Tuwe objective: Mbowe ana sababu gani za kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA

Ninachoona kwenye mkutano mkuu Mbowe atamsifia na kumwunga mkono Lissu,sidhani kama Mbowe atagombea ila anaweza kuwa makamu mwenyekiti. Ila nachoombea kama wote watagombea nafasi moja basi wote uchaguzi uwe wa haki na ukweli ingawa naona Mbowe atashinda tu
 
..mabadiliko gani ataleta Lisu, mifumo iliyomyima haki zake ni ile ile inapambana na chadema, mabadiliko aliyoahidi TLS alipochaguliwa kuwq Rais wa TLS alitimiza?
 
Ila Mbowe hajatangaza kugombea
 
..ilani ya ccm na Mbowe wapi na wapi, Lisu hana jipya lolote ni maneno tu, hana huo uwezo kuongoza chama kikafanikiwa..TLS chini yake ilifanikiwa? Taja mapya aliyofanya TLS..kuongoza chama sio mambo ya ahadi tu, uwezo unao?
 
Mbowe anafaa uenyekiti ila kwa mazingira ya sasa Lissu anafaa zaidi kuliko Mbowe.
 
..mabadiliko gani ataleta Lisu, mifumo iliyomyima haki zake ni ile ile inapambana na chadema, mabadiliko aliyoahidi TLS alipochaguliwa kuwq Rais wa TLS alitimiza?
Mabadiliko ya katiba ya cdm, na uendeshaji ikiwemo kuondoa upendeleo usio na tija. Sijui alichoahidi huko TLS, hivyo siwezi kulisemea hilo. Hata hivyo urais wa TLS ulikuwa wa mwaka mmoja, ni ngumu kufanya mabadiliko serious hasa ya kitaasisi kwa kipindi kifupi hivyo. Hiyo mifumo mibovu itaondoka kwa kuidai sio kwa mijadala ya kitapeli iitwayo maridhiano.

Kwa maneno marahisi tutamuhukumu Lisu baada ya kupata nafasi hiyo, na sio kwa hizi nongwa zako. Mbowe yeye ameshakaa kwa miaka 20, aliyofanya yanatosha, sasa ni muda wa yeye kukaa pembeni na kupisha wengine. Kuna ambacho hakieleweko hapo?
 
Hata kama Sio Lisu basi awe mtu mwingine maana chadama ni Chama kikubwa kina rasilimali watu wengi ambao wanaweza kushika nafasi ya Mbowe na kuleta ufanisi mkubwa pengine kuliko Mbowe.Kama mbowe Anang'ang'ania kuendelea kuwa mwenyekiti kuna mambo mawili makuu;
1.Anaamini kuwa Chama hakina watu wenye sifa za kuwa wenyekiti,Zaido ya yeye tuu.of which ana justify kuwa Chama ni dhaifu Kwani hakina rasilimali wari wakutosha kulishika dola.Self Point of contradiction.
2.Au anaamini kuwa kuna watu wana sifa za kushika nafasi yake lakini haachii Kwa sababu ana maslahi binafsi na Chama na wala si maslahi ya umma kama anavyowahadaa Watanzania
 
Sio shida

Lissu kugombea sio sababu za kuanza kutukana mwingine

Wote wakigombea hakuna haja ya kutukanana,afterall wote mnajenga chama kile kile

Huu mwendo wa wafuasi wa Lissu kutukana mgombea mwingine sio sahihi

Sana sana tunazidi haribu chama chetu,acheni wagombea walete sera zao mpige kura

Matusi na ku baguana sababu ya umri ni namna fulani ya ukichaa hivi,tena watu wa chama kile kile kimoja

What a shame
 
Hii ni miandiko ya CCM au manamba wake
Maana CCM ukitaja udhaifu wao na kuahidi kufanyia kazi basi wao huona ni matusi makubwa sana.

Ili tusikuite manamba taja matusi ya Lissu kwa wagombea wengine
 
Kasema haondoki ,Chama cha mkwe wake analinda maslahi.
Hayo makao makuu ya Chama ni nyumba ya dadaake kitambo tu.
Sasa .nataka aende wapi?
 
Hii ni miandiko ya CCM au manamba wake
Maana CCM ukitaja udhaifu wao na kuahidi kufanyia kazi basi wao huona ni matusi makubwa sana.

Ili tusikuite manamba taja matusi ya Lissu kwa wagombea wengine
Sijakuelewa

Nikijaribu kukuelewa,umemaanisha kwamba mimi ni CCM?

Kua serious aisee

Uzi wako unamnanga na kumtusi Mbowe,haina haja

Kwanini hawa wagombea wote wawili wakagombea na mkapiga kura akapatikana mmoja?

Hii kuzonga zonga mgombea mmoja sio sahihi,nakutuhumu wewe kwa kufanya hili

By the way mimi sio CCM...ni Chadema through and through,and Im not here to prove my membership to you
 
Huwezi kunielewa, kusema uzi wangu nimemtukana Mbowe ni ushahidi kuwa uzi huu umekuzidi kimo na huna uwezo wa kuujadili. Tafuta mtu hapo karibu akujengee uwezo
 
Shiriki uchaguzi mkuu. Mbowe ana haki na uwezo wa kugombea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…