Tuwe wawazi: Hivi chai na kahawa unapendelea kunywa nini?

Tuwe wawazi: Hivi chai na kahawa unapendelea kunywa nini?

Naona ni usiku ila lengo langu la kuleta uzi naomba niliweke wazi. Wengi tunapenda kunywa maji ya moto asubuhi ama jioni, ili kupasha tumbo kabla ya chakula kigumu.

Wengi machaguo yetu huangukia kwenye maziwa, chai na kahawa. Sasa naomba kujua, wewe binafsi chaguo lako ni kahawa au chai?

Na kwa nini?
Ukiweka na supu ntarudi
 
Hukosi shavu dodo mkuu
Shavu gani tena mtani🤣🤣 ni mazoea tu
nilipata kula sana chapati utotoni every day for like 5 years kwa hiyo vitu vya ngano siviwez

uji unatengenezwa nyumbani sinywi uji road na wala sipendi kununua maandaz au vitu wanavyopika huko barabarani. Mwaka wa kumi toka nihamie hapa manzese sijawahi nunua chochote hata kitumbua. .
 
Kuna mtu anatuuziaga spices
Anasema kuna hii kahawa ya Moshi, ni nzuri sana.
Sijawahi ijaribu bado
Nunua kahawa iandae mwenyew hutojutua utaona tofauti kubwa sana na hizi za kununua
bahati nzuri huwa nachukua nyumbani Rombo huko sema bi mdachi ananiandalia. Kisha naend chukua hapo home

nyumban kuna nyumbu zinapiga kahawa hatare. .
 
Shavu gani tena mtani🤣🤣 ni mazoea tu
nilipata kula sana chapati utotoni every day for like 5 years kwa hiyo vitu vya ngano siviwez

uji unatengenezwa nyumbani sinywi uji road na wala sipendi kununua maandaz au vitu wanavyopika huko barabarani. Mwaka wa kumi toka nihamie hapa manzese sijawahi nunua chochote hata kitumbua. .
Uji daily lazima utoke shavu 😂
Ni lazima yan.

Me kitaa bado nanunua mtori na chapati 1 😜
 
Kuna mtu anatuuziaga spices
Anasema kuna hii kahawa ya Moshi, ni nzuri sana.
Sijawahi ijaribu bado
Kahawa ya moshi inanukia nikienda home nitaiba kidogo nikuleteee maana wazee wanauza😀
 
Ginger tea all the way. Faida ni nyingi kwa sisi wana weightloss. Nachemsha tangawizi tu. Kikombe kimoja asubuhi, kimoja jioni. Visceral fat inapungua plus siku nzima nakua very active.
 
Mimi kahawa hapana, ninamwaka toka niache kutumia kahawa Kuna siku niliweka kahawa nyingi nikanywa hivyohivyo moyo ulianza kudunda kwa nguvu Hadi nausikia ndo ikawa mwisho wangu.

Chai ya rangi SI sana ila iwe na tangawizi na kashagwala.

Tea masala ndio Kila kitu, the best tea masala nilikunywa Zanzibar I felt the aroma of those spices.
In Dar es Salaam I had the best tea masala at Paparoti one cup for 8,000 the mint flavor was waoooh!
 
Sasa hilo ni kosa lako. Hutakiwi kutumia in excess.!

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom