Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

michongo yote ambayo hawa mapedeshe na wajanja wa mujini wa zamani walikuwa wanapiga ilikuwa inafahamika vizuri tu na vijana wa Tiss.

shida ni kwamba kwa utawala ule wa JK ilikuwa hakuna mtu wa kumfunga paka kengele kwasababu the whole system was corrupt.

halafu hawa mapedeshee kwa kugundua weakness hiyo, wakajipenyeza mpaka kwa wakubwa wa hao vijana wa Tiss na jeshi la polisi. wakipiga madeal yao, mgao ulikuwa unaenda kwa wakubwa.

kwa mfano afande alfred tibaigana wakati huo akiwa RPC wa dar es salaam, alifaidika sana na matukio ya upigaji ya papaa msofe.

kuna kisa kimoja niliwahi kusimuliwa, msofe aliwapiga waisrael mamilioni fedha baada ya kuwauzia almas fake.

wale waisrael walihangaika sana kutafuta haki yao. hilo suala lilipofika mezani kwa tibaigana likafia hapo. jamaa wakarudi kwao kichwa chini.
Inasemekana ni mke wa waziri mkuu wa Israel yule aliyekuwa kwenye koma mda mrefu ndio aliingizwa mjini
Kutokana na wao kuja kimagumashi msala ukawa hauna nguvu sana kwa kuchafua reputation ya nchii

Pia kuna wakili mmoja ndio alikuwa nyuma ya kina msofe ku endooze stamp na signature
Currently huyu wakili alisha rudisha namba kwa sir GOd
 
Kuna mtu alikuwa anaitwa Juma Ngida huyu alikuwa mtoto wa mjini kweli kweli na hela ilikuwepo...huyu ndio mtu wa kwanza kuingiza hizi gari Rav 4 mpya nchini ..kipindi mererani inaanza kuchimbwa jamaa akaanza safari akaenda kufika arusha wakamwambia mzee hiki kipindi cha mvua saa hivi barabara ya merelani gari hazipitiki kwa hizi gari za kifahari ujamaa pale pale akatoa mpunga akanunua land cruiser mpya impeleke ...yaan kama ananunua shati vile .ila amefariki kwa sasa aliimbwa mpaka na dudu baya kwenye nyimbo yake ya nidhamu mana jamaa ndio alikuwa anajiita don king minyamihela .
 
Acha ubishi mzee mwenyeji wa Arusha wote hakuna asie mjua Hidaya tena alikua maarufu kwa jina la Hidaya Wa pepe kale kafariki mwaka jana , Hidaya ni miongon mwa wanawake matajiri wa Arusha enzi hizo, ameishi pia france ninavyo kueleza kafariki mwaka jana elewa hivyo
Alafu mi nazungumzia wimbo wa pepe kale Hidaya hiyo ya kwako ya Hedaya mimi siijui
uko sahihi
images%20-%202022-06-28T062137.659.jpg
 
Nje ya mada kidogo: unakumbuka kipindi cha Radio Kenya - je, huu ni unungwana? Na lenadi mambo mbotela?
 

Attachments

  • IMG_5489.MOV
    13.5 MB
Nimekuelewa ila nimekurudisha nyuma kwanza ukumbuke rhumba lilianza kunoga enzi za Silent huku Mustahiki meya wa Jiji Allan Mulumba Kashama akirap kama Titinaa Alcapone au Robert Wunda Ekokota wa Wenge Musica Bcbg 4 × 4 kipindi hicho Wenge ndio wametowa nyimbo yao ya Kien Bunjee na Saplaisi Kapangala.
Titina hukuwahi kuwa rapper(atalaku) Bali ni alikuwa mpiga drums wa wenge kwenye kurap walikuwa Roberto wunda na tutu kaludji
 
Huu uzi mwandishi atakuwa na IQ nzuri.

Hapa JF unatakiwa upewe hata mji kama ile mitaa ya Nape.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:

Huyu brother wa umri wa akina papaa Msofe.

Ni wa Tunduma alikuwa mwajiriwa wa TRA na mke wake fundi cherehani.

Upapaa wake ni kama uliisha baada ya ajira ile kukomeshwa, umaarufu ulimponza.

Uzi mzuri sana huu.
Sasa hivi amechoka sana Mutarika...Yupo Masasi...Kapooza upande mmoja
 
Nadhan Hussein makabureta unamsema alianzia magomen wasanii walikuwa wanapeleka magar yao kwake enz hizo kutokana na kaz yake na kupenda ukitonga kwa wasanii wakaanza kumrusha kwenye nyimbo zao

Kuna car wash maarufu pale sinza kwa jina la MAN CITY CAR WASH Napo wasanii Kama akina Christian Bella huenda kuosha magari yao hapo Kuna wimbo kaitaja car wash hi i nadhan ule wimbo wa Rudi
Man city car wash na Africa sana 😂
 
Hao Wanamuziki wa Congo wote break yao kuna Don wa Ki Ivory coast anaishi Paris anaitwa Hemed Bakayoko, huyu ndio funga kazi, hii treasure.

Huyu ndio hakauki mdomoni mwa Boss ya Mboka Koffi Ollomide then ndio anakula shavu Samuel Etoo, hizi ni international level.
Hamedi bakayoko kafariki mwaka jana, ...jamaa alijiingiza kwenye siasa na alikuwa anaandaliwa kuwa Rais wa ivory cost
 
hivi ni kweli mboni alizaa na mcheza kandanda maarufu wa west africa, gorge weah/samwel eto?.

hizi habari zilikuwa zinazungumzwa sana miaka yetu ile.
Inasemekana ni Solomon kalou yule dogo m-ivory cost alikuwa akikipiga Chelsea enzi hizo akiwa na nduguye Didierdrogba
 
Ilikua mama moja pisi kali ya Arusha, pepe kalee alifichwa hadi akanyoosha mikono, nadhani bado yupo alikua na mtoto mmoja wa kike aliuliwa na mume wake walikua wakiishi UK
Nae pia aliefariki. Mungu amrehemu marehemu Hidaya
 
Back
Top Bottom