Hakuna rais wa Tanzania aliyewekewa kesi mahakamani kutakiwa kuhalalisha uteuzi wake wa kuwa mgombea urais, kibaya zaidi kesi kawekewa na mwanachama wa CCM.
Samia hata akishinda urais, urais wake utagubikwa na wingu la kukosa uhalali.
Tuukubali ukweli kuwa nahodha ni mchanga sana. Sikiliza kutokuwepo coherence kwa hotuba zake. Angalia wasaidizi wake wa wakaribu angalia waandalizi wa kampeni.
Kimsingi tuna safari kubwa.
Tuiombee nchi yetu. Ni wazi hakuna maono ya kiuongozi tena. Ni vurugu tupu.
Matoeko ya serikali dhaifu, ni ustawi wa matajiri kwa gharama ya umaskini kwa wengi.
Kukosekana kwa maono;
-tatizo la ajira litazidi kuwa kubwa zaidi.
-rushwa, ufisadi na mikataba ya unyonyaji ndio wakati wake sasa,
-matumizi mabaya ya fedha kodi za watu ni haki ya msingi ya watawala.
-wateso, utekaji, na mauaji ya wakosoaji ndio uzalendo
Kuna mtumishi wa umma Kaambiwa kuna uwezekano Kuanzia next year kupanda daraja lazima afanye Kwanza Mtihani.Alitamka hilo duuuh nikasema kweli watu wamevurugwa.