Tuwe na utaratibu wa kuziweka wazi taarifa kificho muda unapofika

Content yako inajieleza soma vizuri
Ametoa kitabu kinachoelezea mengi maovu ya JPM katka utawala wake! Mengi kati yake si mageni.. Yalikuwa ni tetesi ambazo zilijadiliwa kwa siri na kwa uoga mkubwa! Hakuna chombo chochote cha habari ama mwandishi binafsi alijaribu kuziweka wazi kama alivyofanya Eric sasa hivi..!
Umeelewa maana yake?
 
Labda nikuulize swali kuondoa mtanziko.....ww unaamini kilichoandikwa na huyo muandishi?
 
Ametoa kitabu kinachoelezea mengi maovu ya JPM katka utawala wake! Mengi kati yake si mageni.. Yalikuwa ni tetesi ambazo zilijadiliwa kwa siri na kwa uoga mkubwa! Hakuna chombo chochote cha habari ama mwandishi binafsi alijaribu kuziweka wazi kama alivyofanya Eric sasa hivi
 
Wazungu kuna kitu wanaita classified information! Hizi ni taarifa kificho zinazofahamika kwa kaliba fulani ya watu ndani ya mamlaka ya nchi..
Hizi huwa ni taarifa za siri zinazowahusu viongozi wa nchi mambo yahusuyo nchi ambazo kama zikivuja kwa wakati huo nchi inaweza kuingia matatani
Huitwa classified information kwakuwa duniani hakuna siri ya mtu mmoja milele.. Hivyo huwa na kipindi maalum cha mpito mpaka zipoe na kuwa na madhara madogo ndio hutolewa public.. Hii husaidia sana kuwakata kalima wale wote ambao wangezivujisha kwa ladha na vionjo vyao kabla ya mamlaka!
Afrika na Tanzania na pengine mataifa mengi mengine hayana huo utaratibu.. Na hii hutoa nafasi kwa watu binafsi.. Kuzitafuta taarifa husika na kuzovujisha kwa Jamii kupitia maandiko ya vitabuni machapisho mitandaoni nknk!
Tumeunza mwaka 2025 na machapisho ya mwandishi Erick Kabendera mmojawapo wa wahanga wa utawala wa JPM

Kitabu chake hicho kimezua mijadala ya kila aina.. Kuna ambao wamefikia kuishauri mamalaka kukifungia kwakuwa kinamchafua marehemu na kuitia doa ccm na serikali yote
Mimi nashauri kiachwe.. Na mijadala mingi zaidi iruhusiwe na ikiwezekana taarifa zile zipewe majibu ya kweli na ya hhakika
Kwa kufanya hivyo serikali itakuwa imejitua mzigo mkubwa sana na kufunga ukursaha wa hayo mazonge yote ya utawala wa JPM
Jaribio lolote la kutaka kukizuia kitabu cha Kabendera na kuahirisha tatizo ambalo linakuja kuibuka tena na kwa nguvu zaidi katika kipindi ambacho hakina afya sana!

Suala lililopo ni kwa kiasi gani mambo aliyoyaandika Kabendera ni sahihi.
Kwa maana siyo kila kitu kikiandikwa na mtunzi ni sahihi. Kwa maana kuna usemi unasema... "asiyesoma magazeti/vitabu ni mjinga. Lakini anayeamini kila anachosoma kwenye magazeti/vitabu ni mjinga hata zaidi".
 
Wazungu kuna kitu wanaita classified information! Hizi ni taarifa kificho zinazofahamika kwa kaliba fulani ya watu ndani ya mamlaka ya nchi..
Hizi huwa ni taarifa za siri zinazowahusu viongozi wa nchi mambo yahusuyo nchi ambazo kama zikivuja kwa wakati huo nchi inaweza kuingia matatani
Huitwa classified information kwakuwa duniani hakuna siri ya mtu mmoja milele.. Hivyo huwa na kipindi maalum cha mpito mpaka zipoe na kuwa na madhara madogo ndio hutolewa public.. Hii husaidia sana kuwakata kalima wale wote ambao wangezivujisha kwa ladha na vionjo vyao kabla ya mamlaka!
Afrika na Tanzania na pengine mataifa mengi mengine hayana huo utaratibu.. Na hii hutoa nafasi kwa watu binafsi.. Kuzitafuta taarifa husika na kuzovujisha kwa Jamii kupitia maandiko ya vitabuni machapisho mitandaoni nknk!
Tumeunza mwaka 2025 na machapisho ya mwandishi Erick Kabendera mmojawapo wa wahanga wa utawala wa JPM
Ametoa kitabu kinachoelezea mengi maovu ya JPM katka utawala wake! Mengi kati yake si mageni.. Yalikuwa ni tetesi ambazo zilijadiliwa kwa siri na kwa uoga mkubwa! Hakuna chombo chochote cha habari ama mwandishi binafsi alijaribu kuziweka wazi kama alivyofanya Eric sasa hivi

Kitabu chake hicho kimezua mijadala ya kila aina.. Kuna ambao wamefikia kuishauri mamalaka kukifungia kwakuwa kinamchafua marehemu na kuitia doa ccm na serikali yote
Mimi nashauri kiachwe.. Na mijadala mingi zaidi iruhusiwe na ikiwezekana taarifa zile zipewe majibu ya kweli na ya hhakika
Kwa kufanya hivyo serikali itakuwa imejitua mzigo mkubwa sana na kufunga ukursaha wa hayo mazonge yote ya utawala wa JPM
Jaribio lolote la kutaka kukizuia kitabu cha Kabendera na kuahirisha tatizo ambalo linakuja kuibuka tena na kwa nguvu zaidi katika kipindi ambacho hakina afya sana!
SIku nikipigwa na baa la njaa naiba huu uzi na nyuzi kadhaa zenye kushabihiana na huu natengeneza mbuku mkubwa mithili ya ule wa JERICHO Kisha najiita Jasusi na jina la kitabu kitakuwa 'UJUE UJASUSI KINDAKINDAKI', naanza kuuupromote mbuku huo kupitia JF na najua wengi wenu mtaununua.

Je mpaka hapo nitakuwa sijapiga pesa?
Naombeni ni u langu.
 
😂😂😂😂😂😂
 
Mkuu, claassified huwa zina kawaida ya kuwa classified kwa kuanzia angalau miaka 30. Ulitaka wakina Kabendera wasubiri miaka yote hiyo ndiyo waje na hizo taarifa. Pia Kandera siyo mtu wao wa ndani bali ni Mwandishi wa habari za uchunguzi.
Kuhusu Tz kuwa na sheria za classified, mbona hizo sheria zipo!

Kabendera ni muongo na ni mchumia tumbo. Kama unavyosema kwamba yeye siyo mtu wao. Ni kweli kabisa, yeye hata hana uwezo wa kusogelea classified areas. Hivyo yeye atategemea apewe habari na mtu/watu ambao hatujui kama wao pia wana hisia hasi kumuelekea JPM kama yeye Kabendera.

Yeye ni muandishi tu. Hata hiyo unavyosema ni muandishi wa habari za uchunguzi. Ni habari zipi za uchunguzi amewahi kuandika zaidi ya habari za kuichafua serikali na nchi kwa ujumla?

Hii "dis publication" against JPM ni ya kuipuuza. Kwa maana imejaa hisia na habari zisizothibitishwa au uzushi. Pia hakuna mtu yeyote duniani ambaye ana upande mmoja tu wa uzuri pekee au ubaya pekee. Binadamu daima, ana pande mbili, nazo ni ubaya na uzuri. Muandishi hataji zuri hata moja la JPM. What a biased book
 
Kwa Tanzania hii?? I don't expect this to happen!

Kwa tawala zenye itikadi za siasa za Kikomunisti/Ujamaa hawana utamaduni huo wa kufanya De-classification ya taarifa zao za Siri (Classified Information). Hii ni kutokana na sababu nyingi Sana, lakini sababu kuu ikiwa ni kuficha Uovu na Uhalifu ambao umefanywa na Utawala husika.

Kumbuka: Uhai au existence ya utawala wowote ule wa Kikomunisti/Ujamaa hutegemea na suala zima la kuwaangamiza au kufanyia madhila na uhalifu wale wapinzani wao au wakosoaji wao.
Case Study: Rejea suala zima la kuanguka kwa Utawala wa Shirikisho la Urusi ya zamani (USSR) na KGB pamoja na Ushetani uliokuwa ukifanyika kwa Wananchi kwa kutumia genge hilo la KGB.

Msipende kuambiana uongo. Once Classified Information always classifieds Information. Duniani kote bila kujali mrengo wa kisiasa, lazima kuwe na Classified information and Classified areas. Haya mambo yapo kwa ajili ya uthabiti na usalama wa nchi. Hata kwa level yako binafsi huwezi kuwa unatoa kila kitu unachofanya. Hiyo ninkwa ustawi, heshima na usalama wako. Hata kwa nchi ni vivyo hivyo. Hawawezi kukupa kila kitu ukijue. Kuna mambo wataficha. Ndiyo maana akina Snowden muannzilishi wa wiki leak aliingia matatani na serikali yake kwa kukiuka hili.

Lingine kuhusu kuvujisha siri. Nchi nyingi zikitaka kuvujisha taarifa hizo inafanya kwa mtindo wa conspiracy. Inatolewa taarifa kina, lakini yenye uwalakini.

CC: Mshana Jr
 
Je kuna mifano kwa Tanganyika? Miaka 30 inategemea na ukubwa wa jambo. Kuna mengine ndani ya miaka 10 huvujishwa hadharani.. Kikubwa kinachoangaliwa ni impact ya taarifa husika
Mfano ile ya CDF Mstaafu Mabeyo.
Kuhusu mchakato wa kifo cha Mh. Rais JPM ilikuwa classified Information.
 
Msipende kuambiana uongo. Once Classified Information always classifieds Information. Duniani kote bila kujali mrengo wa kisiasa, lazima kuwe na Classified information and Classified areas. Haya mambo yapo kwa ajili ya uthabiti na usalama wa nchi. Hata kwa level yako binafsi huwezi kuwa unatoa kila kitu unachofanya. Hiyo ninkwa ustawi, heshima na usalama wako. Hata kwa nchi ni vivyo hivyo. Hawawezi kukupa kila kitu ukijue. Kuna mambo wataficha. Ndiyo maana akina Snowden muannzilishi wa wiki leak aliingia matatani na serikali yake kwa kukiuka hili.

Lingine kuhusu kuvujisha siri. Nchi nyingi zikitaka kuvujisha taarifa hizo inafanya kwa mtindo wa conspiracy. Inatolewa taarifa kina, lakini yenye uwalakini.

CC: Mshana Jr
Lingine kuhusu kuvujisha siri. Nchi nyingi zikitaka kuvujisha taarifa hizo inafanya kwa mtindo wa conspiracy. Inatolewa taarifa kina, lakini yenye uwalakini.🤔🙇🏿‍♂
 
Msipende kuambiana uongo. Once Classified Information always classifieds Information. Duniani kote bila kujali mrengo wa kisiasa, lazima kuwe na Classified information and Classified areas. Haya mambo yapo kwa ajili ya uthabiti na usalama wa nchi. Hata kwa level yako binafsi huwezi kuwa unatoa kila kitu unachofanya. Hiyo ninkwa ustawi, heshima na usalama wako. Hata kwa nchi ni vivyo hivyo. Hawawezi kukupa kila kitu ukijue. Kuna mambo wataficha. Ndiyo maana akina Snowden muannzilishi wa wiki leak aliingia matatani na serikali yake kwa kukiuka hili.

Lingine kuhusu kuvujisha siri. Nchi nyingi zikitaka kuvujisha taarifa hizo inafanya kwa mtindo wa conspiracy. Inatolewa taarifa kina, lakini yenye uwalakini.

CC: Mshana Jr
KABENDERA ANADAI BEN SANANE ALIUAWA NA 'BWANA MKUBWA'!

Mwishoni mwa mwaka 2020, nilipata ujumbe mzito kutoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa mtu wake mmoja ambaye jina lake linatunzwa. Rais alimtuma kwangu akiniomba nishawishi Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Tundu Lissu waridhie wabunge wanawake 19 waapishwe kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Nilijitahidi kufurukuta kueleza Rais ajue kuwa sikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wala mimi sikuwa na ushawishi wowote katika jambo lile. Lakini Rais aliamini kuwa Lissu na Mbowe watanisikiliza mimi. Lilikuwa jambo gumu sana kwangu kumshawishi mtu yule aniamini mimi. Ahadi niliyoahidiwa na ambayo pia CHADEMA wangepewa kama 'dili' lile lingefanyika ingali katika kilindi cha moyo.

Nakiri kuwa baada ya ombi la Rais la kunitaka niwashawishi Lissu na Mbowe kushindikana, zoezi la uapishwaji liliendelea na mimi nikajua kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini hoja la andiko hili sio jambo hili.

Mwezi Januari 2021, alitumwa tena kwangu mtu yule yule. Safari hii haikuwa kunishawishi ili niwashawishi Mbowe na Lissu, bali ilikuwa ni kunitisha niachane na harakati, la sivyo basi nilikuwa nachungulia mauti. Nilikuwa nimetoka kuitangazia dunia kuwa maisha ya Mhe. Lissu yalikuwa hatarini na ndipo Ubalozi mmojawapo ukamchukua na kumpeleka nje ya nchi.

Kwa hiyo jibu langu kwake lilikuwa moja tu: "Mwambie Mheshimiwa kuwa akitaka aniue, lakini Askofu hatarudi nyuma"! Vitisho vya aina hiyo niliwahi kupewa na Polisi mmoja nikiwa Central Polisi, Dar es Salaam mwezi mmoja kabla Rais Magufuli hajafariki dunia.

Baada ya majibu yale, yule mtu alitetemeka na ikabidi aropoke mambo mengi sana ambayo sio sehemu ya andiko hili kwani kwa sasa Bado mambo yale ni 'classified information'! Baada ya hapo nikaanza kupata taarifa nyingi ambazo zilinitisha na kunipatia matumaini.

Siku moja nilitafutwa na mtu mmoja ambaye ni mzima na kada wa CCM. Kwa kuwa mtu huyo tunaheshimiana na kwa kuwa aliaminishwa ya kuwa mimi nilikuwa natumiwa na 'mabeberu'; ilibidi nimueleze pia baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanamzunguka Rais. Nilifanya hivyo ikiwa kinga yangu kwani nilijua kuwa ataelewa mazingira yangu na hivyo ataweza kupangua hoja dhaifu dhidi yangu akiwa katika 'Pango la Wakilindi'. Aliishia kunikodolea macho na ndipo tukaagana akiwa kama mtu asiyeamini.

Lakini kabla mtu huyo hajaondoka, aliniuliza: "Wewe umejuaje habari hizi'? Nikamjibu kuwa: "Mimi ni mskofu wa mnyororo na pia mimi ni askofu wa kiapo"! Mambo haya yaliaminiwa pia kwangu chini ya kiapo kwa hiyo nisingeyasema hadharani wakati ule na hata sasa. Hapa sio mahali pake kuelezea kisa cha askari aliyeacha kufanya ibada baada ya kushiriki kuwaua watu na baadaye kumbukumbu za watu wale zikawa zinamjia na kuharibu akili yake.

Mambo haya ni ya kitubio na kwa hiyo mtu ye yote atakayemuendea Mchungaji (Padri) au Askofu kwa kitubio, jambo lile linabakia katika kifua cha mtubishaji, anayetubu na Mungu.

Taarifa za kuchapishwa kwa kitabu cha Erick Kabendera zimeanza kusambaa kwa kasi sana mitandaoni siku ya leo tarehe 3 Januari 2025. Kitabu kinaitwa: 'In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist'. Nimesikiliza mahojiano ya Erick Kabendera kuhusu kitabu hicho. Nimeanza kufuatilia maudhui ya kitabu. Mengi ya mambo anayojadili ni sehemu ya yale niliyojulishwa kama 'sisi Askofu'! Ila sikutarajia mambo yale yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu. Ujasiri wa Kabendera unaivuka mipaka ya Nshamba na Kamachumu.

Ninaamini watu ambao walinishangaa kwa nini mimi nilijitoa muhanga kwa ajili ya kutetea haki nchini sasa wataanza kuelewa baada ya kuona na kusoma kitabu cha Erick Kabendera. Taarifa nyingi zilizofikishwa katika kilindi cha moyo wangu ziliishurutisha nafasi yangu kuchukua ili kupaza sauti na kutetea pale nilipoweza. Lakini pamoja na uropokaji wangu, mambo ambayo yalitiwa muhuri (sealed) katika moyo wangu yameamriwa na dhamiri iliyo kuu ili yasiyoke.

Kitabu cha Kabendera kitasaidia katika mambo muhimu. Kwamba tukisome na kumjua Rais Magufuli nje ya uelewa uliojulikana. Baada ya hapo, tuone kuwa alikuwa binadamu kama sisi na mwenye mapungufu na kisha tumsamehe. Kikubwa, kama jamii tutafute njia ya kuponya ikiwemo kuondoa vimelea au masalia ya yale aliyoayaasisi ambayo hayakuwa mazuri na hili itawezekana kama tutasoma na kuielewa sura ya mwisho ya Kitabu cha Kabendera.

Kitabu hiki kinaposambazwa na kusomwa ni vizuri tujue kuwa kinayahusu maisha fichika ya Rais Magufuli na sio maisha ya familia na ukoo wake. Hatuhitaji kwa namna yeyote kuwaona ndugu hata familia kama sehemu ya mambo aliyoyafanya kama Rais kwani nao walikuwa ni washangaaji kama sisi.

Mwisho, natoa wito kwa viongozi wa dini walio karibu na familia ya Ben Sanane na familia ya Azorly Gwanda kuzifikia kwa ajili ya huduma ya kiroho. Kupitia kitabu cha Erick Kabendera na mahojiano yake ni rasmi sasa ya kuwa umma umejulishwa kuwa watu hao hawapo pamoja nasi katika maisha haya.

Hekima iliyo ndani ya kilindi cha moyo wa Rais Samia inaweza kumsaidia afanye nini kwa ajili ya familia hizo. Bila shaka, CHADEMA itatafuta namna njema ya kuhitimisha kwa heshima kwa kumkumbuka Ben, mwanachama na Msaidizi maalum wa Mhe. Mbowe. Kadhalika, Gazeti la Mwananchi litaona pia namna ya kulihitimisha l kwa heshima ya Azorly, aliyekuwa mtumishi.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam
FB_IMG_1736029999803.jpg
, 3 Januari 2025; saa 2:00 usiku
 
Msipende kuambiana uongo. Once Classified Information always classifieds Information. Duniani kote bila kujali mrengo wa kisiasa, lazima kuwe na Classified information and Classified areas. Haya mambo yapo kwa ajili ya uthabiti na usalama wa nchi. Hata kwa level yako binafsi huwezi kuwa unatoa kila kitu unachofanya. Hiyo ninkwa ustawi, heshima na usalama wako. Hata kwa nchi ni vivyo hivyo. Hawawezi kukupa kila kitu ukijue. Kuna mambo wataficha. Ndiyo maana akina Snowden muannzilishi wa wiki leak aliingia matatani na serikali yake kwa kukiuka hili.

Lingine kuhusu kuvujisha siri. Nchi nyingi zikitaka kuvujisha taarifa hizo inafanya kwa mtindo wa conspiracy. Inatolewa taarifa kina, lakini yenye uwalakini.

CC: Mshana Jr
Siyo kweli hata kidogo kwamba taarifa yoyote ile inapokuwa ni taarifa ya Siri (Classified information) Basi ni LAZIMA iwe Siri daima milele, Siyo kweli kuhusu suala hili.
Zipo baadhi ya nchi huwa waba utaratibu wa kuzianika wazi taarifa zao za Siri baada ya kupita muda Fulani. Mamlaka za Ujasusi za Nchi zao zimekuwa zikifanya kazi hii, hata baadhi ya taarifa zingine nyeti kabisa pia zimekuwa zikiwekwa wazi hadharani kwa umma (De-classifying the Classified Information). Taarifa nyeti kuhusu Operesheni za kijasusi walizofanya zinawekwa wazi na kila mtu mwenye uhitaji anaweza akawa na access nazo.

Mfano ulio hai, CIA waliwahi kuweka Wazi taarifa yote kabisa ya iliyokuwa ya Siri hapo kabla kuhusiana na Mpango na Mikakati ya Operesheni ya Kupindua Serikali ya Sultan wa Zanzibar, Bw. Jamshind ambaye amefariki wiki iliyopita huko Oman.
Taarifa ile imeeleza kwa uwazi kabisa juu ya Operesheni ya Mapinduzi ya Serikali ya Sultan ilivyokuwa hapo Mwaka 1964, taarifa hiyo ilitolewa miaka ya hivi karibuni, lakini hapo kabla iliwekwa kuwa ni Siri kubwa ya CIA kwa zaidi ya miaka hamsini.
Aidha, hata baadhi ya taarifa zingine nyeti Sana za Mipango ya CIA juu ya Operesheni za Siri za kuwaua baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi zingine au Watu Maarufu duniani walioonekana kuwa ni kikwazo kwa Utawala wa Marekani pia zimekuwa zikiwekwa wazi kabisa. Mathalani, taarifa nyeti za missions za majaribio ya kumuua aliyekuwa Rais wa Cuba, Fidel Castro, mauaji ya Patrice Lumumba wa Congo DR (Zaire), Mwanamuziki Bob Marley, n.k, ziliwahi kuwekwa hadharani,
 
Hapo katumika vibaya
When it suits you ego and agenda anasema ukweli. Anapogusa usipopataka "katumika vibaya".Kuna kutumika vibaya na kutumika vizuri.Once a liar always a liar.Huwezi kuchuja unachokitaka wewe usikie na kikigusa maslahi yako basi anatumika.
Kipi kinazuia awe anatumika moja moja kwani umesema hapo ametumika vibaya?
 
Siyo kweli hata kidogo kwamba taarifa yoyote ile inapokuwa ni taarifa ya Siri (Classified information) Basi ni LAZIMA iwe Siri daima milele, Siyo kweli kuhusu suala hili.
Zipo baadhi ya nchi huwa waba utaratibu wa kuzianika wazi taarifa zao za Siri baada ya kupita muda Fulani. Mamlaka za Ujasusi za Nchi zao zimekuwa zikifanya kazi hii, hata baadhi ya taarifa zingine nyeti kabisa pia zimekuwa zikiwekwa wazi hadharani kwa umma (De-classifying the Classified Information). Taarifa nyeti kuhusu Operesheni za kijasusi walizofanya zinawekwa wazi na kila mtu mwenye uhitaji anaweza akawa na access nazo.

Mfano ulio hai, CIA waliwahi kuweka Wazi taarifa yote kabisa ya iliyokuwa ya Siri hapo kabla kuhusiana na Mpango na Mikakati ya Operesheni ya Kupindua Serikali ya Sultan wa Zanzibar, Bw. Jamshind ambaye amefariki wiki iliyopita huko Oman.
Taarifa ile imeeleza kwa uwazi kabisa juu ya Operesheni ya Mapinduzi ya Serikali ya Sultan ilivyokuwa hapo Mwaka 1964, taarifa hiyo ilitolewa miaka ya hivi karibuni, lakini hapo kabla iliwekwa kuwa ni Siri kubwa ya CIA kwa zaidi ya miaka hamsini.
Aidha, hata baadhi ya taarifa zingine nyeti Sana za Mipango ya CIA juu ya Operesheni za Siri za kuwaua baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi zingine au Watu Maarufu duniani walioonekana kuwa ni kikwazo kwa Utawala wa Marekani pia zimekuwa zikiwekwa wazi kabisa. Mathalani, taarifa nyeti za missions za majaribio ya kumuua aliyekuwa Rais wa Cuba, Fidel Castro, mauaji ya Patrice Lumumba wa Congo DR (Zaire), Mwanamuziki Bob Marley, n.k, ziliwahi kuwekwa hadharani,

Yaa inategemea pia aina ya secrets.
 
Kuna vistatement vingivingi vyenye kutia shaka

Kwa mfano, siamini eti Vice President alitishia kuresign kwa sababu eti kuna siku JPM aliibukia kwa madame SSH usiku mnene akiwa kavaa Pajama

Tetesi za VP kudaiwa kutaka kuresign zilisikika kipindi flani na sababu haikuwa hiyo aliyoitaja Kabendera

Kwani VP na President wanakaa compound moja mpaka amfikie mida hiyo akiwa katika hali aliyoieleza?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom