Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

NAGONA NA MZINGILE YA KEZILAHABI.je tutarudi na roho zetu BEN MTOBWA.BLACK HERMIT AU MTAWA MWEUSI.MPISHI MWENYE KIBYONGO,KIPOFU MWENYE MIWANI MIEUSI
 
Euphrace Kezilahabi
1. Roza Mistika
2. Dunia Uwanja wa Fujo

Faraji Katalambula

1. Simu ya Kifo
Mimi natamani sana kitabu cha ROSE MISTIKA,HEKAYA ZA ABUNWASI,MASHIMO YA MFALUME SULEIMANI,VITUKO VYA BULICHEKA.
Sijui mdau gani anaweza kunitonya wapi nitapata nakala ya riwaya/vitabu hivyo.
Vitabu hivyo tulikuwa twavisoma kwa mwanga wa vibatali,chai ya pipi,viatu vya maana vilikuwa ni chachacha ambavyo ni yeboyebo siku hizi.
Kisa sukari ilipanda ghafla na kilo moja kuuzwa kwa sh 2.00 za kitanzania,enzi hizo kiatu kwa dent ilikuwa anasa,chupi haikuwa ya muhimu na aliyekuwa nayo '007'alikuwa anaipandisha hadi juu ila kata k haikuwepo/////
Next time i will explain more fantastic true stories soon after independence,
I submit p,se////////////////////////////////
 
Vitabu vya JAMES HADLEY viko vingi sana niliwahi kuvisoma zaidi ya 75 na vile vya watunzi wa Kenya na Uganda,Malawi,Afrika magharibi n.k
Kama watoto wetu waangekuwa wadadisi kama sisi wangefika mbali sana,THE RIVER BETWEEN,NO BRIDE PRICE,THINGS FALL APART,SONG OF LAWINO AND OCHOL,MINE BOY,wale waliosoma language three uwanja wenu.
NOVEL:-ambazo bado ziko kichwani baada ya miaka 25 ni kama THE WHIFF OF MONEY,WHAT IS BETTER THAN MONEY,AN EAR TO THE GROUND,THERE IS HIPPY ON THE HIGH WAY,THE WAY THE COOKIE CRUMBLES,DOUBLE SHUFFLE,DO ME A FEVOUR,A CANE OF WORMS,THIS IS FOR REAL,MAKE THE CORPSE WALK,na nyingine nyingi sana zilitusaidia kujiamini katika midahalo kati ya shule na shule kwa kutumia zile bombastic kama "the situation is very cantankerous/cantankerousness.Dame with swushbuckling look,blonde and very odd.
Mkuu naomba kuwasilisha////////////
:doh: amigoooh...........
 
Ama zako ama zangu part 11 yake ikaitwa Sanda ya Jambazi - Hemmie Rajab.

Talaka ya Chozi- Hemed Kimwanga

Jamani nikiwa standard 3 nilianza kusoma kitabu cha Rosa Mistika kisha Kufa na Kupona na vingine vingi vilivyotolewa na Elvis Musiba (Will Gamba) na vingine vya Ben Mtobwa (Joram Kiango). hivi vitabu vilinifanya niwe na weledi wa kuyajua mambo mengi sana, nawashukuru sana watunzi wa enzi hizo.
 
Kufa na Kupona
Kikosi Cha Kazi
Njama

vyote Elvis Musiba.
 
1.Pesa zako zinanuka mnakikumbuka?(skumbuki katunga nani)
2.pia kuna kitabu cha Hofu
3.kuna kitabu cha Janga sugu la wazawa chake Gabriel Ruhumbika
 
Elvis Aristablus Musiba

Kufa na Kupona
Hofu
Njama
Pori la kijani
 
Alfu Lea Ulela
Visa vya Said Beneza
Bado Mmoja
Ubeberu Utashindwa:A S 41: na JK Kiimbila, kitabu matata sana
 
Wakuu, kuna kitabu nilisoma nikiwa std 3 miaka hiyo ya 80, kinaitwa NTEKO VANO MAPUTO ingawa sikukimaliza. Natamani nikitafute. Mtunzi alikuwa nani jamani?
Enzi zetu Sekondari za private hazikuwa deal kabisa kama hukufaulu kwenda shule ya Serikali ulilazimika wazazi wafoji ili urudie, siku hizi sekondari za private zinatafutwa kwa mamilioni!
Nashangaa eti siku hizi mtu anafaulu mtihani std 7 hajui kusoma wala kuandika. Watoto wa siku hizi wana bahati!
 
Sina hakika kama siku hizi akipatikana mtunzi mzuri akaandika riwaya kama za akina Mtobwa, Kiryamiti na Musiba, vijana wa siku hizi watavisoma. Maana inaonekana kama video zimebadilikabisha kabisa mfumo wa burudani.

Inaonekana siku hizi watu wamebebwa zaidi na hisia za mapenzi. Kwa kweli sina hakika kama tunaelekea wapi na utunzi wetu jamani. Watunzi wenyewe ndio akina Shigongo!!! Hakianani tasnia hii itapotea hivi hivi! Roho inaniuma.
 
Wadau, siku hizi moyo wa kusoma vitabu vya aina zote-vya Taaluma na Riwaya umepungua sana na imepelekea Watunzi wa Riwaya kutoandika tena vitabu. Leo nawakumbuka baadhi ya Waandishi/ Watunzi wa Riwaya wa Tanzania.

Hamie Rajab
1. Miujiza ya Mlima Kolelo
2. Dunia Hadaa



mi nataka sana sasa ndo muda muafaka wa kusoma vitabu kwangu kwa maana ntakuwa naelewa si kusoma kwa kujibu mitihani kunakitabu nakitafuta kinaitwa you can not hold a bible and a spear naweza pata wapi nielekeze jamani nina orodha ndefu sasa nataka niwe napata copy moja baada ya moja
Hiki chaitwa: "Is it Possible?" Maduka ya vitabu yanauza kitabu hiki. Kama uko Arudsha, tembelea KASE Bookshop!
 
Ni kweli kabisa kuhusu waandishi wetu wa vitabu vya hadithi. Nina swali moja ambalo ninaomba kama munaweza kuchangia, itanisaidia kujua.
Swali: Ni kitabu gani cha hadithi hizi kitafaa kuigizwa kwenye film za video. Naomba ushauri wenu

Ipan
 
Ni kweli kabisa kuhusu waandishi wetu wa vitabu vya hadithi. Nina swali moja ambalo ninaomba kama munaweza kuchangia, itanisaidia kujua.
Swali: Ni kitabu gani cha hadithi hizi kitafaa kuigizwa kwenye film za video. Naomba ushauri wenu

Ipan

Tafuta kitabu kinaitwa "Bado mmoja"
kitafaa kutengeneza detective movie.
Vitabu kama "kitanda cha mauti"; "Tuanze lini" na "Mpenzi- juzuu ya kwanza na ya pili" vyote vya Kajubi D mukajanga vitafaa kwenye mambo ya mapenzi pamoja na "theme" ya ukombozi wa mwanamke.
Mapenzi ya masharobaro yanaweza kuigizwa kwa kutumia kitabu cha John M.S. Simbambwene kinaitwa kivumbi uwanjani.
Masuala ya uvumilivu wa shida za maisha, kuteswa na mama wa kambo nk, tafuta kitabu kinaitwa " Mbutolwe mwana wa umma"
 
Ahsante Nanren kwa wazo lako, Nitavifuatilia vitabu hivyo....detective movie I believe can be very interesting licha ya kuwa technology kidogo inaweza kusumbua wakati wa kutengeneza, lakini ndiyo changamoto yenyewe inayoitajika. Inaonekana film za mapenzi na masuala ya uvumilivu wa maisha watu wengi watapenda zaidi au unaonaje?
 
KOSA LA BWANA MSA by Muhammed Sais Abdullah
FAILI MAALUM by Eddie Ganzel
JOGOO LA SHAMBA by eddie Ganzel
 
Back
Top Bottom