Tuwaheshimu hawa wanawake wanaozungusha biashara mtaani

Tuwaheshimu hawa wanawake wanaozungusha biashara mtaani

Hao wanawake wenyewe wakifika wanakuuzia ndizi kwa maneno ya hisia hisia tupu
Kifupi wao na wateja wao wanajuana
Ni mwendo wa mizaha mizaha hadi mwisho
 
Ila wengine nao hawajiheshimu,unakuta wanafanya biashara kama zuga tu ila kuna biashara nyingine nyuma ya pazia ya kujiuza ndio inayofanyika
 
Hii tabia imeota mizizi kuna baadhi ya wanaume wameshaona kawaida kuwashika wanawake wanaowahudumia, wewe mwanaume kabla hujafanya hicho kitendo jiulize huyo mwanamke unaemshika angekuwa mkeo au mama yako au dada yako ndo anafanyiwa kitendo kama hicho ungefurahi?
Wanaume jaribuni kuwa na heshima na nidhamu kwa wanawake wanaoamua kujitajifutia rizki zao bila kutweza utu wao.
Ni washenzi sana
 
"Shambulio la aibu" wazee msiingie kwenye huo mtego.

Serikali imewapendelea sana wanawake kwenye sheria. Unaweza ukakaa ndani miaka zaidi ya kumi kwa kifungu hicho tu.
 
Wanawauliza, "hilo beseni lote ni bei gani?"
Jibu litakuwa, "shilingi elfu ishirini".

Ataambiwa, "nanunua lote halafu twende lodge".
Anajibu, "sawa ila utaongeza elfu kumi".

Siku inaishia hapo!
 
Kuna demu Pic kali hatari..age ni ya hivi vibinti vya afu mbili inauza uji kuanzia saa 10 jioni pale ferry...

Vijana wanakunywa uji bila kukusudia.
 
Mi nikiona mwanamke anafanyiwa hivyo huwa na react kumkemea mwanaume anayemfanyia mwanamke hivyo, si vizuri, wengine ni wake za watu. Hata migahawani sipendi wanawake wafanyiwe hivyo. Ni bora umuulize kwa heshima kama ameolewa au la kama unamtaka awe mke wako approach kwa heshima
 
Kuna wanawake na mabinti wanazunguka mtaani hasa maeeneo yenye shughuri za kazi mbalimbali kama masoko,workshop,gerejeji nk wakiuza hasa matunda .

Kunatabia ambayo imeota mizizi naweza kusema ni sawa na kidharirisha utu wao.

Anaitwa apeleke matunda katika kundi la wanaume ktk sehemu hiyo,wananunua ndio lakini unakuta mwanaume mmoja mara ashike titi mwingine tako,mwinge mbavu,mwinge began kwa nyakati tofauti tofauti.

Huu ni upuuzi,hao wanawake wapo kujitafutia ridhiki kwa njia halali nu kazi kama kazi nyingine waheshimiwe msi take advantages kipuuzi kutweza utu wao.

Hao wana wake si kwamba wapo tu wengi wanafamilia zao na waume zao,waheshimuni.

Si kwamba wanapenda kufanyiwa hivyo ni kwa sababu hawana jinsi na wanachukulia kama ni changamoto Mei-take advantage,wangetaka kufanyiwa hivyo basi wangekuja kivingine.

Nimeshuhudia maeneo tofauti hii tabia mara kenda hasa buguruni wanapouza mbao na gereji nikienda service ya baby walker yangu.

NINA ICHUKIA HII TABIA.
Umeandika jambo jema kwa kuliangalia juujuu, kiundani fanya uchunguzi wa kina kwa wauza soseji na sambusa kwenye mabaa na sehemu za starehe, nimani yangu utapata majibu tofauti,maana wengi wao ni kama wanajiuza na hizo biashara unazoziona wanafanya ni kama kisingizio tu.
 
Hao wanawake wenyewe wakifika wanakuuzia ndizi kwa maneno ya hisia hisia tupu
Kifupi wao na wateja wao wanajuana
Ni mwendo wa mizaha mizaha hadi mwisho
Sasa unataka aongee kama mandonga?,ile ni biashara mteja hawezi ongeleqa kwalugha mbovu,maneno yake sio sababu
Umeandika jambo jema kwa kuliangalia juujuu, kiundani fanya uchunguzi wa kina kwa wauza soseji na sambusa kwenye mabaa na sehemu za starehe, nimani yangu utapata majibu tofauti,maana wengi wao ni kama wanajiuza na hizo biashara unazoziona wanafanya ni kama kisingizio tu.
Kwenye baa nimeyaona sana na wengine wanauza mayai ya kuchemsha kakini hawa wa mitaani wengi sio willingly
 
Mi nikiona mwanamke anafanyiwa hivyo huwa na react kumkemea mwanaume anayemfanyia mwanamke hivyo, si vizuri, wengine ni wake za watu. Hata migahawani sipendi wanawake wafanyiwe hivyo. Ni bora umuulize kwa heshima kama ameolewa au la kama unamtaka awe mke wako approach kwa heshima
Hiyo heshima hawana,,wanajiona miamba
 
Wanawauliza, "hilo beseni lote ni bei gani?"
Jibu litakuwa, "shilingi elfu ishirini".

Ataambiwa, "nanunua lote halafu twende lodge".
Anajibu, "sawa ila utaongeza elfu kumi".

Siku inaishia hapo!
Hapo siwamekubaliana?,ninacho kataa nikuanza kushika viungo bila Richaaa yake
 
Back
Top Bottom