziboziana, BongoMan, Loketo/ Aurlus Mabel), Papa Wemba, Wenge Musica BCBG nk). Kumbuka soko lao lilikuwa Afrika yote hasa Afrika Magharibi. It was so amazing!!
Yeye mwenyewe kasema alimuimbia Hidaya na alimrudia hadi kuzaa amezaa na huyo Hidaya Kama hujui ndo ujue leo
Hidaya alikua anaishi Arusha na kafariki mwaka jana
 
Uncle Salehe ni mwandishi alikuwaga bbc swahili baadae akawa mbunge
Uncle Saleh huyo sidhani kama ni Ali Saleh mwandiahi wa habari. Huyu alikuwa akiitwa Saleh Jabir??, (kama nimepatia jina la ubini wake) maarufu uncle Saleh mtangazaji wa TVZ enzi hizo akitangaza kipindi cha miziki na dada mmoja akiitwa princess Selme.
 
Yeye mwenyewe kasema alimuimbia Hidaya na alimrudia hadi kuzaa amezaa na huyo Hidaya Kama hujui ndo ujue leo
Hidaya alikua anaishi Arusha na kafariki mwaka jana
Kasema wapi? Jiulize kama huyo Hidaya alikuwa Arusha why kwenye wimbo amtafute iwapo alimuona Moro au Arusha, au Mwanza. Ilitengenezwa tu na wabongo.
 
Hayo mengine sawa, ila kuhusu kukosa umaarufu kwa mziki wa dansi napingana na wewe.

Mziki wa dansi ulikuja kukosa umaarufu baada ya kuvuma kwa bongo fleva kuanzia miaka ya 2010 hivi.

Kabla ya mwaka 2010 ilikuwa ni nusu kwa nusu, yaani mziki wa dansi na bongo fleva ulikuwa unachuana katika mashabiki.

Chuma kimeingia ikulu 2015 huku mziki wa dansi ukiwa hoi bin taabani.

Hilo ni suala la kawaida katika fasihi. Nafikiri tunakumbuka kuna kipindi miaka ya 2000 hivi taarabu ilikuwa juu kuliko bongo fleva, enzi za Hadija Kopa na yule mama sijui alikuwa naitwa nani mpinzani wa kopa.
Ruge na kusaga walishiriki kikamilifu kuua mziki wa dansi tena kwa fitina za wazi, kama mradi wa kujiongezea kipato kibwanyenye.
Ruge alitoka USA na maono hayo.
Mziki ni kama chakula, unawalisha watu unachotaka tu hadi wanaamin ndo kitamu.
Pia kuliibuka saikolojia ya mziki mfupi dk 4 ndo upigwe radio na tv wakat kwa dansi unaua utam wote.
Pia gharama za kuendesha dansi kwa faida zikawa juu kuliko bongo fleva, ikampa standing point mfitini wa dansi.
Umarekan na uniga wa akina sugu, na prof j, nature, sele n.k nao ukachukua hatam.
Lakin ukiachilia mbali suala la gharama bado dansi ndo mziki kabsa kabsa kwa walio wengi. Bas tu, tunalishwa tunachopikiwa bila menu!
Ndo maana likipigwa sebene hata nikki wa pili atajitingisha tu!
 
Kasema wapi? Jiulize kama huyo Hidaya alikuwa Arusha why kwenye wimbo amtafute iwapo alimuona Moro au Arusha, au Mwanza. Ilitengenezwa tu na wabongo.
Acha ubishi mzee mwenyeji wa Arusha wote hakuna asie mjua Hidaya tena alikua maarufu kwa jina la Hidaya Wa pepe kale kafariki mwaka jana , Hidaya ni miongon mwa wanawake matajiri wa Arusha enzi hizo, ameishi pia france ninavyo kueleza kafariki mwaka jana elewa hivyo
Alafu mi nazungumzia wimbo wa pepe kale Hidaya hiyo ya kwako ya Hedaya mimi siijui
 
Back
Top Bottom