Hatimaye serikali ya awamu ya sita ilitangaza rasmi uwepo wa ugonjwa hatari wa Corona hapa nchini. Hii ikienda sambamba na kutolewa kwa maelekezo thabiti ya hatua gani za kuchukuliwa tunaposubiria kuwasili kwa chanjo.
Hatua hii ni njema kabisa ya kupongezwa na kila mzalendo na hasa kila muelewa.
Hata hivyo wamekuwapo wanaoendelea kushikilia misimamo isiyokuwa na mashiko kutokea awamu ile kuhusiana na huu ugonjwa. Wakihusianisha hatua hizi mpya za serikali na kiu tu cha mikopo kutoka kwa mabeberu.
Matokeo yake, hadi sasa takwimu za ugonjwa hazitolewi na mwitikio mzima wa hatua za tahadhari ni mdogo mno.
Tathmini ya kawaida inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu wanaopinga mtizamo huu mpya wa serikali, ni wale wale ambao pia wanapinga kurejelewa kwa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.
Wakati wanaounga mkono msimamo huu wa serikali, pia ndiyo wale wale wenye kuhitaji kurejelewa kwa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.
Kuna elements za wazi za ujinga kwenye kupinga hatua hizi dhidi ya Corona. Wakati kuna elements za ujinga na ubinafsi uliopitiliza kwenye kupinga suala la mchakato wa katiba mpya.
Bila shaka habari za kuanzishwa kwa kiwanda cha kutengeneza chanjo za Corona nchini, ni namna ya kujaribu kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa wajinga hao.
Ushauri wa bure kwa serikali inapohangaika kuwashawishi ndugu zetu hawa dhidi ya gonjwa hili:
"Serikali itangaze rasmi kusitisha jitihada zote za kupata mkopo wowote kuhusiana na ugonjwa huu au labda hata na kwa shughuli nyingine zozote ikibidi."
Ndugu zetu hawa hawaelewi kuwa mikopo huombwa tena kwa kunyenyekea. Ni fikra potofu kudhani kuwa pana mikopo mahali bwerere inayohitaji wakopaji."
Ni vyema serikali ikafanya hivyo huku ikitambua pia kwanini si sahihi sana nchi kuendekeza agenda zinazosukumwa na watu wenye uelewa mdogo (yaani wajinga).
Ninawasilisha.