Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Ni neno moja tu Hidaya na hedaya. Labda tusaidie huyo mtoto amezaa naye mwaka gani ili upewe full kisa ndipo ujue wabongo wanajua kuchangamkia fursa. Sikatai kwamba huyo Hidaya wa Pepe Kale kama mnavyomuita alikuwepo, ila kilichoimbwa kwenye wimbo sio Hidaya mwanamke. Ila wabongo kwa kuchangamkia fursa mko vizuri. Stori ndefu kidogo na muda hautoshi.
 
Kuna yule fundi wa makabureta haha
Naye alikuwa anapaishwa

Ova
Nadhan Hussein makabureta unamsema alianzia magomen wasanii walikuwa wanapeleka magar yao kwake enz hizo kutokana na kaz yake na kupenda ukitonga kwa wasanii wakaanza kumrusha kwenye nyimbo zao

Kuna car wash maarufu pale sinza kwa jina la MAN CITY CAR WASH Napo wasanii Kama akina Christian Bella huenda kuosha magari yao hapo Kuna wimbo kaitaja car wash hi i nadhan ule wimbo wa Rudi
 
Papa msofe alikuwa sana salamander samora,alianzaga enzi zile za bandika
Bandua port
Hi michezo vijana wengi enzi zile walifanya na connection zote zilikuwa zinatoka kwa wafanyakazi wa hizo taasisi..kama tra,uhamiaji,ttcl nk
Wao ndy walikuwa wanawaletea watoto wa mjini wafanye alafu wao wanakula mgao....wao

Ova
 
 
 
Soma huo uzi jamaa amekuquote hapo juu utamjua vizuri huyo Hidaya
 
Yupo masasi choka mbaya
 
Ni kweli mkuu, miaka ya 90 na mwanzo wa miaka ya 2000 muziki wa Congo ulisumbua sana. Shukrani za pekee ni kwa Mulumba Kashama na bendi yake kipindi hicho akighani "mwenge mwenge daladala shilingi mia... " na kibinda nkoi yake, iliwaamsha akina Banza stone na Ali Choki (kisa cha mpemba) kuja na muziki wa dansi wa kizazi kipya.
Nao Clouds Fm wakaifufua taarabu iliyo kuwa imezimia... Kwa mbaali unakasikia kakionjo ka Onyango "wewe mambo iko huku... " huku kamsemo ka "taarabu imo humo?" kakivuma kuchagiza utamu wa taarabu.
Nashindwa kuisahau siku niliyo tembea kwa mguu kutoka Msasani club hadi Temeke mwisho, huku tukiimba wimbo wa Profesa Jay,kwa mara ya kwanza amepafomu pale beach, muandaaji Taji Liundi.
Miaka imeenda sana.
 
Hawa wote waliimbwa na akina Nyoshi, Patcho Mwamba, Bela baada ya kutupiwa buku 10 wanapokuwa stejini si unajua njaa za wakongoman ,na wote hao waliotajwa wengi wao walikuwa matapeli enzi za mzee wa Msoga, huyu Ali Kileo alikuwa mwajiriwa wa uhamiaji na ndie alikuwa msemaji wa idara ya uhamiaji nadhani alipigwa chini baada ya kulewa sifa na kuwa na ukwasi ambao haukuwa unalingana na ajira yake.
 
Enzi hizo hawa ndo walishika pesa za kufadhili mtandao... Amos alikua ukipiga simu moja tu umejaa. Now umri umeenda tu...bado yupo njema.
Bado kijana sana ila noti zilimtembelea haraka. Salome alikuwa nyodo sana pia
 
kulikua na wadau wengine sio mapedeshee lakini walipaishwa sana.

Chesco mzee wa matunda.
mama Mingoi.
Meja matunda.
Hassan Miundombinu R.I.P.
Swetu Fundikila R.I.P.
daladala camp.

mrangi ngoja niwa tag wakali wa donta.


mziki wa dansi ulikuwa na mambo matatu

kwanza kulikuwa na mapedeshee hawa watuzaji
ndio hao aliowataja mtoa mada

halafu kulikuwa na mashabiki damu
kama hapo unemtaja
MAMA MINGOI CHESCO MAZEE WA MATUNDA kuna pia Kina MANKA MUSHI
ambao ndo waliikuwa navijiwe vyao au CAMP zao
karanga camp
HOME ALONE
VINGUNGUTI TIMBERLAND
DALADALA CAMP
SWAZI INTER
n CAMP nyingine nyingi sana
ambazo hizo CAMP zina mashabiki haswa na mapedeshee wajanjawajanja ndo zilikiwa maskani zao na watoto wa mjini na wakati mwingine hata wanamuziki wenyewe pia huweka vijiwe katika hizo CAMP
hizo CAMP kulikuwa na mashabiki WAZARENDO
nakumbuka kuna SHABIKI MMOJA wa VINGUNGUTI TIMBERLAND huyo Mdau alikuwa anaipenda sana TWANGA kiasi alikuwa mpk anapanda NDEGE kuifuata TWANGA ikiwa NJE ya MKOA haswa ARUSHA au MWANZA

halafu kundi Jingine sasa ni la wanaofanikisha BENDI kuwa na Mziki bora

mfano HUSSEIN MIUNDOMBINU
huyu alikuwa fundi mitambo(umeme)
Twanga popote itakapopiga huyu alikuwa anahakikisha mambo yote ya umeme yako sawa mziki unatoka vizuri

THABITI MTOTO ILALA huyu alikuwa mkali wa kucheza na Keyboad

lakini pia kulikuwa na mkali mwingine wa KEYBOAD
ukisikia PROFESHENARI TARIBONARI VIctor mkambi huyu mkali wa KEYBOAD hata kama akifa inapaswa TWANGA wamjengee Sanamu lake maana alikuwa PROFESHENO haswa kaipaisha sana twanaga na UFUNDI wake wa KEYBOAD


Ukisikia MCD basi hapo anatajwa SUDI MOHAMED TIMBO(marehemu)
huyu alikuwa mpiga tumba matata sana

halafu ukisikia SHAKASHAKA SHAKUZURU hapa alikuwa anapaishwa MIRAJI SHAKASHIA huyu ni mpiga gitaa matata sana

halafu kulikuwa kulikuwa na mkung'uta DRUM hatari sana BABA DIANA BABAA SHARIFA BABAA ZAITUNI basi alikuuwa anatwaja ABUU SEMHANDO mpiga DRUM hatari

sasa utakuj kugundua kulikuwa na makundi matatu yalikuwa yanatwaja sana kwenye nyimbo ndio hao mapedeshee
wngine walikuwa mashabiki damu wa dansi
wengine ndio hao wenyewe wa wanamuziki
 
Wakati Mustahiki Meya wa Jiji Allan Mulumba Kashama anatuchezesha Dar es salaam kibinda nkoyi ndani ya Silent in Mwenge ulikuwa darasa la ngapi?

Unamjuwa Joseph Rwegasira?
Mzee wa Rwegasira alikuwa muumini wa Mlima wa Moto baada ya ikibinda nkoi kufa kifo cha mende, unawakumbuka akina Jesus Ibonga, binti wa Lovy Longomba akitwa jinala stage Sungura, Elyston Angai na wengineo wengi,Mwenge ilikuwa inasimama ikfika Jumamosi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…