Tuwe na adabu Kwa Jakaya, yaani wewe kijana wa misungwi , mbinga, kibondo unajua mipango ya nchi kuliko jakaya hadi umzodoe?

Tuwe na adabu Kwa Jakaya, yaani wewe kijana wa misungwi , mbinga, kibondo unajua mipango ya nchi kuliko jakaya hadi umzodoe?

Hakika Kikwete apewe haki yake.
Ameongea ukweli kuhusu SGR.
Salary Slip aliweka thread hapa JF mwaka 2013 JK akizungumzia mpango wa ujenzi wa SGR.
Hivi shida yake nini bado anajitokezatokeza majukwaani! Basi akachukue fomu 2025 anadi sera zake agombee kama ameshindwa kutulia Msoga, tamaa nyingi kama mkewe, aibu!!
 
Hakuna anayempa credit samia ktk mradi wa SGR,maana ameukuta tayar uko hatua nyingi za ujenzi,tutampongeza kwa kumalizia palipobakia.
Yeye mzaramo kama angekuwa mwaminifu angekumbuka pia hatukumnyima pongezi ktk BRT maana aliiacha iko miles kadhaa mbele.
Tutamkumbuka pia ktk shule za kata za sekondari hatuna hiyana.

Kama kupanga na kutekeleza ni jambo moja,panga kupata mtoto na mkeo,miezi 9 baadae azaliwe muhindi,ndio utaelewa.
 
jakaya legacy pekee ameacha ni majizi na utani. hakuna cha maana alichofanya zaidi ya kujilimbikizia mali.
Ambaye hajajilimbikizia mali ni nani? Usitake watu wafunguke mengi ujue.

Kikwete ndiye Rais aliyefanya maisha yakawa na nafuu kuwahi kutokea nchi hii.

Pesa ilionekana mtaani hata kwa mtu wa chini aliweza kukidhi mahitaji yake pasipo tatizo kabisa.

Yeye ndiye mwanzilishi wa miradi mingi unayoiona leo kuanzia SGR, Mwendokasi, daraja la Kigamboni, Saraja la Ifakara, ujenzi chuo kikuu cha UDOM ambacho ndicho kikubwa kwa eneo lote la Afrika Mashariki na Kati.

Acha chuki zisizo na maana wewe.
 
Hakuna anayempa credit samia ktk mradi wa SGR,maana ameukuta tayar uko hatua nyingi za ujenzi,tutampongeza kwa kumalizia palipobakia.
Yeye mzaramo kama angekuwa mwaminifu angekumbuka pia hatukumnyima pongezi ktk BRT maana aliiacha iko miles kadhaa mbele.
Tutamkumbuka pia ktk shule za kata za sekondari hatuna hiyana.

Kama kupanga na kutekeleza ni jambo moja,panga kupata mtoto na mkeo,miezi 9 baadae azaliwe muhindi,ndio utaelewa.
Irrelevant example.
 
Viongozi wetu wakuu tokea uhuru kila mmoja amejitahidi kwa namna na maarifa yake kutekeleza majukumu yake , japo ki % Kila mmoja wanatofautiana. Viongozi wanapigania kuongeza Pato la ndani na hata kukopa nje Kwa ajili ya miradi mikubwa na midogo ,Moja ya pesa alizotafuta Mh Kikwete ni mradi wa Maji Mwanga, Same na Korogwe Toka BADEA kazi ilianza wakati anaondoka madarakani, sijui mchawi nani ila upigaji na uzembe mkubwa umefanywa, hata Mh Magu na ukali wake wote mitano yake ya kwanza mradi haukufanikiwa, awamu ya sita Mh Mpango alitoa ahadi kuwa Maji yasipotoka by June anaachia umakamu, thubutu mbona alivyoona June imefika na Maji hamna kaenda kuzindu hewa Hadi Leo si Same Wala Korogwe waliopata hata glasi moja ya Maji, ninichotaka kuweka wazi hapa nikuwa matokea ni mchakato anaweza aanzishe kiongozi huyu amalizie mwingine vzr ama aanzishe na anayefuata anyongelee mbali mradi na kazi za mwanzilishi zisionekane. Ila kwasasa Kuna mtu ni mcharo, tutajua vzr baadaye!!!
 
Kutokana na kushindwa vibaya kwa utawala wale, inatosha kusema ALITAMANI, hakujaribu wala kuthubutu!

Hakuna asiyejua kuwa Mwalimu alipanga na kutamani kuhamia Dodoma...mnajua nini kilitokea.

Jakaya hana jema alilofanya kwa watanganyika.
Hiyo sentensi ya mwisho imenifikirisha sana
 
wanajua wap hao. utadhani walisoma faili na kujua kitu. mim naskiaga wakizodoa ila hawajui kuwa mafaili yana minitiwa na kufanyiwa kaz.na j.k ana mchango
 
Mzee Kikwete alirahisisha upatikanaji wa passport na vijana wanaozamia SA alisema wakirudishwa wasipelekwe mahakamani ni watafutaji hao mambo za network ya bara bara pia alijitahidi binafsi siwezi kumsema Vibaya wacha apumzike mambo za biashara wacha afanye kama ana mchongo ila mbaya zaidi wao wakifanya zitaenda sawa kwa kuwa hakuna tra atagusa kuwauliza kwa chochote...
 
Ifike hatua tuwe na adabu,
Jakaya kikwete ndio Rais mstaafu tuliyenaye, huyu ni msaada Kwa nchi yetu, angeamua kua kama uhuru anaweza lakini katulia na amebaki akiambiwa panda pikipiki wala hajali,
Nawapa hizi dondoo chache, fedha za SGR hadi dodoma aliacha ametafuta Jakaya, ile kijazi interchange alitafuta jakaya, tena magufuli akavuruga ramani, ilikua ni bonge la kitu,
Upanuzi wa barabara kimara hadi mile moja fedha alitafuta jakaya, daraja la tanzanite pesa aliacha jakaya,
Jakaya kawa muwazi kua mipango ilianza Kwa mkapa, akaihanikiza, magufuli kaisimamia, kosa lake ni lipi?
Nchi haijengwi na mtu mmoja, nchi inajengwa Kwa kupokezana, uongozi ni mbio za vijiti ni kupokezana huyu anakimbia hadi hapa na mwingine hadi kule.
Viongozi wetu wana mazuri na mabaya yao na kila mmoja anakitu alifanyia nchi yake tuwe na heshima,
Acha akili za zamani. Unaelewa maana ya utandawazi? Ulitaka waongee wa Mkoa gani ndio ujue wanajua?
Yeye ni nani hata asisemwe?
Kama alikuwa na uwezo wa kujenga kwa nini asijenge baada ya kuachiwa na mtangulizi wake kama alivyosema?
 
Back
Top Bottom