Tuwaze mrejereo: Hivi DP World ingeletwa na Magufuli ingepingwa?

Kwanza rekebisha uelewa wako. Bandari zote za Tanganyika zimenyakuliwa bila malipo. Hazijauzwa bali zimekabidhiwa kwa mwarabu milele bila ukomo.

Pili, acha kuwaandama wafu. Magufuli alishafariki siku nyingi. Usitake kumbambikia uchafu wako wa mikataba ya kitapeli.
 
Sasa kama bandari zote wamepewa Waarabu mbona hatuwaoni?
.
Wengine tunawangoja kwa hamu kubwa sana.
 
Kutokana na hili sakata la uporaji wa bandari za Tanganyika, ninawashauri Wazanzibari wajitahidi haraka sana wajitoe kwenye huu muungano feki.

Nionavyo mimi, endapo kutakuja kuibuka sintofahamu juu ya huu mkataba wa DP World, rais atakayekuwepo anaweza kuja kuiuza stone Town ya Zanzibar ili kuwalipa Wazanzibari madhambi na kufuru wanazotupitishia watanganyika bila ridhaa yetu.

Sisi tunachoona ni kuwa Wazanzibari wameamua kuuza rasilimali zetu kwa bei chee ili siku zijazo tusiwe na pa kushika.
 
Tungeipinga kama angeleta mkataba wa kishenzi kama huu.

Tulimpinga yule mwovu kwa mambo mengi tu.
 
naona huelewi kitu, au kama unaelewa, basi ni mwendelezo ule ule wa upotoshaji wa maksudi kabisa unaofanywa na baadhi ya watu kwenye sakata hili la Bandari kwa sababu wanazozifahamu wao.

Unalinganisha mambo ambayo ni tofauti kabisa; uchafuzi wa uchaguzi na ugawaji wa mali za nchi kwa watu toka nje kwa sababu wasizozielewa waTanzania. Utafanya mlinganisho gani hapo?

Unalinganisha Magufuli, ambaye pamoja na ukichaa wake, lakini kundi kubwa sana la waTanzania waliyaona baadhi ya mambo muhimu sana aliyokuwa akiyafanya waliyaelewa kuwa ni kwa manufaa ya nchi; halafu unamlinganisha huyo na Samia ambaye amejipambanua waziwazi kabisa kwamba yeye maslahi yake yapo kwenye kundi maalum la watu, ambao ndio wanaomhimiza kuingia kwenye mipango ya kuinajisi nchi hii.
Hapo kama unazo akili timamu utalinganisha vipi

Badala ya kuziona tofauti hizo zilizo wazi kabisa unaamua kukimbilia kwenye hitimisho potofu kabisa kuhusu sababu zinazowafanya watu wakatae uhujumu huu wa taifa lao, kwa vile anayeyafanya haya siyo Magufuli!

Hovyo Kabisa.
 




Kuna mifano haiwezekan, kwa hiyo hakuna sababu ya kuijadili
 
Sio kwa terms zile never ......bandari bagamoyo alikataa sababu miaka 100 senbuse hii endless forever ......power yote ile khaaass ujingaaa
 
Bro mheshimu basi Magufuli plz. Magufuli huu uchafu hakuna binadamu angweza kumpelekea acha tu kusain. Najua unakumbuka vizur alichofanya kwenye mkataba wa bandari ya bagamoyo mkuu. Hili la uchaguz lina mwisho mzee kila miaka 5 ila hili DP world ni nuksi ya milele
 
Mkataba usingekuwa wakindezi kama huu
 
Mkataba ni IGA kweli? Mbona umesainiwa upande mmoja Waziri na upande mwengine Mkurugenzi wa DPW. Umesoma sheria ndugu.
Watu walipeleka Bungeni wakati ulishasainiwa!
Kiilivyo makubaliano ya Bilateral na Multilateral yakishafikiwa, tunaleta Bungeni kujadili, kuridhia, then serikali ina sign.
 
Pamoja na mapungufu yake yote, ila Jiwe asingetuletea haya matope!! alikuwa mtetezi number moja wa raslimali zetu kwa kukataa mikataba ya hovyo !!

Kwa hili tusimhusishe kabisa.
 
wala asingeweza kufikiria kuleta ujinga kwenye rasilimali za Tanganyika, maana yeye alipenda kulinda rasilimali zetu, baada ya kuona mikataba ya ovyo ikulu, alituambia akaenda haraka kutunga sheria ya kulinda rasilimali za nchi ya mwaka 2017, sheria hiyo hiyo ya kulinda ya kulinda rasilimali za nchi samia kapeleka mswada bungeni ili isitumike kwenye baadhi ya rasilimali ikiwepo swala la bandari, yaani Magufuri hata kama angeleta bandari swala la win-win situation lingekuwa kwa Tanzania. ila mama kagawa nchi zawadi kwa wajomba ndio shida.
 
Isingekuwa na mkataBa kama huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…