#COVID19 Tuwatambue wanaohujumu vita dhidi ya Covid-19 nchini

#COVID19 Tuwatambue wanaohujumu vita dhidi ya Covid-19 nchini

Hatimaye serikali ya awamu ya sita ilitangaza rasmi uwepo wa ugonjwa hatari wa Corona hapa nchini. Hii ikienda sambamba na kutolewa kwa maelekezo thabiti ya hatua gani za kuchukuliwa tunaposubiria kuwasili kwa chanjo.

Hatua hii ni njema kabisa ya kupongezwa na kila mzalendo na hasa kila muelewa.

Hata hivyo wamekuwapo wanaoendelea kushikilia misimamo isiyokuwa na mashiko kutokea awamu ile kuhusiana na huu ugonjwa. Wakihusianisha hatua hizi mpya za serikali na kiu tu cha mikopo kutoka kwa mabeberu.

Matokeo yake, hadi sasa takwimu za ugonjwa hazitolewi na mwitikio mzima wa hatua za tahadhari ni mdogo mno.

Tathmini ya kawaida inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu wanaopinga mtizamo huu mpya wa serikali, ni wale wale ambao pia wanapinga kurejelewa kwa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.

Wakati wanaounga mkono msimamo huu wa serikali, pia ndiyo wale wale wenye kuhitaji kurejelewa kwa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.

Kuna elements za wazi za ujinga kwenye kupinga hatua hizi dhidi ya Corona. Wakati kuna elements za ujinga na ubinafsi uliopitiliza kwenye kupinga suala la mchakato wa katiba mpya.

Bila shaka habari za kuanzishwa kwa kiwanda cha kutengeneza chanjo za Corona nchini, ni namna ya kujaribu kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa wajinga hao.

Ushauri wa bure kwa serikali inapohangaika kuwashawishi ndugu zetu hawa dhidi ya gonjwa hili:

"Serikali itangaze rasmi kusitisha jitihada zote za kupata mkopo wowote kuhusiana na ugonjwa huu au labda hata na kwa shughuli nyingine zozote ikibidi."

Ndugu zetu hawa hawaelewi kuwa mikopo huombwa tena kwa kunyenyekea. Ni fikra potofu kudhani kuwa pana mikopo mahali bwerere inayohitaji wakopaji."

Ni vyema serikali ikafanya hivyo huku ikitambua pia kwanini si sahihi sana nchi kuendekeza agenda zinazosukumwa na watu wenye uelewa mdogo (yaani wajinga).

Ninawasilisha.
Siungi mkono hatua za sasa za kupambana na korona lkn naona kuna umuhimu wa katiba mpya acha watu watu watoe maoni yao.
 
Siungi mkono hatua za sasa za kupambana na korona lkn naona kuna umuhimu wa katiba mpya acha watu watu watoe maoni yao.

Uliona maneno haya: "asilimia kubwa?"

IMG_20210708_165347_312.jpg


Kuna na tathmini nyingine imeenda mbele zaidi kusema kwenye asilimia hiyo kubwa pia wengi wao wako kati ya makundi haya 4 pia:

IMG_20210708_150328_418.jpg


Nakazia hakuna aliyezuia mtu kutoa maoni. Haya ya kuzuiwa unayasoma wapi?
 
Uzuri wa corona inapita nao wale wanaoidharau, yenyewe haina shida hata kidogo ukiiheshimu.
Bado nakumbuka ile clip ya Polepole anaongea, sauti kama anaongelea kwenye chupa. Eti hii corona kama imeamua kukaa hapa Tanzania basi tunaitaka ikae kwa adabu. Haikuchukuwa muda ikaondoka na bosi wake! Kweli ujinga ni kitu kibaya. Corona inafanyiwa dhihaka?
 
Bado nakumbuka ile clip ya Polepole anaongea, sauti kama anaongelea kwenye chupa. Eti hii corona kama imeamua kukaa hapa Tanzania basi tunaitaka ikae kwa adabu. Haikuchukuwa muda ikaondoka na bosi wake! Kweli ujinga ni kitu kibaya. Corona inafanyiwa dhihaka?
Hata wewe nawe unaamini kuwa Jiwe kafa na corona?
 
Siyo tu naamini ila nilipata habari kabla hata hajafariki.
Bila ushahidi inabaki kuwa ni imani tu, kuna wengine walikuwa na imani kali kabisa kuwa Jiwe kachanja chanjo ya china kisirisiri ndio maana alikuwa haogopi corona yani kila mtu ana imani yake.
 
Na wakifa na UKIMWI muwe mnatangaza hivohivo, sio mnasingizia malaria ilimpanda kichwani
 
Yawezekana ni dalali wa mabeberu!! Hapo alipo kwanza huwezi kumkuta amevaa barakoa lakini maneno mengiii!!! Hakuna mtu anayemzuia kujiweka lockdown na kuchanjwa!! Asitupangie!!
Hapo vp?
 
Kapuku endelea kupambana na kuunganisha issue ya katiba ili upate wanaokuunga mkono,maana kwenye corona umechemsha.
Kila siku ulimtaka rais atoe tamko,Sasa tamko lilishatoka,Nani ajifunike mdomo apanuke moyo bila sababu.

Kapuku vipi kwenye Corona wewe ulishapoza siyo mjomba? Vipi rais hajatoa tamko?

Vipi mdomo bado umefunua? Moyo nao umesinyaa?

Kumbukumbu zenu bora kuku!

Cc: Jerusalem2006
 
Matope IQ yako iko chini Sana ndo nyie mliokuwa mnsoma mpaka jicho linakuwa jekundu Kama mchoma mkaa matokeo Sasa🤣🤣🤣
Matope IQ yako inasemaje?

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom