Tuwe makini, nahisi hii mitandao ya simu haina ulinzi wa uhakika

Coincidence tu. Matapeli wanarusha sms kila mara, ilitokea wamerusha sms ukiwa umemaliza maongezi na mama yako.
Ndiyo wataje hadi bei ya Lita 5 nazotaka kuagiza? Wamejuaje kama na shida na Lita tano? Halafu muda huo huo nimetoka kumaliza mazungumzo ya kuuziwa Lita tano. Hapana nasisitiza Kuna kitu hakipo Sawa.
 
Probably hii ni halotel
 
Sitautaja mtandao ninao tumia ila nina mpango wa kuuhama.
Ni mitandao yote inafanyiwa surveillance kwa hio labda uanzishe mtandao wako mwenyewe yaan mitandao yote ipo chini ya uangalizi na Namba zote zilizosajiriwa kwa wale mabwana zinafuatiliwa hata upige chafya wanajua, kwa hio wanaofanya hivyo ni kule kule kwa wale mabwana Ila ukiwaambia km kawaida watasema sio wao
 
Natamani kusema kwamba wafanyakazi wa huko mitandaoni wanashirikiana na matapeli
Msiwapake matope mitandaoni ya simu,

Hawa jamaa matapeli wanachofanya ni kubet tu na kubahatisha namba tofauti tofauti..

Hivi mfano mtu akiandika sms kwa watu 200 "POLE SN KWA MSIMBA" ikaenda kwa watu 200 itakosa watu waliofiwa?
 
Msiwapake matope mitandaoni ya simu,

Hawa jamaa matapeli wanachofanya ni kubet tu na kubahatisha namba tofauti tofauti..

Hivi mfano mtu akiandika sms kwa watu 200 "POLE SN KWA MSIMBA" ikaenda kwa watu 200 itakosa watu waliofiwa?
Inawezekana kabisa, lakini vipi kwa mtu anayekutumia ujumbe mahususi kabisa na mazungumzo yako uliyetoka kuzungumza kupitia simu.?
 
Wala sio Kama unavyofikiria . Ipo hivi Kama atatuma message nyingi labda 3000 lazima Kuna nyingine zitaangukia kwa watu wenye mchakato wa kutumiana hela. Nisawa na wale watabiri wanaosema hapa naona mtu anasumbuliwa na UTI katika kundi la watu 200 lazima hao watu wawepo. Au anaweza kutuma message 5000 kuhusu Mtoto wako ameanguka shule katika Hilo kundi lazima message kadhaa ziwafikie wazazi na nyingine zinaweza kuangukia kwa watu ambao hawana hata mtoto. Hawa majamaa wanabahatisha tu lakini kumbuka kadri wanavyobahatisha kwa kutuma message nyingi lazima nyingine zitaangukia kwa walengwa
 
Uncle basi nitumie na mm ila unitumie kupitia account ya bank
 
Mbonaa tutakomaa mpk CCM watoke madarakani😔😔maaana n wizi wa wazi wazi kbs huu
Mimi Kuna mtu nilimtumia hela yaani namba ni yenyewe na jina lake ni lenyewe ila nilivyobonyeza OK meseji ikaingia kwenye Simu yangu " Umetuma kiasi cha shilingi 100,000/= kwenda kwa Mama Samia..." Nilidata sana....

Kila nikitaka kurudisha muamala yanakuja maandishi mekundu yenye herufi kubwa "ACHA USENGE"
 
ccm wanachukua hela zao za uwanachama. si hamtaki kuwa wanachama muichangie ada za uanachama. wamebinu mbwinu na kampuni za simu 😸
 
Inawezekana kabisa, lakini vipi kwa mtu anayekutumia ujumbe mahususi kabisa na mazungumzo yako uliyetoka kuzungumza kupitia simu.?
Unajuwa kama unaweza ukarecodiwa hata na unayefanya nae mazzungumzo?

Kwani zile connection za video za sex za watu wakiwa falagha zinavuja vp?pia kuna watu wa usalama pia wapo kazini.

Unapaswa uwe na tahadhari kwa kila jambo mkuu.

Niamini mimi mkuu hawa jamaa wana bet namba na ujumbe muhimu ambao ktk watu 50 lazima atapatikana mmoja.

Jiulize mfano wewe kwa siku umeahidi watu wangapi kuwatumia pesa?
Halafu uone sms inasema ile pesa weka huku huweziingia kwenye mfumo? Ukapigwa pesa?

Hizi sms mwanzo watu wamepigwa sn.
 
Bado hujanijibu swali langu, nimetoka kuzungumzia ununuzi wa pikipiki Kisha nakata simu halafu Napokea ujumbe unaohusiana na pikipiki muda huo huo. Najaribu kumrudia hewani muuzaji anasema hajatuma ujumbe wowote Kwangu na makubaliano yetu ni kama awali.

Hizo SMS za kutuma kwa mtu aliyekua na miahadi ya kumtumia mtu pesa ni kawaida lakini si kawaida kwa kulenga kabisa maudhui mazima ya mazungumzo yaliyopita hivi punde.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…