Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Huyo Ally Kitobo na mbwembwe zote hadi leo anapanga majuzi tu kidogo apigwe risasi mitaa ya Mbezi Beach alikwenda kumfanyia unyoko mzee mmoja wa mjini anaitwa Fadhil Mganga(walikuwa jela wote na Msofe). Kwa sasa Kitobo anaishi kama digidigi na hasa ukichukulia hana shule
Ally kitobo ndio yule anajifanya DJ au namfananisha....
 
Awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. Itabidi msome kimyakimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

Huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity stage iliwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

Mwaka 2002 mpaka 2012 mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

Kwa uchache tu, band zilizotamba ni FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Diamond Musica. Band nyingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

Umaarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

Majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

Kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

Nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

Naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.

Kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa John Young Millionaire Muzee ya ma-Range Rover[emoji3][emoji3].

Haya twende kazi:
Pedeshee Mychoice na kati ya Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko Mbeya, watu wa Mbeya mtatusaidia.

Braza K na kati ya Tunduma:
Watu wa Tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
Huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya Mikocheni barabara ya Rose Garden. Those days she was very pretty, kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnata Decoration:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za decoration and catering. shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
Alikuwa mmiliki wa band ya Daimond Musica kwa financial support ya mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages, watu wa zamani wanaelewa. Juddy alikuwa mrembo si kitoto, kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
Sina haja ya kumuelezea, ni mtu maarufu wa misimu yote. Wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. Jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Bill gate Muzamir Katunzi:
Christian Bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la Muzamir Katunzi. I don't know him personally, but it's told he was financially successful.

Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
Sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa Papaa Msofe. Itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. Walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
Ni marehemu kwa sasa, huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya FM Academia. Nilikuwa namfahamu personally. licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa Serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: Jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi za gari Mtaa wa Agrey Kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". Watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiliwa kwa jina la general supply. Katika biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
Najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

Pedeshee David Kabunga:
Sifahamu alikuwa ni nani, jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Papaa Ally Kileo:
He was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe le Big Boss:
Anafahamika vizuri, jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero, Babaa na Gabriele:
Kwa sasa ni RC wa Dar, jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: Anafahamika vizuri, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
Huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk Mkoa wa Morogoro, sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
Binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
Jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za Lumumba.

Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba...?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Nteze wa Nteze....?
John Nzenze....?
Papaa Madenge....?
Muddy Nyambi....?
Jimmy Chokolete....?


Note of Appreciation
.
sikufikiria kama huu uzi ungepata wafuatiliaji wengi kiasi hiki. niwashukuru wote mnaoufatilia na mnaochangia maoni yenu. asanteni sana wadau.[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]
Enzi zetu ilikuwa Kama ifuatavyo,
Mwanyiro- Computer
Shabaan Dede
Mulenga
Kalasya
John Mwakangale
John jambele
Na wengine wengiiiii enzi zetu za RTD enzi za Kavasha wapi raise on na bugaloo huku afro kichwani na mafuta ya Yu yakinukia au headphone kubwa Kama rubani na viredio vidogo viliitwa walkman
 
Enzi zetu ilikuwa Kama ifuatavyo,
Mwanyiro- Computer
Shabaan Dede
Mulenga
Kalasya
John Mwakangale
John jambele
Na wengine wengiiiii enzi zetu za RTD enzi za Kavasha wapi raise on na bugaloo huku afro kichwani na mafuta ya Yu yakinukia au headphone kubwa Kama rubani na viredio vidogo viliitwa walkman
safi sana kyambamasimbi.
 
Nimekulia Sinza ile ya akina Remi ndio wanatamba na Volkswagen imeandikwa.''mambo kwa soksi'' tulikuwa tunajua karibu vijana wote, hivi sasa Sinza imebadirika ni Sinza ya magorofa,mahoteli,vijana wote wa zamani ama wamerudisha namba kwa Sir God ama wamehamia sehemu nyingine nje ya mji,nyumba nyingi tulizokuwa tunapanga chumba kimoja kimoja zimebomolewa na kujengwa mahekalu, nakumbuka pale sinza madukani kulikuwa na mbabe wa kikurya Lucky baba yake alikuwa usalama wa Taifa,namkubuka bibi Uliye alikuwa na mabinti kama 10 hatari sana, nakumbuka akina Banza stone wakiwa wadogo wakicheza disco mtaani, nakumbuka Vatican City ikiwa hotel kumbwa Sinza na Simba walikuwa wakiweka kambi hapo, namkumbuka Fred Mwalasha akiwa ametoka Ulaya na mke wa kizungu ikawa yeye ni bangi na bangi na yeye hadi mwanamke wa kizungu akamkimbia, siku hizi sinza yamejaa madangulo na wazee wale waliokuwa na nyumba ambazo tulikuwa tumepanga nao hatunao duniani ila zile nyumba walizoacha watoto wao wameziuza kwa matajiri na kwenda kunywea pombe na kula sembe. Sinza ya sasa si ile tuliyokuwa tunaitimba, ama kweli siku hazigandi.
Kweli Sinza imebadilika. Nimekulia Makaburini, jirani na kwa L. Tenga na J. Ikangaa! Tenga pesa anayo toka enzi hiyo. Jamaa alikuwa akinunua gari mpya. Nakumbuka alinunua hizi Premio mpya miaka ya 1990! Alinunua Range Rover 2nd generation kutoka CMC!

Sinza Kumekucha kulikuwa na video library ya kuazima latest movies kwa membership!
 
Ilikuwa enzi za JK zile Msofe alikaa sana Keko hadi akawa mweusi.. Mzee Massawe alikimbilia ughaibuni sijui kama amerudi..mwisho wa siku Msofe aliachia ile nyumba plus na riba na usumbufu kwa mjane.Ile nyumba ipo mitaa ya Mikocheni.
Sawa kabisa .Mke wa Marehem walimrudishia Nyumba Wakampa na Hela ya kutosha pamoja na Prado moja
 
Kweli Sinza imebadilika. Nimekulia Makaburini, jirani na kwa L. Tenga na J. Ikangaa! Tenga pesa anayo toka enzi hiyo. Jamaa alikuwa akinunua gari mpya. Nakumbuka alinunua hizi Premio mpya miaka ya 1990! Alinunua Range Rover 2nd generation kutoka CMC!

Sinza Kumekucha kulikuwa na video library ya kuazima latest movies kwa membership!

hiyo video library sio ile ilikuwa inamilikiwa na nteze john?...mchezaji wa zamani wa club za tz.
 

watoto wa mjini bila shaka mnamkumbuka vizuri huyu brother. alikuwa anashinda sana mitaa ya somora. pia walikuwa na duka lao la nguo jirani na jm mall.

ni msiba uliogusa hisia za wengi hususani watoto wa mjini wa ile generation iliyosumbua sana mitaa ya samora avenue,mkwepu street na lumumba.
copy to mrangi and others.
View attachment 2363142
Dah! Huyu bro, nafikiri ndiyo kati ya wabongo wa kwanza kuchapisha majina kwenye soccer jerseys. RIP Moody Mas mzee wa pamba kali original!
 
Hayo mengine sawa, ila kuhusu kukosa umaarufu kwa mziki wa dansi napingana na wewe.

Mziki wa dansi ulikuja kukosa umaarufu baada ya kuvuma kwa bongo fleva kuanzia miaka ya 2010 hivi.

Kabla ya mwaka 2010 ilikuwa ni nusu kwa nusu, yaani mziki wa dansi na bongo fleva ulikuwa unachuana katika mashabiki.

Chuma kimeingia ikulu 2015 huku mziki wa dansi ukiwa hoi bin taabani.

Hilo ni suala la kawaida katika fasihi. Nafikiri tunakumbuka kuna kipindi miaka ya 2000 hivi taarabu ilikuwa juu kuliko bongo fleva, enzi za Hadija Kopa na yule mama sijui alikuwa naitwa nani mpinzani wa kopa.
Nasma hamis kidogo
 
Back
Top Bottom