Tuwe na akiba ya maneno kuhusu IGA na DP World

Tuwe na akiba ya maneno kuhusu IGA na DP World

Kuna nguvu nyingi inatumika na CCM kuharalisha mkataba huu, sasa hivi imeonekana mkataba huu ni agenda ya chama cha CCM, Kwenye utekelezaji wa sera zao, kwahiyo CCM wameamua kulibeba, na kuondoa lawama kwa wote waliongia mkataba kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkataba huu ata kama ni agenda ya CCM, kitu kikubwa nchi hii ni ya vyama vingi vya siasa na vyama vyote vinawanachama ambao nao ni Watanzania pia, lakini mkataba ambao CCM mnataka utekelezeke kila Mtanzania anao sio siri tena, vipengele vipo wazi kabisa, sehemu ambazo Watanzania wanahoji kila msomi anavielewa kabisa, sasa kuna hoja gani nyuma ya pazia ambayo inatakwa kulazimishwa??

Nani ana wasiwasi na Dk. Nshala kwenye uweledi wa sheria, nani ana wasiwasi na Prof. Shivji kwenye kutafsiri sheria, nani hana imani na Tanzania Law Society, kama chama cha mapinduzi mnahitaji ushauri nani mwingine aje ili muelewe????

Ni kitu gani hakieleweki??....kila msomi analia na mkataba na anataja tatizo liko wapi....inaniuma sana kwasababu ya matumbo na nafasi za kuchaguliwa na Raisi, mnaamua baadhi kusema na kushinikiza mkataba ni mzuri ili kulinda matumbo yenu, mnasubiri MAMA aondoke mje tena mumchape na mkataba huu huu kwenye majukwaa kama mnavyofanya sasa kwa magufuri, ila kama kuna kiongozi atapata bahati kusoma andiko ili nataka ujue kuubariki mkataba ni kujiaibisha wewe mwenyewe, kuaibisha uweledi wako, na wenye akili tunajua we ni mpiga dili, mfia tumbo aupo kwa ajili ya vizazi vyako vijavyo, wewe sio mzalendo, wewe ni mbinafsi.

Kama nitakuwepo hai, nitakuwa wa kwanza, kufungua kesi mahakamani kwa kiongozi wa sasa akistaafu alafu aje na kitabu, akiomba radhi kwa kushiriki kuingia na kutekeleza mkataba huu, utakuwa ni unafiki uliotukuka.
 
Back
Top Bottom