Tuwakomalie Polisi kuwarejesha watuhumiwa wakiwa hai

Anza kwanza kuwakomalia majambazi,vibaka, panya road waibe kwa staha na wasiue wanaowadhuru.
 
Acha ujinga, KATIBA na Sheria za Nchi haziruhusu POLICE kumuua mtuhumiwa aliye mikononi mwa POLISI amefungwa pingu.

Mahakama pekee ndo Ina mamlaka kuhukumu mtu KIFO.

Nikuulize swali: Ni KESI ngapi mahakama imehukumu mtu anyongwe na Rais anakwepa Kutia Saini?

Kwann Rais aogope kusain mtu anyongwe afu POLISI alazimishwe kuua, msiwape ndugu zetu POLISI LAANA 😠😠😠
 
Unauhitajika umoja wa hali ya juu sana...
 
Ili iweje kwa hao panya road na majambazi wenye mapanga na visu?
Naona anza kwanza kwa kuwauliza hao majambazi na panya road, kwa nini wanabeba hizo silaha?
Kwa nini wasiende kuiba bila kuiba mahali ambapo panaruhusiwa na katiba ya serikali?
[emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062]
 
Mtu yoyote anayeunga mkono binadamu mwenzake kuuawa kiholela Ni mpumbavu...
 

Hivi ni vigumu kuelewa kiasi hiki?

Japo si nadra kwa panya road na majambazi kubeba visu na panga, si sahihi kumshutumu awaye yote kwa kubeba kisu na panga.

Kubeba kisu au panga hakukufanyi wewe au awaye yote kuwa panya road au jambazi.
 

Kumbukumbu la Torati 19:21

21 Hampaswi kuwahurumia:i Uhai utatolewa kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

Upo uhakikaa gani kuwa waliotolewa uhai na polisi waitoa uhai?

Kumbuka mfanya biashara wa madini Mtwara, wafanya biashara ya madini Ifakara. Hawa waliporwa fedha na kutolewaxuhai na polisi.

Usiwasahau Lissu, Lijenje, Ben, Azory. Hawa ni wahanga wa mamlaka kama navyo kumbushwa mara lukuki na bwana RNA kuwa kuna wavaa makoti marefu meusi.

Kumbuka wa kwenye viroba. Orodha haina mwisho.

NInakazia: ipo tofauti kubwa baina ya watoa uhai na washukiwa.
 
Panya road ni lazima wauwawe ili kulinda maisha ya wengine.
Sheria na mahakama vimeshindwa kupunguza uhalifu, ukatili na mauaji yanayofanywa na vijana hao wa panya road.
 
Panya road ni lazima wauwawe ili kulinda maisha ya wengine.
Sheria na mahakama vimeshindwa kupunguza uhalifu, ukatili na mauaji yanayofanywa na vijana hao wa panya road.

Asemaye kuwa sheria na mahakama vimeshindwa ni nani mkuu?
 
Na majambazi tuwakomalie waibe ila wasiue raia.

Ungekuwa umesema na watuhumiwa wa ujambazi tumawakomalia waache utuhumiwa ungekuwa umejitendea haki zaidi.

Zingatia mada ni kuhusu washukiwa si majambazi wala panya road.
 
Tangu hii operation ya panya road ianze, umevurugika sana...lazma kila siku upost, kuna kitu sio bure!!
 
Issue hii inatuhusu sote,ukisema wahanga wakomalie ni pamoja nami na wewe.Jinsi ulivyoshauri ndivyo watesi wetu wapendavyo-Kutugawanya ili iwe rahisi kutushinda.Wanafahamu kwamba tukiunganisha Nguvu zetu pamoja tutawakomesha mazima.Asili ya mateso mengi wanayopitia wenyenchi hii ni Ukatili wa vyombo vya Dola na Watawala(CCM).
Kuna maandamano ya kupinga Ukatili/Unyama wa POLISI Duniani Jumatatu ya tarehe 03-10-2022.Tuanzie hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…