Tuwaheshimu wana JamiiForums ambao hawajawahi kupigwa ban

Tuwaheshimu wana JamiiForums ambao hawajawahi kupigwa ban

Oops !!
Nawaangalia Halafu Nasema Hii Bhaghosha Sana
By Mzilankende, Jiwe, Ngosha
 
Good Friday Kareem.

Dhumuni la uzi huu ni kuwatambua wenzetu ambao wamekuwa ni watiifu wa mila na desturi na tamaduni zilizowekwa na uongozi wa JamiiForums ili sisi sote tuufuate.

Mzee Mohamed Said amekuwa ni babu na baba bora wa jukwaa hili. Umsimange, umkebehi, umwite jina lolote baya au umkashifu kwa kashfa yoyote ile, atakuangalia, atakuelimisha, na akikuona ni kichwa ngumu atapita zake kando akuache na keyboard ⌨ yako.

Mzee huyu hajawahi kupewa adhabu yoyote, ila muda wote amekuwa akipokea zawadi za kuwa member bora zaidi hapa jukwaani.

Skylar, huyu ni mdada mwenye kichwa chake matata sana. Sio under dog ila ni underground member ambaye amekuwa akijificha kwenye majukwaa rahisi, na inapombidi huwa anaingia kwenye majukwaa magumu na kutema madini adhimu. Skylar hajawahi kuchezea ban.

Pascal Mayalla a.k.a MWANASHERIA msomi, mchambuzi wa kisiasa na mshauri na muonyesha njia wa taifa hili, bro wangu huyu ni miongoni mwa members wanaosakamwa na wakati mwingine kutukanwa matusi makubwa kabisa, lakini ana uvumilivu wa hali ya juu sana. Hekima anayoipata kutoka kwa yohana Mtebezi imemfanya awe very calm muda wote. Huyu braza ana ban moja


Mshana Jr, huyu ni member maarufu kuliko member mwingine yeyote, na pia amekuwa kioo kwa wengi hapa jukwaani. Tangu amejiunga, hajachezea mkasi wa ban.

Gwappo Mwakatobe, amekuwa mchangiaji wa muda mrefu na hajawahi kupatwa na hayo makitu.

Sky Eclat , mwanamama mwenye upeo wake, muhabarishaji ,muelimishaji na mchangamshajo. Kwake ban NO.

Wengine ni Nazjaz, Jemima Mrembo , Chakorii, ndyoko, Kipaji Halisi, Madame B na wengine wengi.

FaizaFoxy yeye kachezea sana ban enzi zile, na mwenzake Malaria Sugu alipigwa life ban.

Maisha ni mazuri sana aisee
Mbona hujanitaja au kuna siku umeona nikila ban
 
Ban nyingi hutoka kijinga tu,Kuna fala aliniripoti nikala ban kisa kumuuliza 'wewe siyo Fulani!?..sikusema yeye ni Fulani,aliniripoti nikala ban,nadhani yeye ni miongoni mwa watoa ban,maana ana miaka zaidi ya 7 humu anatoa nyuzi daily
Name calling kwa sherianza JF ni ban
 
Ban Ni nini Haswa? Huwa Nawasikia Humu Mkisema mmepogwa Bam, Ila huwa sijui na Sitegemei kupigwa hio Ban yenu.
 
Niko JF since 2012 sikumbuki kama nimewahi pigwa ban.

Soon nitarudi kwenye ID yangu ya mwanzo kabisa.

Nimeipumzisha miaka 3/4 sasa
 
Back
Top Bottom