Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Hayo mengine sawa, ila kuhusu kukosa umaarufu kwa mziki wa dansi napingana na wewe.

Mziki wa dansi ulikuja kukosa umaarufu baada ya kuvuma kwa bongo fleva kuanzia miaka ya 2010 hivi.

Kabla ya mwaka 2010 ilikuwa ni nusu kwa nusu, yaani mziki wa dansi na bongo fleva ulikuwa unachuana katika mashabiki.

Chuma kimeingia ikulu 2015 huku mziki wa dansi ukiwa hoi bin taabani.

Hilo ni suala la kawaida katika fasihi. Nafikiri tunakumbuka kuna kipindi miaka ya 2000 hivi taarabu ilikuwa juu kuliko bongo fleva, enzi za Hadija Kopa na yule mama sijui alikuwa naitwa nani mpinzani wa kopa.
Nasma Hamisi, alishavuta
 
Umemsahau papaa misifa,, diamond alikuwa anamtaja sana enzi hizo sasa nae kawa na hela hawataji tena kwenye nyimbo zake anawataja ndugu zake na wafanyakazi wake tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]dah maisha haya
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
umenikumbusha late 90s nimemaliza O-Level, nipo home idol nasubiri majibu yatoke. mshua akanitafutia temporary job mitaa ya mjini posta kwenye ofisi ya rafiki yake.

ofisi ilikuwa mtaa wa jamhuri jirani na ile round about ambayo inakutanisha india street na mkwepu street, almaarufu mitaa ya azam take away.

ilikuwa kila ikifika mida ya saa tatu mpaka saa nne asubuhi, lile eneo walikuwa wanatokea mabroo smart kwelikweli kimuonekano. mkononi wamebeba vi-diary.

walikuwa wanavaa mashati nadhifu, surauli za kadeti na viatu safi vya ngozi. kwa ujumla walikuwa wanapendeza sana, mimi mwenyewe nilikuwa nawa admire.

siku moja nikamuuliza broo mmoja ambaye tulikuwa tunafanya kazi pale, kwamba hawa jamaa ni akina nani,mbona mda mwingi wanautumia kakaa kwenye vijiwe vya shoe shiners, hawana kazi ya kufanya?.

akanijibu ukisikia mission town ndio hao, na hapo kwenye vijiwe vya shoeshiners ndio sehemu zao za kupanga mipango na kupeana deals mbalimbali.

akaniambia kile kipande chote cha mtaa wa mkwepu kinachokatiza club ya billicanas mpaka kule kwenye maungio ya samora avenue, ni territory ya ma-mission town.

hata papaa msofe alianza kujifunzia upigaji mitaa hiyo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pisi kali kuna yule aliyeimbwa sana na Fali Ipupa alipokuja Dar kwa mara ya kwanza Yasmine
Jasmine alikuwa full package mguu mjazo. Ule mguu lazma hakuwa mchaga!
Lakin ile show aliyekuwa hot girl ni Mboni! Hata fally alicheza nae kwa hisia na adabu za matamanio na kale ka suti ka kung'aa bei mbaya kitovu nje km halagi chips!
Mboni popote ulipo pole. huwez kurudsha nyuma saa!
Nadhan watu maarufu wanaotoaga vitabu vya maisha yao, mboni atatusimuliaga walifanya nini na Fally thereafter!
 
awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. itabidi msome kimya kimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity liwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

mwaka 2002 mpaka 2012, mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

kwa uchache tu, band zilizotamba ni fm academia, akudo impact, twanga pepeta na diamond musica. zingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

umuarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.
kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa john young millionaire muzee ya range rover[emoji3][emoji3].

haya twende kazi:
Pedeshee Mychoisi na Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko mbeya, watu wa mbeya mtatusaidia.

Braza K na Tunduma:
watu wa tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya mikocheni barabara ya rose garden. those days she was very pretty. kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnana:
bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV. baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za catering. shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana.sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. fm academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
alikuwa mmiliki wa band ya daimond musica kwa kuwezeshwa na mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages. watu wa zamani wanaelewa. juddy alikuwa mrembo si kitoto. kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
sina haja ya kumuelezea , ni mtu maarufu wa nyakati zote. wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Billgate Muzamil Katunzi:
Christian bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la muzamir katunzi. i don't know him personally, but it's told he was financially very successful.

Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa papaa msofe. itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana. halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
ni marehemu kwa sasa. huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya Fm Academia. nilikuwa namfahamu personally.licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer ktk Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi mpya za gari mtaa wa agrey kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiriwa kwa jina la general supply. ktk biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

pedeshee David Kabunga:
sifahamu alikuwa ni nani. jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Papaa Ali Kileo:
he was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe Big Boss:
anafahamika vizuri. jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero:
kwa sasa ni RC wa dar. jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: anafahamika vizuri, wajanja wa wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk mkoa wa morogoro. sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za lumumba.

Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba Kali...
?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Ntenze wa Ntenze....?
Me nikafikri utawaja akina Cheusi Magala, Mayasa, Abas Gulamali wale wa zamani kweli kweli!
 
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
?/
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba Kali...
?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Ntenze wa Ntenze....?
Rais wa sinza alikutwa na kesi ya ujambazi na kufungwa,naskia katoka
 
Charles Mtawali nimemfahamu toka 2002 alikuwa anafanya biashara na bro wangu muuza spare used ni mmoja wa waanzilishi wa mwanzo mwanzo kabisa wa yards za magari barabara ya Kawawa show room yake ilikuwa pale Morocco alikuwa mtu mmoja peace sana nahisi mpaka sasa ipo.

Kipindi hiko ukiingia show room hakuna cha kusema niagizie sijui Subaru sijui Mazda hiyo itafika mwakani ulikuwa unakutana na machaguo kadhaa tu either uchukue MarkII Grand Kisu,MarkII Mayai au Chaser Avante single glass or double glass (Balloon bado hazijafika bongo),Corolla Limited au Corona ST 150 hizi ni gari za 80/90s huko ukitaka SUV uchukue Suzuki Vitara 5 doors au Land Cruiser Prado II au VX ya Mrema ambazo ni gari walikuwa wananunua wachache kutokana na ukubwa wa bei.

Said Mukuu wa Lumumba na Omar Tolu hawa nao niliwahi kuwaona walikuwa wauza magari na wapokea bond wa magari wadau wakikwama mpunga town maskani yao ilikuwa pale Lumumba wanaowajua waliowahi kufanya nao kazi wanasema hawa jamaa hata urudishe mkopo wote ibaki laki hiyo hela huipati mpaka siku mkataba wenu unaisha na gari wanachukua.

Salum Chicago yeye alikuwa na show room yake town pale ilipo clock tower round about ya kwanza ukitoka Mnazi Mmoja kuelekea town mkewe wakati wa Kikwete aliukwaa ubunge viti maalumu,huyu mkewe alikuwa na scandal ya kutembea na driver wao jamaa mmoja akiitwa Mwinyi muhuni wa Manzese Chicago akamfukuza kazi,waya ulimchukua huyu dereva kwenye mwaka 2015/16.
Salum alikua na duka la nguo kariakoo kabla hajawa maarufu,kuna ndgu yng alikua na duka jirani na mama yake salum...sijui siku hizi yuko wapi
 
Kizaizai alikuwa na yard ya magari ya uzushi mitaa ya shopper's...
Mwenye eneo alikuwa na mpango wa kuliuza,kila akimwambia Anunue eneo ni blhblh tu
Mwisho wa siku wakaja watu wenye pesa wakamtoa hapo kabakia kungaamacho tu

Ova
Nlifanya nae biashara ya range rover ya ndgu yangu akanidhulumu...mwisho wa siku gari ikashindikana kusajiliwa wakatema hela
 
Hawa walianza ujanja tu toka zamani
Alipotoka bukoba alipokelewa na ndg
Yake,akamuwekaga kwenye duka la dawa kino studio
Alijua mambo ya mjinimjini
Msofe naye wote walianzia salamander mjini...mambo ya mihuri,pport etc
Huko ndiko walijua michongo mingine
Kwa mtoto wa mjini zamani lazima uende salamander,azam kutega ujue na kupata a,b,c,d
Nashanga sahv mtoto wa mjini anaonekana na kutambulika
Kisa anaenda kidimbwi
Mtoto wa mjini maana yake huko mjini
Unakutana na watu,viongozi wanakupata connection au wanakupa mchongo kwa kukutumia wewwe nk
Siku mtu kwenda Juliana kidimbwi
Anaonekana umjini

Ova
Salamander unakuta watu wako smart utafikiria afisa wa ubalozi,mchana unawakuta post club wako na warembo wanakula na kunywa...pia kulikua na kijiwe kingine cha azam round about nyuma ya benjamin mkapa tower posta
 
Hawa wote waliimbwa na akina Nyoshi, Patcho Mwamba, Bela baada ya kutupiwa buku 10 wanapokuwa stejini si unajua njaa za wakongoman ,na wote hao waliotajwa wengi wao walikuwa matapeli enzi za mzee wa Msoga, huyu Ali Kileo alikuwa mwajiriwa wa uhamiaji na ndie alikuwa msemaji wa idara ya uhamiaji nadhani alipigwa chini baada ya kulewa sifa na kuwa na ukwasi ambao haukuwa unalingana na ajira yake.
Ilikuwa enzi za mkapa
 
Kuna pedeshee Ndunguru na pedeshee Ndomba wa Makongo. Nteze wa Nteze mzee wa kifusi.... dah old good days. Kuna siku niko pale makumbusho, Papaa Msofe akanunua bia kwa kila mtu aliyekuwepo mle ndani nilichoka sana, anakujua hakujui unapewa bia [emoji28]
wangoni wenzangu hao...[emoji3][emoji3]
 
Kuna siku tuko new msasani club
Kwenye buzuki,wakongi kubao
Ali kileo alilileta karandinga
Pale ebwana watu walitafutana mule
Wakongo walitoka mbiooo
Alikuwa anajua kutengeneza mazingira,sema alikuja zinguaga wakamtupa kusini huko ndy kupotea
[emoji1]
Mara ya mwisho nlionana naye mtwara....muda sana nlikuwa naekea msumbj(sidadi)akawa anasema nyie watoto wa kjnondoni janjajanja sana
Mazabe tu,hatukutaka kuuweka sana kwake aside akatugeuza dili [emoji1]

Ova
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom