Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Majutoo heee toa helaa hee,hee[emoji444] [emoji444][emoji444]
Majutoo hee toa helaa hee,hee[emoji444][emoji444]
Pedeshee Majuto.
ila wanamuziki wa kicongo wanajua kupaisha na kiwasifia mapedeshee lazima pedeshee atoe heraaaaaa jukwaani.
 
Hayo mengine sawa, ila kuhusu kukosa umaarufu kwa mziki wa dansi napingana na wewe.

Mziki wa dansi ulikuja kukosa umaarufu baada ya kuvuma kwa bongo fleva kuanzia miaka ya 2010 hivi.

Kabla ya mwaka 2010 ilikuwa ni nusu kwa nusu, yaani mziki wa dansi na bongo fleva ulikuwa unachuana katika mashabiki.

Chuma kimeingia ikulu 2015 huku mziki wa dansi ukiwa hoi bin taabani.

Hilo ni suala la kawaida katika fasihi. Nafikiri tunakumbuka kuna kipindi miaka ya 2000 hivi taarabu ilikuwa juu kuliko bongo fleva, enzi za Hadija Kopa na yule mama sijui alikuwa naitwa nani mpinzani wa kopa.
Khadija Kopa vs Nasma Kadogo.
 
Maisha Kitendawili, Dr Rama, Abdala Nyumba nyingi, Bitebo saloon, Songolo, Haji mbabe mwanamanyema, somebody Miundombinu, utajiju Camp, Daladala camp, Andrew Trader, Side Mkuluma,Freedom Camp, Salumu na Merelani, Home alone camp, Salum masim, Chikago matelephone nk
 
Huyo Abdul Mteketa alikuwa Mbunge wa Kilombero,Mkoani Morogoro na Sasa ni marehemu baada ya kuugua sana na mwisho wake aliishiwa mpaka alikosa pesa ya matibabu pale Muhimbili na kuomba msaada kwa mh.hayati JPM,

Huyo Charles Mtawali ni tajiri mmoja hivi aliwika na mpaka sasa nafikiri yuko na pesa maana alikuwa anaishi Kinondoni Stereo aliwahi kununua mtaa mzima pale,na mle ndani kwake parking ukiingia ilikuwa Kama yard magari ya kifahari akirudi ama mkewe akirudi ilikuwa hatumii gari ile ambayo amerudi nayo anatoka na nyingine.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
Abdul Mteketa ni kweli alifariki mkuu. Mara ya mwisho 2015 aligombea ubunge lakini hakupata nafikiri hilo pia lilichangia kuwa na mawazo maana alikuwa na rafiki yake naye maarufu Said Ntimizi walikuwa na kesi nyingi za madai.
 
Alikuwa Nasma Hamis,nadhani alikuwa Muungano
Zamani mziki ulikuwa zamu kwa zamu, Kuna muda Taarabu ilishika Kasi balaa, Kuna muda miduara ilibamba kinoma, Kuna wakati bongofleva zilikamata kisawasawa, Kuna muda muziki wa dansi asili ya Kongo ulikamata nchi nzima, Ila Kuna kipindi muziki wa dansi wa msondo na sikinde ilishika nchi ikatikisika Sana, Hasa kipindi kile msondo waliposhusha Kilio Cha mtu mzima utunzi wake John Jambele msondo ulikuwa Moto Sana. Chenja alitajwa Sana msondo Hadi wakamuimbia wimbo. Zamani ulikuwa balaa na nusu
 
Nadhani hizi FM station kidogo zilishindwa ku promote muziki wa dance.

Mussa mzee wa korosho huyu ndio babake na Jux mwimbaji. Huyu maarehemu

Dr Ayoub siki hizi nadhani ni Profesa Ayoub wa magonjwa ya akili

Pedeshee Ndama Mtoto wa Ngombe aka Akayesu huyu bado tajiri sana

Papa musofe chuma cha reli mbongo wa kwanza mjanja kuvaa pure gold nyingi mkimya kwa haiba lakini ana akili za kimafia za hela hatari. Huyu kuna sehemu akifika na gari hashuki hapendi macho ya watu sana.

Papa Davis Mwangaba mzee wa Temeke huyu alikuwa anatembea na millioni kadhaa kwemye buti la gari. Kaka yake ndio mwenye mbumba ya hatari mzee Mwangaba tajiri wa Temeke

Papa Muddy mas mzungu wa roho kawasafirisha washikaji kibao kwenda ulaya waliokuwa wana hustle town na hawakuwa na uwezo wa safari kwenda kujilipua ulaya

Wazee wa TCC kuna mwamba mmoja walikuwa wanamuita Abrahamovich naye alikuwa na mbumba za kusumbua kiumeni TMK area.
 
Manka Mushi aliimbwa na mwinjuma Mumini Sana,jamaa Kuna wimbo anamtaja hata Mara tatu
Namfahamu....mara ya mwisho kuonana nae 2016 kama sikosei mileage imesoma si kitoto..
Anapiga tu bia maeneo ya equator grill hapo...
Nilikutana nae enzi bado sielewi elewi..yeye ananiambia unamjua manka mushi aliyeimbwa ndo mimi yaani

Hahaha huyo dada aisee michongo mingi kinoma
 
Namfahamu....mara ya mwisho kuonana nae 2016 kama sikosei mileage imesoma si kitoto..
Anapiga tu bia maeneo ya equator grill hapo...
Nilikutana nae enzi bado sielewi elewi..yeye ananiambia unamjua manka mushi aliyeimbwa ndo mimi yaani

Hahaha huyo dada aisee michongo mingi kinoma
Kumbe, lazima azeeke aise maana wakati anaimbwa Ni Miaka ya 2004 huko
Alikuwa naye Ni pedeshee au aliwapa msaaada gani Hawa wanamuziki Hadi aimbwe Sana?
 
Kumbe,lazima azeeke aise maana wakati anaimbwa Ni Miaka ya 2004 huko
Alikuwa naye Ni pedeshee au aliwapa msaaada gani Hawa wanamuziki Hadi aimbwe Sana ?
Manka mushi alikuwa ni shabiki tu wa mziki wa dansi. alitokea kuupenda mziki kiasi kila band zilipokuwa zinatuambuiza kwenye kumbi za dar, yeye alikuwa anahudhuria. na alikuwa anaingia bure kwasababu tayari alishakuwa mdau.

Hii ikamfanya kuwa karibu na baadhi ya wanamuziki hususani Mwinyjuma muumini wakati ule akiwa na tamtam band.
 
Back
Top Bottom